Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yakwepa lawama mauzo tiketi za Dabi

Muktasari:

  • Mchezo huo umepangwa kuchezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Jumamosi, Oktoba 10, 2026 kuanzia saa 1:00 usiku.

Wakati hadi sasa tiketi za mechi ya Ligi Kuu ya Watani wa Jadi, Simba na Yanga zikiwa hazijaanza kuuzwa, wenyeji wa mechi hiyo ya Ligi Kuu, Simba wamejivua mzigo wa lawama.

Klabu hiyo imesema kwamba haihusiki na mchakato wa mauzo ya tiketi za mechi hiyo na badala yake jambo hilo liko mikononi mwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

“Kumekua na maswali mengi kutoka kwa mashabiki wetu kuhusiana na uuzwaji wa tiketi za mechi dhidi ya Yanga itakayochezwa Jumamosi, 10 Oktoba, 2026 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambapo licha ya viingilio kutangazwa rasmi lakini bado uuzwaji haujaanza.

“Tunapenda kuwataarifu mashabiki kuwa kwa sasa klabu haina mamlaka juu ya upatikanaji wa mzabuni wa tiketi kwa mechi zilizo chini ya TFF/TPLB tofauti na ilivyokuwa misimu ya nyuma.

“TFF ilitangaza tenda na tumetaarifiwa kuwa mchakato wa kumpata mzabuni husika umekamilika ambapo mpaka sasa uongozi wa klabu haujaweza kumfahamu mzabuni huyo,” imefafanua taarifa ya Simba.

Simba imewataka mashabiki wake kuwa na subira na utulivu katika kusubiria taarifa rasmi.

“Hata hivyo kwenye mfumo wa tiketi wa sasa tayari mechi zinazochezwa Oktoba 8 na 9 zimeanza kuuzwa hatua ambayo imeongeza presha na sintofahamu kutoka kwa mashabiki juu ya tiketi za mchezo wa Dabi ya Kariakoo.

“Aidha, Klabu imefanya jitihada za kujua hatma ya mfumo wa tiketi utakaotumika na kupata suluhisho la haraka kuelekea mchezo huo ili kurahisisha zoezi la ununuzi kwa kuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya mchezo.

“Tunawaomba mashabiki wote kuwa na subira wakati Uongozi wa Klabu unasubiri mwongozo wa TFF/TPLB kuhusiana na uuzwaji wa tiketi na mapendekezo tuliyowakilisha,” imefafanua taarifa ya Simba.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Jumamosi, Oktoba 10, 2026 kuanzia saa 1:00 usiku.