Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sitaki tena Urais – Sehemu ya 14

RAIS 14 Pict

UTANGULIZI

Rais Shanga na maafisa wake walisimama kando ya helikopta na kuangalia kazi iliyokuwa ikifanywa na wanajeshi hao.

Mkuu wa jeshi la ulinzi na mkuu wa jeshi la polisi walikuwa wakisimamia zoezi hilo na walipomuona Rais Shanga walimfuata.

Wakuu hao walimpigia saluti Rais Shanga na kupeana naye mkono.

“Mnaendeleaje na zoezi hili?’ Shanga akawauliza uso wake ukiwa umefadhaika.

“Tunaendelea kwa taabu kwa sababu moto unawake na hatuwzi kuuzima” Mkuu wa jeshi la ulinzi alimjibu Shanga na kuongeza.

SASA ENDELEA


“Tunachopenda kukwambia ni kuwa miili ya watu wote waliokuwa kwenye ndege, wakiwemo marubani wawili na wafanyakazi wa ndani ya ndege, imepatikana.”

“Hakuna aliyepatikana akiwa hai?”

“Hakuna tuliyemkuta akiwa hai.”

“Kama miili yote imepatikana, ipakiwe na kupelekwa Maloto.”

“Hilo ndilo zoezi ambalo tutalianza hivi sasa.”

Rais Shanga alishuhudia zoezi la upakiaji wa miili ya watu waliopata ajali, miili mingine ikiwa imeungua vibaya. Mwili wa waziri wake wa mambo ya nje ulikuwa miongoni mwa miili iliyopakiwa kwenye helikopta ya jeshi.

“Kazi ya kukitafuta kisanduku kinachorekodi mwenendo wa ndege tutaifanya kutakapopambazuka. Kwa muda huu kiza kinasumbua,” Mkuu wa Jeshi la Polisi alimwambia Rais Shanga wakati helikopta iliyopakia miili ya watu iliporuka.

“Mjitahidi kiweze kupatikana.”

“Tutajitahidi, mheshimiwa, na tunaamini kitapatikana.”

Baada ya kuzungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Rais Shanga alipakiwa kwenye helikopta pamoja na waziri wake wa mambo ya ndani na maafisa wake wengine. Walirudishwa Ikulu ya Maloto.

Asubuhi kulipokucha, Shanga alitangaza siku tatu za maombolezo kutokana na ajali ya ndege iliyotokea usiku uliopita. Akaliambia taifa kuwa ajali hiyo ilikuwa pigo kubwa kwa taifa la Kamisa.

Saa tatu asubuhi kulifanyika zoezi la kuitambua miili ya marehemu, na serikali ikatangaza kuwa marehemu hao watazikwa kitaifa.

Mazishi yalifanyika siku iliyofuata. Baada ya taratibu zote za mazishi kukamilika, taifa likawa kwenye maombolezo ya siku tatu.

Kisanduku cha kurekodi mwenendo wa ndege kilipatikana asubuhi ya siku iliyofuata baada ya usiku ule ilipotokea ajali. Siku ya pili yake, kikasafirishwa kuelekea Uingereza kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kujua chanzo cha ajali.

Lakini siku ya nne yake, Shanga aliamshwa tena usingizini muda kama ule alioamshwa ilipotokea ajali ya ndege.

Kuna nini tena? Akajiuliza huku akiinuka kutoka kwenye kitanda. Aliwasha taa na kuketi kitandani. Tangu ashike mamlaka ya urais, ilikuwa nadra sana kupigiwa simu usiku akiwa amelala. Na anapopigiwa, kunakuwa na jambo la dharura sana.

“Hello!” akasema baada ya kuunyakua mkono wa simu.

“Mheshimiwa, kuna tukio la ajali mbaya ya treni lililotokea usiku huu.” Sauti ikasikika kutoka upande wa pili wa simu.

“Ajali ya treni imetokea wapi?”

“Ni treni iliyoondoka saa mbili usiku huu kuelekea miji ya bara. Imeacha njia na kupinduka.”

“Imepinduka eneo gani?”

“Imepinduka katika kijiji cha Mtiti, nje kidogo ya jiji la Maloto.”

“Mabehewa mangapi yameanguka?”

“Mabehewa saba yaliyokuwa yamejaa abiria yameanguka. Treni ilikuwa na mabehewa kumi na matano.”

“Kuna watu waliopoteza maisha?”

“Inakadiriwa abiria wengi watakuwa wamepoteza maisha.”

“Hili ni balaa sasa. Juzi ndege, leo treni. Kulikoni?”

“Mheshimiwa, kama ulivyosema, ni balaa limeingia nchini kwetu.”

“Hatua gani zimeshachukuliwa hadi sasa?”

“Vikosi vya uokoaji vimeshapelekwa na baadhi ya viongozi wamekwenda kusimamia zoezi hilo.”

“Sawa. Mtaendelea kunifahamisha kinachoendelea.”

Baada ya kuzungumza na msemaji wa Ikulu, Shanga aliweka simu na kujiuliza utawala wake umepatwa na balaa gani. Kwa nini kumekuwa na matukio ya ajali za kutisha?

Asubuhi kulipokucha, waziri mkuu wake alimpigia simu kabla hajatoka kwenda Ikulu.

“Umeamkaje, mheshimiwa Rais?”

“Nashukuru. Sijui nini kinaendelea huko?”

“Ni kuhusu ile ajali ya treni iliyotokea jana usiku.”

“Kuna yapi ya kunifahamisha?”

“Nimepatiwa idadi ya watu waliopoteza maisha na waliojeruhiwa. Kwa kweli ni idadi kubwa.”

“Abiria wangapi wamepoteza maisha?”

“Mpaka sasa abiria mia moja na hamsini wamepoteza maisha na abiria wengine zaidi ya mia mbili wamejeruhiwa, wakiwemo waliojeruhiwa vibaya.”

“Kwa kweli ni idadi kubwa sana!”

“Tatizo lililojitokeza ni la huduma. Mochwari zimejaa miili ya watu na majeruhi wamefurika katika hospitali, huku wengine wakikosa pa kuwekwa. Pia madaktari waliopo hawatoshi.”

“Sasa umechukua hatua gani kukabiliana na hali hiyo?”

“Ninataka ushauri wako.”

“Madaktari wa jeshi watumike na majeruhi waliokosa nafasi wapelekwe katika shule zilizopo karibu na hospitali watibiwe kwenye madarasa. Serikali igharamie magodoro na vifaa vingine vitakavyohitajika.”

“Sawa, mheshimiwa. Nitatekeleza agizo hilo.”

“Zoezi la kuwatambua marehemu lianze kufanyika asubuhi hii. Marehemu wawekwe kwenye kiwanja kimoja ili ndugu zao wafike kuwatambua na kuwachukua. Serikali itoe ubani kwa kila mfiwa kwa kiasi mtakachokadiria.”

“Nimekuelewa, mheshimiwa.”

Rais alipofika Ikulu alikuwa ameshikwa na fadhaa. Alilitangazia taifa maombolezo mengine ya siku tatu. Akaeleza kuwa msiba wa watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya treni iliyotokea usiku uliopita ni msiba wa taifa.

Tukio hilo la ajali lilisababisha wananchi wa Kamisa kuanza kuuguna utawala wa Rais Shanga. Wananchi hao walikuwa wakiujadili utawala wa Shanga katika kila kona ya jiji.

“Juzi ilitokea ajali mbaya ya ndege, hata siku tatu hazijamalizika, inatokea ajali nyingine inayopoteza mamia ya watu!” Mtu mmoja aliwaambia wenzake ndani ya mkahawa mmoja jijini Maloto.

“Hii si bure, huyu Shanga ameingia Ikulu na balaa. Matukio kama haya hayakuwepo nchini mwetu,” mtu mwingine akamjibu.

“Rais unatakiwa uingie Ikulu kwa kura za wananchi, lakini unapoingia kwa makafara, utawala wako utakuwa ni wa kumwaga damu!” akasema mtu mwingine aliyekuwa akitoka.

Watu wote walinyamaza na kumwangalia yule mtu aliyekuwa akitoka. Maneno yake yalikuwa yamewashitua.

Mnamo saa saba mchana, Rais Shanga alipigiwa simu na kaka yake Maloto, mganga wa kienyeji. Maloto alimweleza Shanga kuwa amepata msiba wa mwanawe aliyekufa katika ajali ya treni.

Rais Shanga akashituka na kumuuliza.

“Ni yupi mmojawapo?”

“Ni Joseph, mwanangu wa pili.”

“Sikujua kuwa mwanangu Joseph alikuwa miongoni mwa watu waliopoteza maisha katika ajali ile!”

“Mwili wa marehemu umeletwa sasa hivi. Tunakusubiri tupange mazishi yake.”

“Anza maandalizi. Mimi nitafika saa nane. Kwa vyovyote itakavyokuwa, itabidi azikwe kesho mchana.”

“Sawa, mheshimiwa, basi tunakusubiri.”

Kwa vile alikuwa Ikulu, mara tu alipomaliza kuzungumza na Maloto, Shanga alitoa taarifa ya kifo hicho kwa maafisa wa Ikulu, kisha akampigia simu mke wake aliyekuwa akiwafariji watu waliofiliwa na ndugu zao.

“Joseph, mtoto wa kaka Maloto, amefariki dunia!” Shanga alimjulisha mke wake.

“Wapi?”

“Alikuwa miongoni mwa abiria waliopata ajali.”

“Yesu wangu!”

“Mwili wake umeshachukuliwa. Ninahitajika niende tukapange mazishi. Sasa rudi nyumbani ili twende huko.”

“Ninakuja.”

Kama alivyoahidi, Shanga aliwasili nyumbani kwa Maloto saa nane akiwa amefuatana na mke wake pamoja na mlinzi wake. Pia kulikuwa na gari moja la maafisa wa Ikulu na magari mawili ya polisi.

Maloto alitoka kuwalaki na kuwakaribisha ndani.

Joyce, mke wa Shanga, alikwenda kwa wanawake wenzake wakati Shanga alipoweka baraza na ndugu zake kuzungumzia mazishi ya mtoto wao.

Walizungumza kwa karibu saa nzima na kupanga taratibu zote za mazishi. Wote walikubaliana kuwa mazishi yafanyike saa nane mchana siku iliyofuata.

Shanga akatoa mchango wake wa shilingi milioni mbili na afisa wa Ikulu akatoa shilingi milioni moja za ubani wa serikali. Kiasi hicho kilitolewa kwa kila mfiwa.

Rais Shanga aliondoka saa kumi kurudi Ikulu, lakini alimuacha mke wake.

Siku iliyofuata, Rais Shanga alihudhuria mazishi yaliyofanyika saa nane mchana.

Katika jiji la Maloto kulikuwa na mazishi mengi siku ile ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya treni. Karibu jiji zima la Maloto lilikuwa vilio vitupu.

Ilikuwa hali iliyomfadhaisha Shanga na kumfanya aanze kuyaona mashaka ya urais.

Miezi mitatu baadaye, wakati wananchi wa Kamisa wameshaanza kuyasahau matukio ya ajali, Shanga aliamshwa kwa simu mnamo saa nane usiku. Akaipokea simu hiyo kwa mashaka.

“Mkuu wa Majeshi hapa. Mheshimiwa, nimelazimika kukuamsha usingizini kukueleza kuwa nimepata taarifa ya kuwepo kwa uasi ndani ya jeshi.”

Shanga alishituka na kung’aka.

“Yesu wangu! Ni kina nani walioasi?”

“Askari wa kikosi cha kumi mpaka cha kumi na tano wameasi. Wamechukua silaha na hawapo tena kwenye makambi!”

“Wanataka nini?”

“Wanataka kukuondoa kwenye madaraka.”

“Kwa sababu gani?”

“Hatujajua ni kwa sababu gani, lakini nimeagiza askari watiifu kutoka kambi nyingine kukabiliana nao. Kumekuwepo na milio ya risasi katika jiji la Maloto na huenda mapambano yakawa makali zaidi.”

“Ulinzi wangu utakuwaje?”

“Nimeshatuma askari na vifaru kuja kukuwekea ulinzi, mheshimiwa.”