Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KISIWA CHAMAUTI - 38

KISIWA 38 Pict

ILIPOISHIA

Huko Unguja tukafanikiwa kukutana na Rais wa Zanzibar.

“Jana ndege ya Comoro ilikuja kumchukua Yasmin kumrudisha kwao. Alitaka aondoke na mimi lakini sikuwa na paspoti na pia sikuwa nimewaona ndugu zangu” nkawambia na kuongeza.

“Yasmin nimempenda na yeye amenipenda. Ameniahidi kuwa tutaoana. Leo asubuhi mama yake mzazi amenipigia simu kunijulia hali na kuniuliza nitakwenda lini Comoro”

SASA ENDELEA...


Habari za Yasmin ziliwatia hamu kubwa ndugu na marafiki zangu, hasa kwa vile Yasmin alikuwa ni binti wa Rais wa Comoro.

“Sasa utakwenda Comoro?” rafiki yangu mmoja akaniuliza huku akitabasamu.

“Ni lazima niende, kwani moyo wangu uko kwa Yasmin. Alinifariji sana na kunipa moyo tulipokuwa katika kile kisiwa.”

“Unadhani kweli utaweza kuoana na binti wa rais wa nchi?” kaka yangu mkubwa akaniuliza.

“Kwanini nisiweze, kaka, kama binti mwenyewe amenipenda?” nikamuuliza kaka yangu aliyekuwa anaitwa Shaali.

“Unadhani wazazi wake watakubali?”

“Kuhusu suala la wazazi sina uhakika sana, lakini nitakwenda kuwasikiliza.”

“Tunakuombea heri, ufanikiwe kumuoa binti wa rais na sisi tupate hadhi kidogo.”

“Haya, karibu sana nyumbani mwanangu. Tunashukuru kuwa umerudi salama na umekuja na habari njema, japokuwa wenzako wote wamepoteza maisha,” baba yangu naye akaniambia.

Habari za kuwasili kwangu zilikuwa zimesikika kwa majirani ambao walianza kufika pale nyumbani mmoja mmoja na kunipa pole.

Haukupita muda polisi wakafika. Nikaambiwa niende kituo cha polisi kuandikisha maelezo yangu, kwa vile tulipotea na chombo baharini na wenzangu walifikwa na umauti.

Polisi hao wakanichukua kituo cha polisi, ambako walinihoji maswali wakitaka kujua jinsi chombo chetu kilivyozima moto siku ile hadi tukatokea katika kile kisiwa.

Nikawaeleza kila kitu walichoniuliza hadi wenzangu walivyouawa mmoja mmoja.

Baada ya kuandikisha maelezo yangu, niliruhusiwa kuondoka.

Kusema kweli, licha ya furaha iliyokuwa nyumbani kwetu, kwa baadhi ya majirani zetu ilikuwa ni huzuni kutokana na vifo vilivyowakuta wenzangu.

Wengi wa marehemu hao waliacha wake na watoto, na mimi ndiye niliyethibitisha juu ya vifo vyao. Iliwapa huzuni watu wengi, kwa vile wenzangu waliokufa waliuawa kikatili.

Baada ya kupita wiki moja ndipo nilipoanza maandalizi ya kwenda Comoro. Nilikwenda Unguja kuulizia ndege itaondoka lini. Nilipojua siku ya kuondoka ndege, nilirudi Pemba kuendelea na maandalizi yangu ya safari.

Siku mbili kabla ya safari, nilipiga simu kwa namba aliyonipa Yasmin. Aliyepokea simu alikuwa kaka wa Yasmin.

Nikajitambulisha kwake kuwa ni Zahran wa Zanzibar, akanikumbuka.

“Oh, Zahran, unaendeleaje?”

“Naendelea vizuri, sijui nyinyi huko?”

“Sisi hatujambo. Ngoja nikuunganishe na Yasmin kwenye simu yangu.”

Nilisubiri kidogo, kisha nikasikia sauti ya Yasmin ikisema, “Hello!”

Nikataka kujibu, lakini nikaisikia sauti ya kaka wa Yasmin ikisema:

“Zungumza na Zahran kutoka Zanzibar.”

“Hello, Zahran!” Sauti ya kusisimua ya Yasmin ikasikika tena.

“Ndiyo, Yasmin, hujambo?”

“Sijambo. Nakuhofia wewe.”

“Mimi sijambo. Nataka kukufahamisha kuwa kesho kutwa ninakuja Comoro.”

“Njoo tu, usiwe na wasiwasi. Utaondoka saa ngapi?”

“Sijajua muda, lakini nitakufahamisha nitakapokata tikiti kesho.”

“Utanipigia simu kesho?”

“Ndiyo, nitakupigia kukufahamisha muda wa kuondoka ndege.”

“Sawa. Nitasubiri simu yako.”

Siku ile ile niliondoka kwenda Unguja. Nilifuatana na kaka yangu Shaali. Unguja tulilala kwenye nyumba ya wageni. Siku ya pili yake nilikwenda kukata tikiti ya ndege ya kwenda Comoro.

Ndege ilikuwa inaondoka kesho yake saa mbili asubuhi. Baada ya kupata tikiti na kujua muda wa safari, nilimpigia tena simu kaka wa Yasmin ambaye aliniunganisha na Yasmin.

“Asalaam alaykum,” Yasmin akanisalimia.

“Wa alayka salaam. Habari ya tangu jana?”

“Nzuri, sijui nyinyi?”

“Sisi hatujambo, tunashukuru. Nimeshakata tikiti ya ndege ya kesho.”

“Ndege itaondoka saa ngapi?”

“Itaondoka saa mbili asubuhi.”

“Basi tutakusubiri kiwanja cha ndege.”

“Nitashukuru sana.”

Nilipomaliza kuzungumza na Yasmin, kaka yangu aliniambia:

“Inaonekana utapata mapokezi makubwa. Natamani tungekuwa sote.”

Aliponiambia hivyo nikacheka.

Siku iliyofuata saa kumi na mbili asubuhi, mimi na kaka yangu tukawa kiwanja cha ndege cha Unguja. Kaka yangu alikuwa amefuatana na mimi kwa ajili ya kunisindikiza.

Baada ya kukamilisha taratibu zote za safari, nikawa kwenye chumba cha abiria wanaosubiri kujipakia kwenye ndege. Nilikuwa nimeshaagana na kaka yangu na alikuwa akisubiri kuona tukijipakia kwenye ndege.

Muda ulipowadia, tangazo lilitolewa kuwa abiria wanaokwenda Comoro wajipakie kwenye ndege. Tangazo likaeleza kuwa ndege itaondoka saa mbili kamili.

Abiria wote tuliokuwa tunakwenda Comoro tukanyanyuka na kwenda kujipakia kwenye ndege. Tulisubiri kwa dakika kadhaa kabla ya tangazo la kuruka kwa ndege kutolewa.

Tulitajiwa majina ya marubani wetu na masafa ambayo ndege itaruka.

Tangazo hilo lilitaka tujifunge mikanda ili tusipate usumbufu wakati ndege inaruka. Ndege ilianza kuvuta kasi. Wakati namaliza tu kujifunga mkanda, ndege ilianza kuruka.

Ilikuwa ni mara yangu ya tatu kupanda ndege. Mara ya kwanza ilikuwa ni wakati ninakwenda Comoro kwa ajili ya harusi ya Yasmin. Na mara ya pili niliporudi Zanzibar kutoka Comoro.

Ulikuwa mwendo wa saa nne. Ndege ilitua katika kiwanja cha Moroni, moja ya visiwa viwili vinavyounganisha Jamhuri ya Comoro.

Mlango wa ndege ulipofunguliwa, abiria tulianza kushuka kwenye ndege. Tulishuka ngazi ya ndege tukaingia kwenye mlango wa jengo la kiwanja cha ndege.

Mara tu nilipokamilisha taratibu za uhamiaji na kukaguliwa, tuliingia katika ukumbi ambako nilikutana na Yasmin.

Yasmin alikuwa amesimama na kikundi cha watu wakinisubiri. Watu hao walinilaki kwa bashasha, nikajiona kama mfalme.

Yasmin alinitambulisha kwa mama yake na wadogo zake wawili wa kike. Pia alikuwepo kaka yake na maafisa usalama kadhaa.

Baada ya kuulizana hali, Yasmin alishika begi langu tukatoka nje ya kiwanja.
Kulikuwa na magari matatu ya familia ya rais na gari moja la serikali.

Mimi na Yasmin tulipanda gari la peke yetu. Nilijisikia furaha sana kupanda gari moja na Yasmin. Mama yake Yasmin alipanda gari la peke yake.

Kaka yake Yasmin na wadogo zao wawili walijipakia katika gari moja. Katika gari la serikali walipanda maafisa usalama peke yao.

Msafara wa magari wa kuelekea mjini ukaanza. Kilichokuwa kinaonekana hapo ni kuwa nilikuwa mgeni wa heshima kubwa.

Baada ya mwendo wa takriban nusu saa, msafara huo ulisimama mbele ya hoteli moja mashuhuri nchini Comoro.

Ilikuwa hoteli iliyokuwa ikimilikiwa na kaka wa Yasmin.

Tukashuka kwenye magari na kuingia katika hoteli hiyo iliyokuwa karibu na ufukwe wa bahari.

Nilikuwa nimekodishiwa sehemu ya familia ambayo ilikuwa na vyumba vitatu, sebule na chumba cha kulia chakula. Vyumba vya aina hiyo vilikuwa vinakodiwa na wageni mashuhuri kutoka nchi za nje. Mswahili kama mimi ilikuwa ndoto kukaa mahali hapo, kwa sababu gharama yake ni kubwa.

Nilihisi kuwa familia ya kina Yasmin ilikuwa imenipa heshima kubwa sana. Mara tu tulipofika hapo hotelini, walifika waheshimiwa wawili wa serikali ya Comoro. Mmoja alikuwa waziri wa mambo ya ndani na mwingine alikuwa naibu waziri wa mambo ya nje.

Walizungumza na mimi kwa karibu nusu saa. Walitaka kupata maelezo yangu kuhusu kukutana kwangu na Yasmin katika kile kisiwa tulichokuwa. Baada ya mazungumzo yetu waliondoka.

Wakaja makachero wa serikali ya Comoro ambao pia walitaka kupata maelezo yangu. Wao walinihoji maswali mengi sana ambayo niliweza kuyajibu.

Makachero hao walipoondoka, walifika waandishi wa habari wa Comoro. Walikuwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuanzia magazeti, redio na televisheni.

Walinihoji maswali mengi hadi walipoondolewa na maafisa usalama. Wakaondoka.

Baada ya hapo nikapata nafasi ya kuzungumza na ndugu na jamaa wa Yasmin ambao walifika pale hotelini kuniona na kunitakia mema.

Mchana nilikaribishwa chakula nyumbani kwa mke wa rais. Kilikuwa chakula cha heshima kubwa ambacho kilihudhuriwa na watu wa familia ya rais, ingawa rais mwenyewe hakuwepo.

Saa tisa mchana nilipelekwa ikulu ambako nilikutana na rais wa Comoro. Katika dakika kadhaa za mazungumzo yetu niligundua kuwa rais huyo alikuwa mtu mcheshi na mkarimu sana.

Alinishukuru na kunipongeza sana na kisha alinikaribisha rasmi nchini Comoro.

Kwa muda wa wiki nzima nilikuwa katika pilikapilika za kupelekwa huku na huku kama mgeni wa shani. Wakati wote Yasmin alikuwa sambamba na mimi.

Pale hotelini nilipofikia nilikuwa nikihudumiwa na wafanyakazi wa hoteli na kupewa heshima wanayopewa watu wa familia ya rais.

Baada ya kupita wiki moja ndipo Yasmin alipoanzisha mazungumzo ya ahadi yetu ya kuoana. Kila tulipokuwa peke yetu alikuwa akinikumbusha tulivyokuwa katika kile kisiwa cha Harishi.

Aliniambia kwamba wapelelezi wa Kifaransa walikwenda kukichunguza kisiwa hicho ili kuthibitisha kama kweli tulikuwa katika kisiwa hicho. Kwa mujibu wa uchunguzi huo, Yasmin aliniambia, kisiwa hicho kilikumbwa na gharika miaka mia moja iliyopita na kusababisha watu wote kufa na kubaki majumba pekee.

Yasmin akanieleza kuwa wapelelezi hao wamedai kuwa kila baada ya miaka mia moja gharika hutokea katika kisiwa hicho.