Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yammy aweka wazi yupo Single

Muktasari:

  • Yammy ametoa kauli hiyo, leo Agosti 19, 2026 kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiwafahamisha mashabiki wake kuwa hana tena uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo ambaye katika kipindi cha hivi karibuni alikuwa akionekana naye katika matukio mbalimbali.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Yasirun Yasin Shaban, maarufu Yammy, ameweka wazi kuwa kwa sasa yupo single baada ya kumaliza uhusiano wake wa kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, Ahmed.

Yammy ametoa kauli hiyo, leo Agosti 19, 2026 kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiwafahamisha mashabiki wake kuwa hana tena uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo ambaye katika kipindi cha hivi karibuni alikuwa akionekana naye katika matukio mbalimbali.

“I’m single na sina mahusiano ya kimapenzi na aliyekuwa mwenza wangu, haya waja, dua zenu zimetimia,” ameandika Yammy.

Kauli hiyo imezua gumzo kwa mashabiki wa msanii huyo, hasa ikizingatiwa kuwa uhusiano wake na Ahmed ulianza kuonekana zaidi hadharani katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.

Kabla ya kumweka wazi, Yammy alikuwa akifanya mambo ya kimapenzi kwa tahadhari bila kumtambulisha moja kwa moja mwanaume aliyekuwa nyuma ya matukio hayo.

Miongoni mwa mambo yaliyowahi kuwasha moto wa mashabiki ni tukio la Siku ya Wapendanao Februari 14, 2026, ambapo Yammy alishirikisha zawadi pamoja na kiasi kikubwa cha fedha alichodai kupewa na mpenzi wake.

Wakati huo, hakumtaja wala kumuonyesha wazi Ahmed, jambo lililowaacha mashabiki wake wakijiuliza kuhusu mwanaume huyo na nafasi yake katika maisha ya msanii huyo.

Hata hivyo, kadiri muda ulivyokwenda, mambo yakaanza kuwa wazi zaidi na Julai 2026, Yammy na Ahmed walionekana pamoja hadharani, huku Ahmed akitambulishwa kama mtu aliyekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo.

Uhusiano huo pia uliingia kwenye upande wa muziki baada ya Ahmed kuonekana katika video ya wimbo wa Yammy uitwao Wasiwasi, uliotoka Julai 31, 2026.

Katika video hiyo, Ahmed alionekana kama muhusika, hali iliyozidi kuwafanya mashabiki kuamini uhusiano wao ulikuwa ukiendelea vizuri na kwamba wawili hao walikuwa wameamua kutoficha tena mapenzi yao.

Mbali na video hiyo, Yammy na Ahmed pia waliwahi kuonekana pamoja katika matukio ya kijamii, ikiwamo baby shower ya msanii Zuchu, ambapo walishiriki kumpongeza kwa kumpa fedha.

Matukio hayo yalifanya uhusiano wao kuendelea kuwa sehemu ya gumzo kwa mashabiki wa Yammy, huku wawili hao wakionekana kuwa karibu katika nyakati mbalimbali.

Lakini sasa, baada ya muda mfupi wa kuonekana hadharani kama wapenzi, Yammy ametangaza kuwa mambo yamebadilika na kwamba kwa sasa hana tena uhusiano wa kimapenzi.

Kauli yake haijaweka wazi sababu ya kuvunjika kwa uhusiano huo, huku Ahmed naye akiwa hajatoa kauli yake kuhusu tangazo hilo la Yammy.