Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Khadija Kopa avunja ukimya talaka ya Zuchu na Diamond

KOPA Pict


MAMA mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Zuchu, mkongwe wa taarab Khadija Kopa, amesema hana taarifa zozote kuhusu hatua ya binti yake kutangaza kuachana na mumewe, Diamond Platnumz, huku akisisitiza kuwa masuala ya ndoa ni ya kawaida na yapo mikononi mwa Mungu.


Akizungumza na Mwanaspoti, Khadija alisema hajawasiliana na Zuchu kuhusu suala hilo na kama kweli kuna mchakato wa talaka unaoendelea, anaamini binti yake ndiye atakuwa wa kwanza kumweleza kabla ya mtu mwingine yeyote.


“Mimi sijui chochote kuhusu hilo. Kama kweli Zuchu ameomba talaka, yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuniambia. Masuala ya ndoa ni mapenzi ya Mungu, nani asiyejua kwamba watu wengi hupitia changamoto kwenye ndoa?” Alisema Khadija Kopa.

KOP 01

Kauli ya Khadija imekuja siku chache baada ya Zuchu kutangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa yeye na Diamond Platnumz wametengana na wako katika mchakato wa talaka, akieleza kuwa baada ya miaka sita ya uhusiano ameamua kujichagua mwenyewe, kuponya maisha yake na kuelekeza nguvu kwenye afya pamoja na kazi zake.

Diamond na Zuchu, ambao walithibitisha kufunga ndoa mwaka 2025, walikuwa miongoni mwa wanandoa waliofuatiliwa zaidi katika tasnia ya burudani nchini.

Tangu walipoanza uhusiano wao, walipitia vipindi vya kuachana na kurudiana kabla ya kufunga ndoa, huku migogoro mbalimbali ikiendelea kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

KOP 01

Hii si mara ya kwanza kwa Khadija Kopa kuzungumzia ndoa ya binti yake. Mwaka 2025 aliwahi kuthibitisha kwa Mwanaspoti kuwa Diamond na Zuchu walikuwa wamefunga ndoa halali, akieleza kuwa ndoa ni jambo la kheri na kwamba furaha ya Zuchu ndiyo furaha ya familia yao.

Kwa sasa, mashabiki wa wawili hao wanaendelea kusubiri kuona kama Diamond Platnumz atazungumza hadharani kuhusu kauli ya Zuchu na mchakato wa talaka, huku wengi wakifuatilia hatma ya mmoja wa uhusiano uliotikisa zaidi ulimwengu wa burudani Afrika Mashariki.