Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya kutisha - Sehemu ya 30

MAUAJI 30 Pict

UTANGULIZI

Miaka kadhaa ikapita.

Mwisho akasahau kabisa kama kuna masharti alipewa na ameacha kuyatekeleza.

Ndipo siku moja mtoto wake wa kwanza aliyemuita Martin alipovamiwa na watu watatu wa ajabu, akachinjwa na kunyang’anywa mkoba wa pesa….

Sasa Almasi akiwa kwa mganga waliyemwendea yeye na Maria alitingisha kichwa chake taratibu baada ya kuwaza.

“Nimekumbuka kitu…” akamwambia mganga kwa sauti iliyonywea.

SASA ENDELEA


“Enhe… nieleze umekumbuka kitu gani?” mganga akamuuliza.

Almasi akamtazama Maria na kumuomba atoke nje ya kile chumba.

Maria akatoka. Almasi akamwambia mganga.

“Mimi nilikuwa mchimbaji wa madini. Nikashauriwa na wenzangu kwamba ili nipate madini ya kutosha niende kwa mganga. Nikaenda kwa mganga mmoja wa Korogwe ambaye alinifanyia uganga wake, lakini ulikuwa na masharti…”

Almasi aliendelea kumweleza mganga huyo jinsi alivyotakiwa na mganga huyo kumtoa mtu kafara ili apate utajiri wa madini, na yeye akafanya hivyo.

“Ni masharti gani ambayo alikupa?”

“Aliniambia kila mwaka nitoe robo ya mapato yangu, niyamwage baharini.”

“Ulifanya hivyo?”

“Nilifanya mara moja, halafu sikufanya tena.”

“Ni miaka mingapi sasa tangu uache kutimiza hilo sharti?”

“Ni miaka mingi.”

Mganga alichungulia kwenye mdomo wa tunguri aliyokuwa ameiweka mbele yake, kisha akamwambia Almasi.

“Unajua maana ya mganga kukwambia uwaweke watoto wako na mke wako kama dhamana?”

Almasi akatikisa kichwa.

“Sijui.”

“Maana yake ni kwamba kama hutatimiza masharti uliyopewa, watawajibishwa wao. Ndiyo maana wale waliokuwa wanakuja kuwaua walikuwa wanawaambia, ‘Baba yenu aliwaweka kama dhamana na mmeshindwa kutimiza masharti ya dhamana.’”

Almasi akatikisa kichwa kwa kusikitika kabla ya kuuliza.

“Wale watu ni kina nani kwani?”

“Wale wawili wanaovaa mavazi meupe ni majini waliotakiwa kupewa hiyo robo ya mapato yako kila mwaka, na yule aliyevaa nguo nyeusi ni mdogo wako ambaye ulimchinja. Na ndiyo maana unaambiwa kuwa shingo yake imechinjwa na kichwa chake kinaning’inia.”

Almasi akashituka.

“Niliyemchinja alikuwa mdogo wangu?” akauliza.

“Ndiyo, alikuwa mdogo wako. Alikwenda Arusha kukutafuta wewe.”

“Anaitwa nani?”

“Mimi siwezi kukutajia jina lake, lakini kumbuka ni ndugu yako gani ambaye umepoteana naye kwa miaka mingi.”

“Sisi tulizaliwa wawili tu, mimi na mdogo wangu anayeitwa Frenk.”

“Huyo Frenk yuko wapi?”

“Sijui yuko wapi.”

“Mdogo wako humjui yuko wapi?”

“Tulipoteana miaka mingi.”

“Hamjakutana kwa miaka mingapi sasa?”

“Miaka mingi.”

“Sasa nakwambia ndiye huyo ambaye amechinjwa.”

“Mama yangu, sikujua kama yule alikuwa mdogo wangu. Wenzangu ndiyo waliomkamata na kumchinja. Kumbe alikuwa Frenk!”

“Sasa dhambi yake umeiona. Na wewe watoto wako wote wamekwisha.”

Almasi aliendelea kutikisa kichwa.

“Sikujua… sikujua… sasa nifanye nini jamani?”

“Umechelewa. Hivi sasa huna la kufanya.”

Almasi akamtumbulia macho mganga huyo.

“Unasemaje?”

“Nimekwambia kwamba umechelewa.”

“Nimechelewa nini?”

“Kuchukua uamuzi.”

“Uamuzi gani sasa?”

“Uamuzi wa kunusuru.”

“Nitakwenda kutupa baharini zile pesa.”

Mganga akatikisa kichwa.

“Umechelewa. Hao majini wana hasira na huwezi kuwatuliza tena. Wanachotaka ni roho tu.”

“Roho ya nani sasa?”

“Roho yako wewe!”

Almasi aliposikia maneno hayo kwamba hao majini waliompatia huo utajiri wana hasira na wanachotaka sasa ni roho yake tu, alimtolea macho mganga huyo. Akamtazama kwa sekunde kadhaa akiwa ametaharuki, kisha ghafla aliinuka na kutoka mle chumbani bila kuaga.

Alimwambia shemeji yake, mdogo wa marehemu mke wake.

“Twende zetu.”

Walitoka na kujipakia kwenye gari. Aliliwasha gari hilo huku akijisemea.

“Mganga amenitisha sana.”

“Amekwambiaje?”

“Ameniambia wanachotaka hao majini ni roho yangu tu!”

“Majini gani hao?”

Almasi aliliondoa gari kwa kasi.

“Kumbe wewe hukuwepo wakati tunazungumza.”

“Si uliniambia nitoke ili nisisikie mnachozungumza?”

“Nilikwambia vile kwa sababu. Lakini hayo tuyaache. Zamani nilikuwa ninachimba madini. Na unajua wanaofanya kazi ile mara nyingi hupendelea kwenda kwa waganga, na mimi nilikwenda. Nikafanyiwa kafara na kuambiwa kwamba nitakapopata mali, kila mwaka nikatose baharini robo ya pesa za mapato yangu. Nilifanya hivyo kwa mwaka mmoja tu, nikaacha. Sasa huyu mganga ameniambia hao majini walionipa huu utajiri wamekasirika na ndiyo wanaoua.”

“Lakini umeamini maneno yake?”

“Naona yana ukweli. Alivyonieleza ndivyo vilivyokuwa. Hao majini wamemaliza watoto wangu pamoja na mke wangu, sasa wanataka roho yangu.”

“Kumbe shemeji, huu utajiri wako ni wa majini?”

“Zamani ndiyo, niliwahi kwenda kwa mganga wakati nashughulika kuchimba madini.”

“Kwa hiyo chanzo cha pesa zako ni majini?”

“Sasa hivi si unaona nafanya biashara. Nilikwenda siku moja tu kwa mganga.”

“Si unajua pesa za namna hii zinasababisha umwagaji wa damu!”

Almasi akanyamaza kimya.

Mwanamke huyo akaendelea.

“Ndiyo sababu watoto wamekuwa wanauawa ovyo na watu wasioeleweka na mwisho dada yangu naye ameuawa.”

“Tatizo ni kwamba natakiwa nikamwage zile pesa baharini. Na kesho tu nitafanya hivyo.”

“Lakini itasaidia nini, shemeji, wakati watoto wako pamoja na dada yangu wameshauawa?”

“Kwa hiyo unataka niache na mimi niuawe?”

“Si uliyataka mwenyewe, shemeji?”

“Usiseme hivyo. Nani ambaye hajafaidika na utajiri wangu?”

“Utajiri wa kutoa watu kafara una maana gani, shemeji? Kumbe wewe ndiyo umemuua dada yangu!”

Almasi akazidi kutaharuki.

“Dada yako nimemuua mimi?”

“Kumbe si umesema uliliacha hilo sharti ndipo wanao pamoja na mke wako walipoanza kuuawa na watu wasiojulikana?”

Almasi akiwa ametaharuki, alilisimamisha gari barabarani.

“Sasa nakuuliza, ndiyo nimemuua mimi dada yako?” akamuuliza shemeji yake kwa ukali.

“Ni wewe! Utasema ni nani? Dada yangu pamoja na wanao wameuawa kutokana na ushirikina wako. Tena afadhali usingeniambia. Kumbe baba wewe ni mshirikina sana!”

“Shuka kwenye gari langu. Huna adabu!” Almasi akafoka.

“Nitashuka, lakini tutakususia mke wako, utamzika mwenyewe. Na nitawambia ndugu wote kwamba wewe ndiyo mhusika wa haya mauaji!”

Mwanamke huyo alifungua mlango wa gari, akashuka na kutembea kwa miguu. Almasi alimtazama kwenye kioo kabla ya kuliondoa gari hilo kwa hasira.

Alifikiria aende kituo cha polisi kutoa ripoti ya kuuawa kwa mkewe, lakini akaona arudi nyumbani kwake. Alipofika, hakuingia ndani, alitoa simu yake na kumpigia Inspekta Amour.

Amour alipokea simu, alimwambia.

“Mke wangu naye ameuawa sasa hivi.”

“Ameuawa na nani?”

“Na wale watu walioua watoto wangu. Leo ndiyo nimewashuhudia kwa macho yangu.”

“Uliwaona?”

“Ndiyo, niliwaona.”

“Walimuua wapi mke wako?”

“Walimuulia hapa nyumbani. Waliingia chumbani mwetu, wakamuua.”

“Umeshapiga ripoti kituo cha polisi?”

“Wewe ndiye mtu wa kwanza kukuarifu.”

“Sasa uko wapi?”

“Niko nyumbani kwangu. Hawa watu nimewafungia mlango, kama bado wapo mtakuja kuwaona.”

“Yaani hao wauaji umewafungia mlango humo chumbani?”

“Ndiyo.”

“Sawa. Tunakuja sasa hivi nyumbani kwako.”

Almasi alikata simu na kuirudisha mfukoni. Alikuwa ametoka ndani ya gari lake na kujiegemeza kwenye boneti la mbele la gari hilo.

Hasira ya kuambiwa kuwa amemuua mke wake ilikuwa bado ikimkereketa moyoni. Alijuta kwa nini alimweleza shemeji yake maelezo aliyoambiwa na mganga wakati akijua baadhi ya wanawake hawafikiri mbali.

“Mimi nimuue mke wangu, kwani sina akili?” akajiambia peke yake.

“Kweli yule msichana ni mjinga. Anaweza kuniponza,” akaendelea kujiambia.

Kwanza alimuona alikuwa hodari na mwenye hekima kumwelekeza kwenda kwa mganga ambako tatizo lake lilikwenda kugundulika. Lakini alipofikia hatua ya kumwambia amemuua mke wake, alimuona mpumbavu.

Baada ya nusu saa tu, magari mawili ya polisi yakawasili nyumbani kwa Almasi. Vile polisi walivyoambiwa kwamba wauaji hao walikuwa wamefungiwa kwenye chumba, walikuja polisi tisa. Watano wakiwa na bunduki. Inspekta Amour, ambaye huvaa kiraia, alikuwa wa kumi.

Almasi aliwakaribisha.

“Hao watu wamo ndani?” Amour akamuuliza akiwa ameshika bastola mkononi.

“Niliwafungia chumbani mwangu na sijafungua mlango hadi sasa.”