Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KISIWA CHAMAUTI - 32

KISIWA 32 Pict

ILIPOISHIA

Nilimuangalia tu Yasmin, sikumjibu kitu tena. Nikaendelea kunywa uji huku nikiwaza kama ni kweli alikuwa amejitolea nafsi yake kwa ajili yangu.

Maneno yake yalionesha alichokuwa akisema kilikuwa na udhati.

Hata hivyo niliwaza kuwa msimamo wa Yasmin haukuwa na msaada wowote kwangu zaidi ya kuonesha upendo. Ulikuwa msimamo wa kukata tamaa na haukuwa na maana..

SASA ENDELEA...


ATANGULIE yeye kufa halafu nifuatie mimi? Maana yake ni kuwa sote tutafikwa na mauti. Jambo hilo kwangu lilikuwa tishio ingawa yeye aliona lilikuwa la kijasiri.

Jambo la maana lilikuwa kupata wazo la kutunusuru sote na sio tufe sote.

Tulibaki kimya tukinywa uji. Uji huo niliunywa kwa kujilazimisha ili kumridhisha Yasmin. Kama ningekuwa peke yangu ningebaki na njaa hadi mauti yatakaponikuta.

Nilipomaliza kikombe changu cha uji Yasmin aliniuliza.

“Nikutilie tena?”

“Umetosha’ nikamjibu.

Yeye pia alikuwa amemaliza uji wake akaniambia.

“Basi nenda ukaoge, umeshatia nguvu kidogo”

Pamoja na kukabiliwa na tishio hilo la kifo kusema kweli nilihitajika sana kuusafisha mwili wangu. Nilikuwa nimechafuka sana na nilikuwa sijaoga kwa siku tatu.

Niliona aibu kumwambia Yasmin kuwa sitaoga. Nikainuka.

Yasmin akanipeleka bafuni kisha akaondoka. Nilioga haraka haraka. Nilipomaliza niliondoka bafuni na kumbishia Yasmin mlango.

Yasmin alinifungulia mlango na kuniambia.

“Karibu”

Niliingia mle chumbani alimokuwa. Hamkuwa na kiti. Akaniambia.

Kaa kitandani”

Nikakaa.

“Unajisikia vizuri kidogo?” akaniuliza.

Nilijaribu kutabasamu bila kufanikiwa. Niliishia kubenua midomo tu, uso haukukunjuka.

Yasmin akaja kukaa kando yangu.

“Unajua maisha?” akaniuliza. Sikujua alikuwa na maana gani.

“Maisha ni nini?” nikamuuliza.

“Maisha ya mwanaadamu ni mtihani. Lolote linalokufika liwe zuri au baya ni mtihani kwako. Kama wewe ni muumini unatakiwa ulijue hilo”

“Ndio ninalijua”

“Mungu hashindwi kutuokoa sisi waja zake tunaomtegemea yeye ila anatupa mitihani kuona ni kwa kiasi gani tunaweza kuweka matumaini kwake na kwa jinsi gani tunaweza kumuomba kwa unyenyekevu katika siku hii ambayo mimi na wewe tunahitaji sana msaada wake”

Ndani ya moyo wangu nilikiri kuwa Yasmin alikuwa amenieleza maneno ya maana kuliko aliyowahi kunieleza wakati wowote. Nilifarijika kuona juhudi zake za kunitia moyo zilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuamsha imani yangu.

Nikajiambia laiti kama ningekuwa na mke kama Yasmin nisingeshindwa kimaisha hata itokee shida ya kiasi gani.

Hatimaye jua lilikuchwa. Giza lilianza kuingia. Yasmin aliwasha taa za nyumba nzima. Alikuwa ameniacha mle chumbani mwake, akanifuata na kuniuliza. “Utakula chakula?”

Nikatikisa kichwa.

“Sitakula”

“Hutakula hata kidogo”

Nikaendelea kutikisa kichwa.

“Sitakula”

Yasmin akakaa karibu yangu.

“Usiku ndio huu” akaniambia.

“Kwani Harishi atakuja muda huu?”

“Anaweza kuja wakati wowote kutoka sasa hadi alfajiri”

“Anakujaje?” nikamuuliza Yasmin huku nikiitazama ile chupa iliyokuwa juu ya kabati.

“Anakuja kama moshi. Unajaa ndani ya ile chupa kisha unatoka. Unapotoka unabadilika na kuwa jini”

“Na ni kwanini anakuja hivyo?”

Yasmin akabetua mabega yake

“Sijui lakini ondoa hofu. Mwisho wa mateso yetu utakuwa leo”

Sikusema kitu tena nikanyamaza kimya. Tulikaa kimya kwa muda mrefu. Ile shauku ya kuzungumza ilikuwa imetuishia. Tukaamua kukaa tu kusubiri muda wetu.

Tulikuwa tumekaa chini tumeelekezana migongo. Kila mmoja alielekea upande wake. Yasmin alipochoka au kuhisi kusinzia aliuegemeza mgongo wake kwenye mgongo wangu.

Kitu gani kilimfanya Yasmin asipande kitandani na kulala?

Alikuwa amejitolea kufa na mimi. Alikuwa ameamua akae na mimi pale chini hadi Harishi atakapokuja.

Ilikuwa kama saa saba usiku nywele zangu zilipoanza kunisisimka. Nikayapeleka macho yangu kwenye ile chupa ya Harishi iliyokuwa juu ya kabati. Moyo wangu ulishituka nilipoiona chupa inaingia moshi kwa ndani. Nikamgutusha Yasmin aliyekuwa anasinzia.

“Yasmin!”

“Abee!” Yasmin akaniitikia.

“Tazama ile chupa!”

Yasmin akageuza uso wake na kuitazama chupa hiyo.

“Usimuogope kiumbe aliyeghulukiwa kama wewe. Muogope aliyeghuluku” Ndilo neno aliloniambia Yasmin.

Ule moshi uliendelea kujaa ndani ya ile chupa. Kifiniko cha chupa hiyo kilikuwa pembeni. Moyo haukunipa.

Mara moja nikanyanyuka na kwenda kando ya lile kabati. Nilisubiri ule moshi ujae kabisa kisha nikakichukua kile kifiniko na kukifunga kwenye mdomo wa ile chupa.

Baada ya sekunde chache nilisikia sauti ya Harishi kutoka kwenye ile chupa.

“Nani amefunga kizibo?”

Sote tukanyamaza kimya.

Ile sauti ikasikika tena.

“We Yasmin si nilikwambia usifunge hiki kizibo?”

Tukaendelea kunyamaza lakini moyo wangu ulikuwa ukienda mbio.

“Fungua sasa!” ile sauti sasa ilifoka.

“Usifungue!” Yasmin akaniambia huku akinifuata.

“Ahaa! kumbe uko na hawara yako! Sasa mtanitambua”

“Sifungui!” Yasmin akasema kwa jazba.

“Nimekwambia fungua, nataka nitoke!” Sauti ikafoka.

“Toka mwenyewe!” Yasmin akajibu.

“Yasmin umechoka kuishi? Nakwambia nitakuua wewe na hawara yako!” Sauti ya Harishi iliendelea kuunguruma kwa hasira.

“Ndio tunavyotaka utuue. Tuue sasa hivi!” Yasmin aliendelea kujibu.

“Wewe kijana nani amekuruhusu ufunge hiki kizibo, hujui kuwa hii ni nyumba yangu?” Sauti ya Harishi ikaniuliza.

“Nimemruhusu mimi akifunge. Nimeshachoka na wewe. Kama unaweza kutoka toka mwenyewe utuue. Sisi tunasubiri kufa tu”

“Yasmin umeamua kunigeuka leo?” Sauti ya Harishi sasa ilikuwa imerudi chini. “Nifungulie mke wangu. Nimekuletea zawadi nzuri”

“Sitaki zawadi yako. Njoo utuue!”

“Nani amekwambia kama nataka kuwaua?”

“Si ndio kazi yako kuua watu. Watu wote wa kisiwa hiki si umewamaliza wewe!”

“He he he!” Harishi alitoa kicheko kilichoonesha wazi kuwa ni cha uongo. Kisha akauliza kwa ukali.

“Sasa utakifungua kizibo au hufungui?”

“Sifungui!” Yasmin akamjibu.

“Wewe kijana fungua kizibo hicho?’ Sauti ya Harishi ikanigeukia mimi.

“Usifungue. Mwache atoke mwenyewe. Sisi tumeshajitolea, liwalo na liwe!” Yasmin akaniambia.

Wakati wote nilikuwa najiuliza kama Harishi alikuwa hawezi kutoka mwenyewe kwenye ile chupa mpaka atuombe sisi tufungue kizibo.

Nikataka kupata uhakika kama kweli Harishi alikuwa amenasa na asingeweza kutoka bila msaada wetu.

Nikamwambia Yasmin “Tusifungue hii chupa tuone nini kitatokea”

“Wewe achana naye, kama akitoka mwenyewe na atoke, potelea mbali!”

Nilikuwa nimesimama kando ya lile kabati. Yasmin alisimama karibu na kitanda. Macho yetu sote yalikuwa kwenye ile chupa.

Ingawa nilikuwa nimejikaza kiume, hofu ilikuwa ikitambaa kwenye mishipa yangu. Yasmin hakuonesha kuwa na hofu hata chembe. Nilishangaa kuona msichana ambaye siku zote nilimuona dhaifu, siku ile alikuwa amejaa ujasiri usio kifani. Hapo niliamini kweli kuwa Yasmin alikuwa amejitolea kufa kupona.

Ile sauti ya Harishi iliyokuwa ikitoka kwenye chupa ilipotea lakini ule moshi uliendelea kuonekana. Kwanza ulionekana moshi wa rangi nyeusi kisha ukabadilika na kuwa wa rangi nyeupe. Baada ya muda kidogo ulibadilika tena na kuwa wa rangi nyeusi.

Mawazo yangu yote yalikuwa kwenye kifo kibaya kilichokuwa kinatungoja. Nilijua kuwa Harishi angekizibua mwenyewe kile kizibo na kutoka. Hapo hasira zake zisingekuwa na kifani. Nilipata wazo la kumwambia Yasmin tukimbie lakini nikajiuliza tutakimbilia wapi usiku ule? Na ni wapi ambapo Harishi hataweza kufika?

Muda uliendelea kupita. Tuliona Harishi hatoki kwenye ile chupa kama ilivyo kawaida yake. Aliendelea kututaka tukifungue kizibo kwa sauti ya upole akiahidi kwamba hatamuua yeyote.

Nikahisi inawezekana kwamba kitendo kile cha kuwahi kukifunga kile kizibo cha cha chupa wakati Harishi yumo ndani ya chupa ile akiwa katika umbile la moshi, kilikuwa kimemzuia kutoka na hakuwa na uwezo tena wa kutoka mwenyewe.

Hapo hapo nikazikumbuka simulizi za wazee wa zamani zilizosema kwamba majini walikuwa wakifungiwa ndani ya chupa na kutoswa baharini pindi wanapofanya makosa.

Kumbe ni kitu kinachowezekana kweli, nikajiambia.

“Sisi tunaiondoa hii chupa!” nikasema kwa sauti ili kusikia Harishi atajibu nini.

“Usiiondoe. Nataka mnifungulie niende zangu” Sauti ya Harishi ikasikika kutoka kwenye ile chupa.

“Hakuna atakayekufungulia muuaji wewe”Yasmin akamwambia.

“Nifungulie nitakurudisha kwenu”

“Mbona siku zote hukunirudisha?”

“Nakwambia kweli kabisa. Ukinifungulia nitakurudisha kwenu Comoro”

“Kwenda zako, mimi si mjinga wa kukufungulia wewe.. Bora ubaki humo humo. Siku zako zimeshafika”

Yasmin akanigeukia mimi na kuniambia.

“Twende tukaizike hii chupa”

“Hapana.. hapana. Msiizike!” Sauti ya Harishi ikalalamika.

“Mimi naona tukaizike baharini” nikamwambia Yasmin.

“Hapana…hapana. Msiitose baharini!” Ilikuwa sauti ya Harishi lakini hatukuipatiliza.

“Niliwahi kusikia kule kwetu kwamba majini wanafungiwa kwenye chupa na kutoswa baharini,” nikamwambia Yasmin.