Dili iliyokufa - 43
ILIPOISHIA
Hapo ndipo nilipokumbuka. Wakati ule nilipokuwa nakwenda kwake kufuatia dawa ya mume wangu akanichukua hadi mahali hapo ambapo alikwenda kuniingiliakimwili akajidaiananifanyia dawa, kumbe alikuwa akinizuga mimi. Na kutoka siku ile sikutamani tenakurudi kwa mume wangu.
Sasa kilichomshinda mganga huyokukieleza wazi ni kuniambiakwamba mahali hapo ni pale tulipokwenda akaniingiliakimwili.
“Nimeshapakumbuka”nikamwambia.
SASA ENDELEA...
“Basi ndio hapo hapo.Pale ndio mzimuni kwangu. Mambo yangu yote ya kiganga nayachukua pale”
Nilitaka nikatae kwenda kwa sababu nilivyowasikia wakisema na mke wake ni kuwa ameambiwa na majini wake kuwa siku yangu ni leo kisha akasema kafara la majini hao hufanyika usiku na akaongeza zaidi kwa kusema kuwa kama nitakwenda na mganga huyo peke yetu ninawezakushituka.
Hapo nikapata tafsiri kuwa huenda ninakwenda kutolewa kafara mimi!
Nikaona kukataa ile safari kunaweza kuniletea matatizo mengine. Yule mganga anaweza kuhisi nimewashitukia na hivyo wanaweza kunifanya lolote baya kabla ya polisi kutokea.
Nikamwambia yule mganga.
“Sawa”
“Lakini si kwa sasa, tutasubiri jualitakapokuchwa ndio tuondoke. Wewe na huyo mke mwenzako ndio mtatangulia kwenda”
“Sawa. Hakuna shida”
“Sasa nenda ukabadili nguo upumzike kidogo kwa vile unatoka mjini”
“Sawa”
Nikainuka na kutoka mle chumbani. Niliingia katika kile chumba nilichokuwa ninalala nikabadili nguo kumridhisha mganga huyo ili asijue kama sikuwa mwenzake tena. Sikutaka kumuonesha dalili yoyote ya mabadiliko ambayo yangemtia wasiwasi.
Nikiwa mle chumbani baada ya kubadili nguo nilimtumia meseji mume wangu nikamjulisha kuhusu ile safari ya kwenda mzimuni. Akaniambia na yeye atawajulisha polisi.
Baadaye akanitumia meseji na kuniuliza kama ingekuwa vyema polisi wawasili kwa muda ule kabla hatujaondoka kwenda huko mzimuni.. Niakamjibu “Ndiyo”
Baadaye tena mume wangu akanitumia meseji kunijulisha kwamba wako njiani wanakuja na polisi.
Yule mganga alikuwa mtu wa kushituka shituka. Mara akanifuata mle chumbani akaniambia.
“Mke wangu naona muda umewadia. Mnaweza kutangulia kwenda sasa”
Kwanza niliguna nikamtazama yule mganga kwa jicho kali. Nilivyoona atanigundua kuwa nilikuwa na kitu nikainamisha uso wangu chini.
“Sawa, Ngoja nijiandae” nikamwambia kwa sauti ya chini.
Mganga huyo alipoondoka kwenye mlango nikamatumia meseji mume wangu kumjulisha kuwa tunaondoka kwenda huko mzimuni ambako nilikuwa sijajua tunafuata nini.
Mume wangu alinitumia meseji kutaka kujua huko mzimuni tulikokuwa tunakwenda ni wapi lakini sikuweza kumjibu kwani muda ule ule mke mkubwa wa yule mganga akaingia mle chumbani.
“Umeshajitayarisha?” akaniuliza.
“Tusubiri kidogo” nikamwambia.
“Tusubiri nini?”
Sikuwa na jibu la maana, nikajikuta nikimwambia.
“Nataka niende nikajisaidie”
Nilimaanisha kwenda haja.
“Haya nenda. Unajua muda nao unakwenda”
Nikatoka na kuelekea maliwatoni. Lengo langu lilikuwa kuvuta muda ili hao polisi wanaokuja watukute pale pale. Nikaingia maliwatoni na kumtumia meseji mume wangu kumwambia waharakishe.
Nilipoona muda unazidi kwenda nikatoka maliwatoni. Mwanamke alikuwa akinisubiri uani. Nikaingia chumbani. Sikuwa na kitu chochote kilichonipeleka humo zaidi ya kupoteza muda. Nikamuoona na yeye anaingia. Nikajidai kuweka vitu vyangu sawa kisha tukatoka.
Tukaanza safari ya kwenda huko mzimuni. Nilikuwa nimechukia kuliko maelezo. Nilikuwa nikizisikia meseji zikiingia kwenye simu yangu nikajua zinatoka kwa mume wangu lakini sikuweza kuzisoma wala kuzijibu mbele ya yule mwanamke.
Kila nilipopiga hatua chache nilikuwa natazama nyuma kuwaangalia wale polisi lakini sikuwaona. Tulitembea mwendo mrefu mpaka tukapotea katika lile eneo. lakini njia nilikuwa naifahamu na ningeweza kumuelekeza mume wangu endapo ningepata nafasi ya kutumia simu.
Nilikuwa siwezi kupiga wala kutuma meseji kwa sababu ya yule mwanamke niliyekuwa nimefuatana naye. Hivyo nikaona niendeleea kwenda ila mara kwa mara nilikuwa natazama nyuma.
Yule mwanamke naye akawa anatazama nyuma baada ya kuniona mimi nikifanya hivyo mara kwa mara.
Niliporudia tena kwa mara nyingine aliniuliza.
“Unatazama nini?”
“Natazama nyuma kwa sababu za kiusalama. Nataka nihakikishe kuwa tuko salama”
“Mbona huku kwetu ni salama. Hakuna matatizo ya wahuni wala wakabaji kama sehemu zingine”
“Kwenye sehemu sehemu za vichakavichaka kama hizi, unaweza kuona watu wanakufuata lakini si watu wazuri”
“Ni kweli lakini huku kwetu sijaona matukio ya aina hiyo. Kuna siku ninatumwa peke yangu na ninakwenda na kurudi bila matatizo”
“Pengine ni wasiwasi wangu tu. Nahisi labda kuna watu wanatufuata ndiyo maana natazama nyuma kila wakati”
“Usiwe na wasiwasi, tupo salama”
Tukaenda huku tukizungumza mpaka tukafika katika hilo eneo ambalo siku ya kwanza kufika ilikuwa ni siku ile niliyokuja na mganga, tukaingia katika huo mzimu wake akanifanyia mambo ya ajabu kisha tukaondoka.
Mbali ya huo mzimu ambao ulizungukwa na mibuyu mitatu, kulikuwa na nyumba moja pembeni. Ilikuwa nyumba iliyojengwa kwa miti na udongo. Tukaenda katika nyumba hiyo.
Yule mwanamke akafungua mlango akaingia ndani.
“Karibu, pita ndani” akaniambia.
Nikatazama nyuma kisha nikaingia. Ndani kulikuwa kiza. Akaenda kufungua mlango wa kutokea uani na kuuacha wazi. Sasa kidogo kukawa na mwanga.
“Hii ndiyo nyumba yetu. Wenyewe tukija tunafikizia humu” akaniambia yule mwanamke halafu akafungua mlango wa chumba kimoja wapo.
Akaingia ndani. Baada ya muda kidogo akatoa kichwa na kuniambia.
“Ingia”
Nikaingia. Alikuwa amewasha taa ya kibatari ili kuleta mwanga kwani chumba hicho hakikuwa na dirisha na kilikuwa kimejaa makorokoro.
Kulikuwa na kiti kimoja cha marimba, akaniambia.
“Kaa hapo kwenye kiti”
Nikakaa. Wakati nakaa akaniambia tena.
“Subiri hapo hapo”
Aliuponiambia hivyo akatoka mle chumbani. Na mimi nilitaka atoke ili nipate nafasi ya kutumia simu yangu.
Nikatoa simu yangu na kuishika mkononi. Nikajaribu kupiga namba ya mume wangu lakini niligundua mahali nilipokuwa ama hapakuwa na mtandao au kulikuwa na matatizo ya mtandao. Simu haikwenda. Nikagwaya.
Wakati nazungusha macho yangu huku na huku kukitazama kile chumba huku nikiwazia hatima yangu nilisikia harufu kama ya mafukisho ya mashetani kisha nikasikia sauti ya yule mke wa mganga ikinong’ona kutokachumba cha pili.
“Enyi wafalme wa kiti hiki ninawaomba mje mule mhanga wenu, muda umeshafika. Mje mmoja mmoja. Utaanza wewe baba wa majini na mke wako kisha watafuatia na hao masubiani ambao ni wasaidiziwako…”
Yale maneno yalinishitua. Nikajiuliza ni viumbe gani wanaoitwa waje wale mhanga wao na mhanga huo ni upi?
Ghafla nikasikia sauti nyingine ambayo ilikuwa ni sauti ya yule mganga lakini ilikuwa inakoroma.
“Ndiyo nimekuja…mimi mfalme wa majini…nataka nianze kula mhanga wangu…hauwezi tena kuendelea kuishi katika nyumba yangu…muda wake wa kutolewa kafara umeshafika…”
Sasa moyo ulikuwa ukinienda mbio huku nikijiuliza ni nani anayeambwa maneno hayo wakati mimi sikuwa katika chumba hicho.
Nikaona nisimame ili nitoke kule chumbani. Nikasimama haraka na kupiga hatua kuelekea kwenye mlango. Ghafla nikamuona mtu aliyevaa joho lenye rangi tatu nyeupe, nyeusi na nyekundu akiingia mle chumbani.
Ingawa nilimtambua kuwa alikuwa ni yule mganga lakini hakuwa katika sura yake kamili. Alikuwa ameacha kinywa wazi. Meno yake ya mbele yalikuwa yamerefuka na yalikuwa yanatoka damu. Macho yalikuwa yamemtoka.
Ule weusi wa macho haukuwepo. Macho yake yalikuwa ni meupe tu. Kwa maneno mengine hayakuwa na mboni.
Alikuwa ameinua mikono yake kama vile alikuwa anataka kuvamia kitu. Vidole vilkuwa vimekaza na kucha zilikuwa ndefu kuliko za kawaida. Hali ya yule mganga ilinishitua zaidi.
Nikawa ninarudi nyuma kumkwepa huku nikimtazama kwa mshangao.
Wakati narudi nyuma, yeye alikuwa akinifuata kwa taratibu mikono akiwa ameiinua vile vile kama aliyetaka kunivamia. Ile sauti ya kukoroma ilikuwa ikisikika kutoka midomoni mwake.
“Siku zako za kuishi zinaisha leo. Mimi ni Kashkash,jini mnywa damu za watu kila mwaka mara tatu…mimi ndiye niliyekuchagua uolewe na kiti wangu ili muda ukifika ninywe damu yako. Sasa muda huo umeshafika, tulia nilekaramu yangu…!”
Mikono yake ikanivamia ghafla. Nilipiga ukulele mmoja tu kisha sauti yangu ikapotea. Niliendelea kupiga kelele lakini sauti ilikuwa haisikiki. Nilikuwa kama ninayepiga kelele kimoyomoyo au kwenye ndoto.