Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu anapiga kotekote

ZUCHU Pict

Muktasari:

  • Ladha za Bongo Fleva kuanzia Taarab, Singeli hadi Amapiano, Zuchu amekuwa akijaribu midundo mbalimbali na jambo kubwa zaidi ni kila anapobadilisha ladha, amekuwa akiwafikia wasikilizaji wapya bila kupoteza wale aliowajenga.

KUNA wasanii wanaojenga jina kwa kushikilia aina moja ya muziki, lakini kwa msanii Zuhura Othaman ‘Zuchu’ mambo yamekuwa tofauti. Tangu alipoingia rasmi kwenye Bongo Fleva mwaka 2020, ameonyesha uwezo wa kuimba katika ladha tofauti na bado akabaki na mashabiki wake.

Ladha za Bongo Fleva kuanzia Taarab, Singeli hadi Amapiano, Zuchu amekuwa akijaribu midundo mbalimbali na jambo kubwa zaidi ni kila anapobadilisha ladha, amekuwa akiwafikia wasikilizaji wapya bila kupoteza wale aliowajenga.

Uwezo huo hauji kwa bahati mbaya,Zuchu amekulia katika mazingira ya muziki akiwa binti wa mkongwe wa Taarab, Khadija Kopa. Sauti  yake ilionekana kuwa na ladha iliyofanana na Taarab, huku urithi huo ukiendelea kuonekana katika baadhi ya kazi zake.


ZUCH 03

TAARAB NDIO MSINGI

EP yake ya kwanza, I Am Zuchu, ilikuwa na nyimbo zilizochanganya Taarab, Afro Pop hasa za mapenzi. Miongoni mwa zilizotajwa katika mkusanyiko huo ni Wana, Kwaru, Raha, Ashua na Mauzauza, ambayo alimshirikisha mama yake, Khadija Kopa.


ZUCH 01

BONGO FLEVA NDIO NYUMBANI

Katika Bongo Fleva, Zuchu amejenga sehemu kubwa ya jina lake kupitia nyimbo kama Sukari, Kwikwi, Utaniua, Mwambieni, Jaro, Cheche, Litawachoma na nyingine nyingi.

Kundi hili la nyimbo linamlenga zaidi msikilizaji wa Tanzania na Afrika Mashariki, huku Wana, Litawachoma, Sukari, Kwikwi, Mwambieni na Utaniua zikitajwa miongoni mwa kazi zake zinazolenga soko hilo.

Mafanikio yake kwenye eneo hili pia yalionekana mwaka 2024, na alikuwa msanii wa kike aliyeongoza kwa streams Tanzania kwenye Spotify Wrapped  mwaka huo. Wimbo wake Zawadi pia uliingia miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri zaidi nchini.


ZUCH 02

SINGELI NAYO

Zuchu pia ameonyesha hana hofu ya kuingia kwenye Singeli, aina ya muziki yenye kasi ambayo mara nyingi huhitaji nguvu tofauti ya uimbaji na uwasilishaji.

Singeli kama Nyumba Ndogo ya mwaka 2021, Hujanizidi aliyomshirikisha D Voice mwaka 2024 na Afande akiwa na Dogo Paten mwaka 2025, kwa sasa amekuja na Kucheza unajua aliyeimba na Desmile inayoshika nafasi ya pili YouTube.


AMAPIANO HAIJAACHWA MBALI

Kwenye Amapiano, alijaribu bahati yake kupitia Kitu, wimbo aliomshirikisha Bontle Smith na Tyler ICU kutoka Afrika Kusini, huku Apple Music ikiiorodhesha kama single ya Dance. YouTube ya Zuchu pia ina video rasmi ya Kitu, iliyotolewa Desemba 22, 2021.


ZUCHU Pict

KUCHEZA KILA UPANDE

Uwezo huu wa Zuchu wa kuvuka midundo umeonekana pia kwenye albamu yake ya kwanza, Peace and Money, iliyotoka Desemba 2024 ikiwa na nyimbo 13.

Albamu hiyo ilichanganya Afrobeat, Bongo Fleva, Singeli na sauti nyingine za kisasa. Ndani yake kuna Wale Wale, Hujanizidi, Nimechoka, Mama, Mwizi, Antenna na nyingine, huku akiwa na wasanii kutoka Tanzania na Afrika.

Hapo ndipo siri ya Zuchu inapoweza kuonekana si kwamba kila wimbo wake ni wa mfumo moja, bali ana uwezo wa kuchukua ladha tofauti na kuifanya ibebe utambulisho wake.

Na kwa kuwa mashabiki wameendelea kumpokea katika kila upande, jambo hilo limekuwa sehemu ya sababu inayomfanya Zuchu aendelee kuwa miongoni mwa wasanii wa kike wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa Tanzania.