Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KISIWA CHA MAUTI - 28

KISIWA 28 - Pict

ILIPOISHIA

Mimi na Haji na Shazume tulitazamana tukiwa tumeacha midomo wazi.

“Aliyataka mwenyewe!” Yasmin akasema.

“Ni kweli aliyataka mwenyewe, kifo kilikuwa kinamuita,” nikamuunga mkono.

“Angekuja kulala na wenzake, pengine angenusurika,” Yasmin aliendelea kutuambia.

“Mbona hukuja mapema kutuambia?” nikamuuliza.

“Harishi ameondoka sasa hivi. Jana usiku alipokuja alikuwa amelewa na alipomuua Masudi hakuondoka tena hadi hii asubuhi.”

“Kumbe majini pia wanalewa?”

“Wanalewa kama watu. Harishi analewa sana.”

“Hiyo pombe anaipata wapi?”

“Sijui mwenyewe.”


“Na anapokuta mtu mle ndani, anakuuliza ni nani?”

“Anaua kwanza, halafu ndiyo anauliza. Mimi humwambia kwamba ni wavuvi wameingia kwa bahati mbaya. Lakini kama angenikuta nimelala naye, angejua ni mwanaume wangu.”

“Angekuua?”

“Sijui ingekuwaje?”

Pakapita kimya cha sekunde kadhaa. Sote tulikuwa tukimkumbuka kaka yetu Masudi.

“Mtanisamehe, sikuwaletea chai. Nilikuwa nimetaharuki sana,” Yasmin akatuambia baadaye.

“Misiba kama hii, kila siku anakufa mtu. Hamu ya kula pia inapotea,” nikamwambia..

SASA ENDELEA...


“Nyinyi mtabaki huku huku mjaribu bahati zenu. Mnaweza kusalimika”

“Tutakufa kama wenzetu. Sidhani kama tutapona kwa maana tulikuwa watu saba, sasa tumebaki watatu” nikamwambia Yasmin.

“Msikate tamaa ndugu zangu. Kama ni kufa tutakufa sote. Hamuwezi kufa mkaniacha mimi”

Nilimuona Haji akijifuta machozi.

“Usilie ndugu yangu. Ushinde moyo. Safari yenu bado ni ndefu” akaambiwa na Yasmin.

Shazume akageuza uso na kunitazama.

“Nina tamaa ndogo sana kama tutapona” akaniambia.

Sikumjibu kitu. Yasmin akanyanyuka.

Nitawatayarishia japokuwa uji mchangamke” akatuambia.

“Sawa” nikamjibu.

“Naenda kuwapikia halafu nitawaletea”

“Kama tutakusumbua ninaweza kuja kuuchukua”

“Harishi hatakuja tena leo. Mnaweza hata kuja nyote”

Nikawatazama wenzangu.

“Eti mnasemaje?”

“Akituletea huku itakuwa bora” Haji akasema.

“Tutakuwa tunamsumbua. Tungekwenda tu kwa vile ametuhakikishia kuwa leo hakuna tatizo” nikawambia wenzangu.

“Haya twendeni ila tusikae sana” Shazume akasema.

Tukaondoka pamoja na Yasmin kuelekea katika lile jumba la Harishi.

“Tangu mmekuja nyinyi nimejisikia kuchangamka sana” Yasmin alituambia tukiwa njiani.

“Kikwazo chetu kikubwa ni huyu Harishi. Kama si yeye tungekuwa na furaha sana” nikasema.

“Roho zetu sasa zina wasiwasi. Kila siku mmoja wetu anakufa. Tulikuwa watu saba, sasa tumebaki watatu” Haji akalalamika.

“Ni kweli Haji lakini kama nyinyi mtakuwa makini mnaweza kusalimika” Yasmin akatuambia.

“Yasmin unatuambia ukweli? Tutasalimikaje? Hata kama hatutauawa na Harishi tutakaa katika kisiwa hiki hadi lini?” nikamuuliza Yasmin.

“Kwani mimi nitakaa hadi lini?” Yasmin akatuulisa. Sauti yake ilikuwa imebadilika.

“Wewe mwenyewe umeshajitolea” nikamjibu.

“Kwa sababu sijipendi?”

“Hapana, si hivyo”

“Basi mimi na nyinyi ni sawa tu. Kama mimi nimejitolea na nyinyi mjitolee kama mimi. Muwe tayari kwa lolote”

“Sisi tumeshajitolea Yasmin. Hatuna la kufanya” nikamwambia Yasmin aliyekuwa amekasirika kidogo.

“Tunaona juhudi zako Yasmin” nikaendelea kumwambia. “Kama si wewe kutupokea kwa nia moja tungekuwa tumeshakufa kwa kuhangaika na njaa.

Tulipofika kwenye lile jumba tulipumzika ukumbini. Yasmin alituletea karata kisha tukaenda kupika uji. Uji ulipokuwa tayari Yasmin alituletea tukanywa. Huji huo ulikuwa umechanganywa na asali. Tuliposhiba Yasmin aliondoka tena kwenda kupika chakula cha mchana. Sisi tuliendelea kucheza karata, tulipochoka tukalala hapo hapo. Yasmin ndiye aliyekuja kutuamsha.

“Wenzangu kumbe mmelala?” akatuuliza.

“Ah! tumepitiwa na usingizi bila kujijua” nikamwambia na kumuuliza “Umeshapika?”

“Nimeshapika, kwani mna njaa niwapakulie?”

“Bado kwanza. Tusubiri kidogo”

“Naona mko wachovu sana. Twendeni baharini mchangamke kidogo”

Kwa vile hatukuwa na la kufanya tukakubaliana na wazo la Yasmin la kwenda baharini. Kisiwa hicho kilikuwa na fukwe nzuri zenye mchanga mweupe.

Tukiwa kwenye fukwe za kisiwa hicho tulibuni michezo mbalimbali ya kujichangamsha ikiwemo kukimbizana. Mwisho tuliamua kujitosa kwenye maji na kuogelea tukiwa na nguo zetu.

Yasmin alikuwa hodari wa kuogelea. Alituambia alipokuwa Comoro kila siku za jumapili alikuwa akienda kuogelea na ndugu zake.

Tulipochoka kuogelea tulikaa kwenye fukwe hadi tukakauka maji. Tukaondoka kurudi katika jumba la Harishi

Yasmin alikwenda kuoga maji baridi. Alipomaliza na sisi tulikwenda kuoga. Hatukuwa na nguo za kubadili.

Yasmin alitupa mashuka tukajifunga. Zile nguo zetu tulizifua na kwenda kuzianika nje kwenye jua.

Tulipomaliza kuanika nguo ndipo Yasmin alipotuandalia chakula, tukala. Wakati tunakula alituambia kuwa tunaweza kuendelea kushinda hapo kwake hadi jioni lakini Haji akapinga ushauri wake na kutaka tuondoke tukimaliza chakula.

Baada ya chakula tulikubaliana kuwa turudi katika ile nyumba tuliyohamia. Tukamuaga Yasmin na kuondoka.

“Sasa wenzangu mna ushauri gani, hali ya hapa ndiyo kama hii tunayoiona?” nikawauliza wenzangu mara tu baada ya kufika kwenye ile nyumba

“Kwani wewe una ushauri gani?” Haji akaniuliza.

“Nia yetu sote ni kuondoka katika kisiwa hiki. Sasa nataka tujadili njia itakayotuwezesha kuondoka. Ni vizuri kila mmoja akatoa wazo lake alilonalo” nikasema.

“Ni kweli ulivyosema lakini tunajikuta tumekwama, tusingekuwa hapa hadi leo” Shazume akatuambia.

“Kwa hiyo hatujui tutaendelea kukaa hapa na Yasmin hadi lini?” nikauliza.

“Ukweli ndio huo” Haji akanikubalia.

Nikatikisa kichwa changu kusikitika, baada ya hapo sote tukawa kimya.

Yalipofika majira ya saa kumi na mbili jioni Yasmin akaja.Alikuwa ametuletea chakula cha jioni. Ulikuwa ni wali ule ule tuliokula mchana. Tukakiweka chakula hicho kusubiri usiku.

Yasmin akataka nimsindikize arudi. Nikawambia wenzangu “Namsindikiza Yasmin”

“Usije ukachelewa kurudi. Kumbuka usiku umekaribia” Shazume akaniambia.

“Sitachelewa” nikamjibu.

Tukaondoka na Yasmin. Tukiwa njiani Yasmin alinitazama machoni mwangu kisha akaniambia.”Nimefurahi sana leo kuwa peke yetu mimi na wewe”

“Kwanini?” nikamuuliza.

“Tangu juzi hatujapata nafasi ya kuwa pamoja peke yetu. Mara nyingi unakuwa na wenzako. Jana jioni nilitaka kukwambia nisindikize lakini marehemu Masudi akawahi yeye. Sikuweza kumkatalia. Najua roho ilikuuma na mimi pia iliniuma” Yasmin akaniambia.

“Unajua jana niliwafuatilia nikawakuta mnafukuzana ndani. Kuna wakati marehemu alikushika kiuno mkaanguka chini pamoja”

Nilipomwambia hivyo Yasmin alinywea.

“Kumbe ulikuja kutuchungulia?” akaniuliza.

“Nilikuja, nilipouona mchezo wenu nikaamua kurudi”

“Si mchezo wetu. Masudi ndio alikuwa analazimisha. Alikuwa akinitaka kimapenzi nikamkatalia” Yasmin aliniambia.

“Basi tusimseme sana kwa sababu ameshakufa lakini nilishituka”

“Naomba unisamehe kwa hilo kama limekuudhi”

Nikanyamaza kimya.

“Umeshanisamehe?” Yasmin akaniuliza huku akinitazama machoni mwangu. Alinitazama kwa macho ya huruma sana.

“Kwani wasiwasi wako ni wa nini?”

“Nataka unisamehe!” Yasmin akasisitiza.

“Nimekusamehe”

“Sasa tusizungumze tena habari hiyo. Tuzungumze yanayotuhusu mimi na wewe. Kama tutafankiwa kuondoka katika kisiwa hiki utanioa?”

“Wewe ndio uniambie mimi kama utakubali kuolewa na mimi”

“Mimi niko tayari hata sasa hivi”

“Unadhani wazazi wako watakubali?”

“Watakubali”

“Ujue kuwa wewe ni binti wa rais na mimi ni mtoto wa kimasikini”

“Kusema hivyo si sahihi. Sasa hapa tulipo mimi na wewe tuna tofauti gani?”

“Kwa hapa tuko sawa ila ukirudi kwenu wewe utakuwa mwana wa rais”

“Huo ni ufinyu wa mawazo ya binaadamu. Binaadamu wote ni sawa. Mfano halisi ni wa hapa tulipo. Umesema tupo sawa, basi tutakuwa sawa popote. Hata kama wewe ni mtoto wa kimasikini lakini nimekupenda, utakataa?”

“Labda wewe unikatae mimi”

“Una majibu yasiyoniridhisha. Kwanini huniambii kuwa unanipenda na utanioa. Mimi nataka utamke hivyo”

“Nimekupenda na nitakuoa”

Yasmin nilipomwambia vile alitabasamu. Nilihisi alikuwa akijaribu kuufariji moyo wake uliokosa mapenzi kwa muda mrefu.

“Yasmin unaweza kusema maneno hayo hapa kwa vile hatuna matumaini ya kupona. Lakini kama tutafanikiwa kuondoka hapa unaweza kubadilika na kuniona mimi kama takataka”

“Nakuhakikishia kaka yangu mpenzi sitabadilika. Mimi si kinyonga”

“Tuombe tuokoke katika balaa hili lililotukabili”

“Ishaalah tutaokoka. Tena wewe ndio utaniokoa mimi”

“Sio wewe uniokoe mimi?”

“Mimi nataka wewe uniokoe mimi”