Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ludacris si kinyonge kwa dada yetu Eudoxie!

LUDA Pict

Muktasari:

  • Ludacris ambaye mwaka 2011 alikuja Tanzania kufanya show akitumbuiza katika viwanja vya Leaders Club, anatajwa na Eudoxie kama baba bora katika familia yao yenye watoto wanne.

Rapa wa Marekani, Ludacris ni shemeji yetu kabisa kwa sababu amemuoa mrembo kutokea Afrika, Eudoxie Mbouguiengue ambaye uhusiano wao umedumu kwa miaka 18, huku wakiendelea kuacha alama kupitia misaada wanayotoa.

Ludacris ambaye mwaka 2011 alikuja Tanzania kufanya show akitumbuiza katika viwanja vya Leaders Club, anatajwa na Eudoxie kama baba bora katika familia yao yenye watoto wanne.

Ikumbukwe Ludacris, mkali wa kibao cha My Chick Bad (2010) akimshirikisha Nicki Minaj, alivuma zaidi kupitia albamu yake ya pili, Back For The First Time (2000), ukiwa ni mradi wake wa kwanza tangu aliposaini Def Jam Records.

Kwa mara ya kwanza Ludacris na Eudoxie walikutana mwaka 2018 katika hafla ya kuchangisha fedha (LudaDay) ambayo ilifanyika jijini Atlanta, Marekani. Ludacris amekuwa akiandaa tukio hilo la kila mwaka tangu 2005.

Lengo la tukio hilo ni kuwakutanisha watu wa Atlanta kwa ajili ya kushiriki katika huduma za kijamii kwa kuchangia fedha ambazo zitatumika katika Ludacris Foundation na taasisi nyingine za kijamii zinazosaidia watoto.

Mwaka 2018, Eudoxie akiadhimisha miaka 10 tangu alipokutana na Ludacris, katika ukurasa wake wa Instagram alisema walikutana Agosti 30, 2008, huku akitania Ludacris hakupata nafasi hata ya kumpiga busu hadi 2009.

Eudoxie alisema anafurahi aliweza kuufanya uhusiano wao udumu kwa sababu hakuna mtu mwingine ambaye angependa kuishi naye zaidi ya Ludacris. Alisema baada ya miaka 10 ya kuwa pamoja, walijikuta wakiwa ni marafiki wa karibu zaidi na wazazi yenye ushirikiano mkubwa.

Ludacris alimvisha Eudoxie pete ya uchumba hapo Desemba 26, 2014 wakiwa safarini ndani ya ndege, na saa chache tu baada ya kuchumbiana, wawili hao walifunga ndoa katika sherehe ya kushtukiza nyumbani kwa kina rapa hiyo.

Wakati huo, mwakilishi wa Ludacris alithibitisha wawili hao walifunga ndoa yao ya faragha kama Ludacris alivyokuwa  amepanga, huku chanzo kin gine kili eleza Eudoxie alitaka sherehe ambayo haina mambo mengi.

Akizungumza na mtandao wa People mnamo Juni 2021, Ludacris alisema mke wake alikuwa na kila sifa ambayo aliikuwa akitarajia mwenza wa maisha yake awe nayo!.

“Ninapenda jinsi ambavyo Eudoxie amekuwa na shauku kubwa ya kufanikisha malengo ambayo amejiwekea maishani, inapendeza sana kuwa naye,” alisema Ludacris, mkali wa filamu, End of the Road (2022).

Ludacris ambaye pia ameonekana katika filamu za The Fast and the Furious, alisema alihisi kwamba alikuwa amefikia hatua ya ukuaji (uko mavu) uliomruhusu kuwa mu me, hivyo muda wa kufunga ndoa na Eudoxie ulikuwa sahihi kabisa kwake.

Hadi sasa tayari wana watoto wawili ambao wote ni wa kike, mtoto wao kwanza, Cadence Gaelle alizaliwa Juni 4, 2015, na wa pili, Chance Oyali, alizaliwa Julai 28, 2021. Hata hivyo, Ludacris tayari alikuwa ana watoto wengine wawili wa kike, Karma (2001) na Cai (2013) ambao aliwapata katika mahusiano yake yaliyotangulia.

Ludacris alisema jambo analolipenda zaidi kuhusu kuwa baba wa watoto wa kike ni kila siku huwa tofauti na nyingine kwa sababu kila binti ana mahitaji yake ya kipekee, hivyo naye huendelea kujifunza na kubadilika pamoja nao.

Mwaka 2021, Ludacris kupitia mtandao wa Netflix alitoa vipindi vyake vya katuni, Karma’s World ambavyo vinaelezea maisha ya mtoto wake kwanza, Karma. Alisema mabinti zake ndio waliomhamasisha kuanzisha kipindi hicho kwa lengo la kutoa ujumbe wa kujiamini, ubunifu na kuwawezesha watoto.

Katika siku ya baba duniani mwaka 2023, Eudoxie alimpongeza Ludacris kwa kuwa baba anayewapenda zaidi watoto wake, vilevile alimshukuru kwa kujitolea kwake kwa kuhakikisha familia yao iko salama na inapata mahitaji yote muhimu.

Je, Eudoxie ni nani?, mwanamitindo huyu alizaliwa na kukulia Gabon, nchi iliyopo Afrika ya Kati. Kwa mujibu wa kitabu chake, Unspoken Angel: My Story Through Her Eyes (2016), alihamia Marekani akiwa kijana mdogo na wakati huo alikuwa hajui kuzungumza Kiingereza kabisa.

Hata hivyo, alizoea maisha ya Marekani na kujifunza lugha hiyo, lakini hiyo haijawa sababu ya kusahau nyumbani kwao Gabon, mara kwa mara amekuwa akienda huko kusalimia na kutoa misaada. Mwaka 2020, Ludacris pamoja na watoto wao wawili walipata uraia wa Gabon, hivyo kuwa na uraia wa nchi mbili.

Kipindi cha janga la COVID-19, Ludacris alieleza kuwa walikuwa wakituma misaada nchini Gabon kwa ajili ya watoto, pia kwa ajili ya familia ya mkewe. Naye Eudoxie alisema ana ndugu wengi, hivyo walikuwa wakituma vitu mbalimbali walivyovifungasha katika makontena.

Ludacris alisema moja ya mambo yanayofanya familia yao kuwa imara ni utamaduni wao wa kuwasaidia wengine, kushiriki katika shughuli za kijamii kwa kutoa misaada, kujenga familia na kulea watoto wao katika maadili mema.

Vilevile Eudoxie ni mwanzilishi na mfadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Unspoken Angels ambalo huwasaidia wasichana na wanawake waliowahi kukumbana na ukatili, wakiwemo wale kutoka kijijini kwao nchini Gabon.

Kwa mujibu wa mahojiano aliyofanya mwaka 2016, Eudoxie mwenyewe alipitia ukatili akiwa mtoto, hivyo mapito hayo yalimfanya kuanzisha shirika hilo na kuwasaidia watu ambao hawakuwa na sauti ya kuzungumza kuhusu matatizo yao.

Ludacris amekuwa mmoja wa watu waliompa Eudoxie msaada mkubwa katika kuanzisha taasisi hiyo mwaka 2013. Pia amekuwa akihudhuria matukio mbalimbali ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Unspoken Angels. Eudoxie amewahi kumuelezea Ludacris kama rafiki yake mkubwa ambaye amekuwa akimuunga mkono katika ndoto zake.