Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Geay anaandaa mwili kwa raundi 20

UKIFIKA mkoa wa Arusha mwezi Mei ni kipindi ambacho kunakuwa na baridi kali sana ambayo kwa wale ambao hawana kazi za lazima hujificha ndani, lakini wengine wanakuwa hawana jinsi kwa kuwa ni lazima watoke.

UTASHANGAA MTONYO alioupata mwanariadha GEAY baada ya kuwa mshindi wa pili

Hata hawa wanaotoka hujidhatiti vilivyo kwa kuvaa makoti makubwa na wengine sweta nzito kuhakikisha kuwa wanakuwa kwenye hali nzuri ya usalama wa kulinda afya zao.
Lakini kwa wengine kipindi hiki huwa fursa kwao na ndicho ambacho wanakipenda sana kwa kuwa kinakuwa na faida kubwa sana kwa kazi zao au biashara ambazo wamekuwa wakizifanya kwa kuwa zinataka kuwe na baridi kali.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa wanariadha wengi ambao wamekuwa wakipenda kufanya mazoezi kwenye mazingira yenye baridi kali kuliko maeneo yenye joto, wanaamini kuwa huku wamekuwa wakifanya mazoezi yao vizuri, lakini ndiyo maandalizi yao huwa sahihi kwa kuwa wanapokwenda kushiriki mashindano mbalimbali makubwa, huenda kwenye nchi zenye joto kali.
Mwanaspoti hivi karibuni lilitua mkoani Arusha kwa ajili ya kufanya mahojiano na mwanariadha bora zaidi hapa nchini kwa sasa Gabriel Gerald Geay, ambaye amekuwa akifahamika zaidi kwa jina la Geay.

Haikuwa kazi rahisi kutokana na mazingira yalivyokuwa na wakati mwingine mwenyewe alishangaa kuiona timu ya gazeti hili ikiwa kwenye mazingira yale.
Baada ya kufika Arusha tuliwasiliana na Geay ambaye alitueleza kuwa itakuwa vizuri kama tutafanya mahojiano hayo Arusha mjini ikiwa ni baada ya kutoka mazoezini asubuhi, lakini tuliona itakuwa vizuri kama tutakwenda hukohuko anapofanyia mazoezi ili kuona pia maandalizi yake huwa yanakuwaje wakati anajiandaa na mashindano makubwa.

Hakutaka hilo kwa kuwa aliona itakuwa ngumu kwetu kwenda kwa muida ambao anafanya mazoezi kutokana na baridi kali ambayo ipo kwenye eneo hilo.
“Nafikiri ni vizuri tukakutana mjini, kwa kuwa mazoezi huwa naanza asubuhi sana, wakati mwingine saa moja na shida hapa ni kwamba kuna baridi kali sana kwa kuwa ndiyo mazingira ambayo ninapenda kufanyia mazoezini, lakini kama mnaona kuwa mnaweza kufika karibuni, lakini mjiandae kwa kubeba makoti ya kutosha.

Mwanaspoti latua Iliboru mapema sana:
Kukuwa na ukungu na baridi kali, nilifika kwenye uwanja wa Shule wa Iliboru ambao upo mlimani, kwani kabla ya kufika hapo tulikwea vilima vya kutosha na baada ya dakika kadhaa kutoka mjini tulifika na kukuta kundi kubwa la wanariadha likifanya mazoezi eneo hilo.

Ni ngumu kuwa kwenye maeneo kama Dar es Salaam na kukutana kuna wanariadha wengi namna hivyo, kwa hesabu ya haraka walikuwa wanariadha 86 ukiwa ni mchanganyiko wa wanaume na wanawake huku wakiwa wamejigawa kwenye timu tofautitofauti, nyingine ilikuwa na wanariadha watano, nyingine kumi na nyingine 12, lakini wengine walikuwa mmojammoja.
Kulikuwa na makocha wanaume kwa wanawake  ambao kila mmoja alikuwa ana saa maalumu kwa ajili ya kulinda muda wa wanariadha wakiwa wamekaa kikundi kimoja wanajadiliana.
Ukiachana na Geay, mwanariadha mwingine maarufu ambaye alikuwa kwenye kundi tofauti ni Fabian Joseph ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya riadha ya Tanzania kwa vipindi tofauti.
Geay aandaa mwili kwa raundi 20

Pale uwanjani tulimkuta Geay akiwa tayari ameshaloa mwili mzima kutokana na mazoezi ambayo tulimkuta ameshafanya na kwa haraka alizunguka uwanja wa Ilboru kwa raundi 20 kabla hafanifuata na kusema:
“Mambo vipi, nilikuwa naweka mwili safi kabla sijaanza kufuata programu ya kocha, hivyo naomba mnisubiri kama saa mbili hivi nitakuwa nimemaliza,” alisema.

Makocha wawaita, kazi yaanza

Baada ya dakika mbili makocha waliwaita wanariadha wote na kuwagawa kulingana na mbio ambazo wamekuwa wakikimbia, wengine walitakiwa kushuka na kupanda milima na wengine walitakiwa kuzunguka uwanjani lakini kwa muda maalumu ambao walikuwa wanapangiwa.

Makocha wao pamoja na matroni ambao walikuwa wamejipaga wakiwa na saa kila mmoja alikuwa akisimamia kundi lake na wanariadha wale walipokuwa wakifika sehemu ile walikuwa wanaelezwa kuwa wamekimbia kwa sekunde au dakika ngapi.
Iikuwa rahisi kila kundi lilipokuwa likifika kwenye kona ambayo makocha hao wapo kusikia wakisema 68, 73, 61, 69 71, hizi zilikuwa ni sekunde ambazo mwanariadha ametumia kuzunguka uwanja wa Ilboru kukiwa na baridi kali, mwisho kila mmoja alielezwa kuhusu mazoezi yake ya siku hiyo.
Lakini kwa makocha wale ilikuwa rahisi kwao kumwamisha mwanariadha mmoja kutoka kundi moja kwenda lingine kutokana na uwezo wake wa siku husika.
Geay amaliza baada ya saa 2

Baada ya kupita saa mbili, Geay alikuwa mmoja kati ya wanariadha wa mwanzoni kabisa kumaliza programu ya kocha wake Thomas Tlanka ambaye alimueleza kuhusu maendeleo yake ya siku hiyo, baada ya hapo alimuomba kuja kufanya mahojiano nasi ambapo ilimlazimu kubadilisha nguo kabla ya kuanza mahojiano kutokana na utaratibu ambao amejiwekea.

Aibuliwa na Paul Wema
Geay ambaye ana umbo kama la wanariadha wakubwa duniani anasema yeye ni mzaliwa wa Manyara ambapo amekuwa chini ya maadili mema ya wazazi wake, ambapo alipata elimu ya msingi na sekondari na baada ya hapo alifanikiwa kwenda kusomea utumishi wa Umma, hivyo kama siyo kuwa mwanariadha basi angefanya kazi hiyo ambayo alikuwa anaipenda.

“ Mimi tofauti na watu wengine wengi nilianza riadha nikiwa kijiji kwetu kabisa mkoani Manyara, katikati pitapita zangu niliwahi kukutana na watu wanakimbia, nilijaribu kuuliza hawa wanafanya nini kwa kuwa nilikuwa mdogo sana nikaelezwa kuwa ni wanariadha, ghafla nikaanza kuvutia na fani hiyo.
“Lakini baadaye nikaanza kufuatilia kuhusu wanariadha wakubwa duniani na nikafahamu kuwa ni fani nzuri na ina fedha nyingi sana, nikaanza kufanya mazoezi peke yangu, huku nikiwa natamani kujiona siku moja nakuwa mwanariadha mkubwa.
“Hata nilipokuwa shule ya msingi niliendelea kupenda mchezo huu na kushiriki mashindano mbalimbali ya shule ikiwemo mashindano ya shule za msingi Umitashumta.

“Lakini kama ilivyo bahati kwa watu wengine wengi, nilikutana na rafiki yangu ambaye tulikuwa tunafanya majukumu mbalimbali tukiwa huko nyumbani, tukiwa tunachunga mifugo na shughuli nyingine anaitwa Paulo Wema, huyu baba yake alikuwa anafahamu sana kuhusu riadha, hivyo siku moja akamfuata na kumwambia kuwa anataka kuwa mwanariadha.
Geay anasema baada ya kijana huyo kumweleza baba yake, mzazi huyo ambaye alikuwa anafahamu sana kuhusu mchezo huo alimwambia anatakiwa kutafuta watoto wenzake wawili ili waungane pamoja kwa ajili ya mazoezi ndiyo anaweza kuwa mwanariadha mzuri kuliko kufanya peke yake.

“Alinifuata na kunieleza kuhusu kile alichoelezwa na baba yake na kuanzia hapo akawa anatupa mwelekeo wa nini cha kufanya, akawa anatueleza tunatakiwa kukimbia umbali gani, yaani kila programu tukawa tunapata kwake.
Akawa ananishauri ananielekeza nini natakiwa kufanya yaani kila kitu nilikuwa napata kutoka kwake kila wakati wakati anakuja kule nyumbani, na hatimaye nikaweza kufikia kwenye malengo ambayo nimefikia sasa.


Ashiriki Marathoni akiwa na miaka 12
“Baada ya kufanya mazoezi ya kutosha chini ya baba yake Wema nilialikwa kushiriki half Marathon ambayo ilikuwa inajulikana kama Babati Half Marathoni ambapo alimaliza akiwa ameshika nafasi ya nne na kujiona kuwa sasa amekuwa anaweza kupambana kwenye mbio kubwa hii ikiwa ni mwaka 2014.
Geay anasema baada ya kufanya vizuri kwenye mbio hizo, alishauriwa na watu wengi akiwemo baba yake Wema kuwa anatakiwa kushikilia hapo kwani baadaye atakuwa mwanariadha mkubwa duniani.
Anasema aliendelea na moto ule hata  baada ya kwenda shule ya sekondari kwani alifanya mazoezi kwa bidii na kushiriki mashindano mbalimbali ya shule  ambapo alifanikiwa kufanya vizuri kwenye kila hatua, aliendeleza moto huo pia akiwa chuoni ambapo aliendelea kuwashangaza wengi kutokana na uwezo wake wa juu wa kukimbia na kushinda mashindano mengi aliyoshiriki. Desemba 2014, Geay alienda Angola ambapo alishiriki marathoni kilomita kumi ambapo kiwango kidogo namba 17.

Lakini sijali kuhusu hapa kwani kwangu hii ilikuwa kama daraja kubwa sana la mafanikio ya leo, nilijifunza mambo mengi kuhusu riadha na wanariadha kwa ujumla na kuanzia hapa nilijisemea kuwa hakika siku moja mimi nitakuwa mwanariadha mkubwa.
Akutana na wanariadha wa kimataifa
Geay anasema baada ya hapo aliendeleza harakati zake ambapo baadaye aliondoka na kujiunga na chuo cha Utumishi wa Umma baada ya kumaliza
“Nikiwa Chuoni mkoani Singida, nilikutana na wanariadha wengi wa kimataifa ambao walikuwa wakifanya mazoezi nikiwa naungana nao kwa muda wangu wa ziada, hawa naweza kusema kuwa ndiyo kati ya watu ambao walinipa msingi mzuri sana hadi kufikia hapa nilipo sasa,” alisema mwanariadha huyo tajiri Tanzania.