Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adebayor kuja Yanga, labda kuwa mfadhili

Muktasari:

Mambo mengine huhitaji kuingia darasani ili kuyaelewa au kuyajua, yanahitaji akili ya kawaida tu ya mwanadamu.

AKILI ya kuzaliwa ina umuhimu wake kama ilivyo akili ambayo tunatengezewa darasani. Binadamu amepewa uwezo wa kutumia akili yake ya kuzaliwa ili kujiongoza kwa mambo ya kawaida.

Mambo mengine huhitaji kuingia darasani ili kuyaelewa au kuyajua, yanahitaji akili ya kawaida tu ya mwanadamu.

Mathalani, watu wengi wanaotapeliwa huwa wanashindwa kutumia akili ya kawaida tu kujua kwamba wanatapeliwa. Mfano mzuri ni mtu anapokubali kutoa fedha kwa mtu mwingine eti azizalishe zaidi.

Kuna mambo mengi ukiyasikia mitaani jinsi watu wanavyotapeliwa au kudanganywa unashangaa, ilikuwaje mtu akaibiwa au kutapeliwa kwa staili hiyo, alishindwa kutumia akili yake ya kawaida.

Unawezaje kuamini habari unayoambiwa kwamba mshambuliaji wa timu ya taifa ya Togo, Emmanuel Adebayor ana mpango wa kusajiliwa na Yanga ya Dar es Salaam?

Hata kama kwa sasa hana klabu, lakini katika hali ya kawaida uwe mwandishi au msomaji unaweza kuamini vipi kuwa Adebayor anafikiria kuja kuchezea Yanga?

Utajiri wa Adebayor unatajwa kuwa ni zaidi ya Pauni25 milioni, ambazo ni sawa na Sh60 bilioni. Mshahara wake akiwa Manchester City na Tottenham ulikuwa Pauni 170,000 (sawa na Sh350 milioni) kwa wiki. Mshahara huo ni kwa wiki si kwa mwezi. Maana yake kwa mwezi alikuwa anaondoka na zaidi ya Sh 1.2 bilioni za Tanzania.

Jumla ya mishahara ya wachezaji wote wa Yanga ambayo wanalipwa kila mwezi, bado haijafika mshahara wa wiki moja wa Adebayor akiwa Manchester City na Tottenham.

Ni rahisi kusema kuwa Adebayor kafulia, lakini lazima ifahamike kuwa hata kama amefika kiwango hicho, klabu yoyote atakayojiunga hawezi kukosa mshahara wa pauni 100,000 (Sh 220 milioni) kwa wiki.

Akiwa amechezea Arsenal, Manchester City, Tottenham na Crystal Palace zote za Ligi Kuu England, ni matusi kutaka kumhusisha mchezaji huyo na Yanga? Narudia tena ni matusi makubwa.

Akiwa amezaliwa Februari 26, 1984, bado mchezaji huyo si mzee, ingawa ni kweli kisoka umri umeanza kumkimbia, lakini bado kiwango chake kinaweza kuwa kucheza Ligi Kuu England na ligi nyingine zote za Ulaya na tena kwa sasa ana nafasi kubwa ya kutengeneza fedha katika Ligi Kuu China. Aache kwenda China aende Yanga? Ni matusi.

Waliotaka kuwaaminisha Watanzania kwamba mchezaji huyo anafanya mazungumzo na Yanga ambayo hata hivyo hayakuwepo walifanya kashfa kubwa, lakini hata wao wamejishusha thamani.

Nimezitaja klabu za England tu bila kutaja klabu nyingine alizozichezea kama Metz na Monaco za Ufaransa na Real Madrid ya Hispania hata kama ilikuwa kwa mkopo, lakini tukumbuke kuwa Adebayor alikuwa mchezaji bora wa Afrika mwaka 2008.

Adebayor ameichezea timu ya taifa ya Togo na mafanikio makubwa ilikuwa mwaka 2006 wakati timu hiyo iliposhiriki fainali za Kombe la Dunia na imekuwa ikishiriki fainali za Mataifa ya Afrika mara kwa mara ikiwamo mashindano ya mwaka huu nchini Gabon.

Sababu kubwa inayomfanya Adebayor kutangatanga, si kiwango cha uwanjani ila ni tabia zake nje ya uwanja ambazo zimekuwa zikiathiri mpaka ‘kambi za klabu’ anazochezea.

Baada ya kuona habari hiyo ya Adebayor ‘kufanya’ mazungumzo na Yanga ambayo hata hayakuwepo, niliamini kwamba anataka kuinunua Yanga, lakini nikasema nalo haliwezekani kwa sababu Serikali ni kama imepiga marufuku klabu za Jangwani na Msimbazi kuuzwa.

Nikafikiria kuwa labda Adebayor aje kuwa mdhamini wa Yanga, lakini nikajikuta sina jibu la uhakika, adhamini kwa faida gani ambayo ataipata.

Jibu pekee ambalo nimelipata ni kuwa labda azungumze na viongozi wa Yanga wamuelekeze jinsi ya kupanda Mlima Kilimanjaro na si nje ya hapo.

Mambo mengine yote kila mtu atumie akili zake za kawaida. Adebayor hawezi kucheza Yanga, Simba wala Azam.

Akifika miaka 40, miaka saba baadaye kwa shingo upande anaweza kwenda kumalizia soka lake Qatar au nchi nyingine za Kiarabu zenye fedha nyingi, lakini kumuhusisha na Yanga si kwamba ni matusi tu, ila dharau kwa soka letu.