Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wolper ndani ya penzi jipya  starehe, kujiachia...

WOLPER Pict

Muktasari:

  • Wolper, ambaye kwa kipindi cha ndoa yake alionekana zaidi katika maisha ya kifamilia, siku hizi amekuwa akionekana katika sehemu mbalimbali za starehe, hali inayowakumbusha wengi maisha yake ya kabla ya kuingia kwenye ndoa.

BAADA ya ndoa yake na mfanyabiashara Rich Mitindo kuingia kwenye historia, mwigizaji Jacqueline Wolper anaonekana kurudi kwenye maisha yake ya zamani; starehe, kujiachia na sasa katika uhusiano mpya.

Wolper, ambaye kwa kipindi cha ndoa yake alionekana zaidi katika maisha ya kifamilia, siku hizi amekuwa akionekana katika sehemu mbalimbali za starehe, hali inayowakumbusha wengi maisha yake ya kabla ya kuingia kwenye ndoa.

Lakini si starehe pekee inayozua gumzo,  Wolper mwenyewe ambavyo amekuwa akizungumza wazi kuhusu maisha yake baada ya kuachana na Rich Mitindo, huku akisema yupo huru kuendelea na maisha yake.

Na sasa, amekuwa akijieleza kuhusu kuwa na mpenzi mpya huku akitaja pia suala la kusubiri talaka.

Hapo ndipo swali linapokuja: Wolper anasubiri talaka gani, wakati yeye na Rich Mitindo walifunga ndoa ya Kikristo kanisani?


Wolper anarudi kwa kasi?

Kabla ya kuingia kwenye ndoa, Wolper alikuwa miongoni mwa mastaa waliokuwa wakionekana mara kwa mara kwenye matukio mbalimbali ya starehe na burudani.

Baada ya kuingia kwenye ndoa, maisha yake yalibadilika na akaonekana zaidi katika upande wa familia, huku akijenga maisha yake na Rich Mitindo.

Lakini sasa, baada ya uhusiano huo kufikia mwisho, picha nyingine ya Wolper imeanza kuonekana.

Ameonekana tena katika mazingira mbalimbali ya starehe, huku akiwa huru zaidi katika namna anavyozungumzia maisha yake binafsi. Kwa mashabiki waliomzoea Wolper wa zamani, hali hiyo imekuwa kama kumwona mtu aliyerudi kwenye maisha yake baada ya kipindi kirefu cha ndoa. Wolper mwenyewe hajaonekana kuwa na mpango wa kuficha ukurasa huo mpya.


WOLP 01

Penzi jipya lipo

Hapa ndipo stori inakuwa tamu zaidi.

Wolper amekuwa akijieleza kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano na ana mpenzi, huku akizungumza pia kuhusu kusubiri kukamilika kwa mchakato wa talaka.

Kauli hiyo imeanza kuwafanya watu wajiulize maswali kadhaa.

Kama tayari amesema yeye na Rich hawapo tena kwenye mahusiano ya ndoa, na sasa anaendelea na maisha yake pamoja na kuwa kwenye mahusiano mengine, mchakato wa talaka umefikia wapi?


Je, talaka hiyo bado haijakamilika rasmi?

Au neno ‘nasubiri talaka’  linatumika kwa maana ya mchakato ambao aliwahi kuutangaza tangu Januari 2025?

Haya ni maswali ambayo majibu yake yapo kwa wahusika wenyewe, kwa sababu Wolper ndiye aliyewahi kutangaza kuwa yupo kwenye mchakato wa talaka, wakati Rich amekuwa akiepuka kuzungumza kwa kina kuhusu maisha yao ya familia.


WOLP 03

Wolper hakai kimya kuhusu ndoa

Jambo lingine linaloifanya stori hii iwe na uzito ni tangu uhusiano wake na Rich uanze kuyumba, Wolper amekuwa ndiye anayezungumza zaidi kuhusu hali ya ndoa yao.

Januari 2025, Wolper alitangaza hadharani kwamba yeye na Rich Mitindo walikuwa wameachana na kwamba alikuwa kwenye mchakato wa Talaka.

Wakati huo aliwaambia watu wasiingilie mambo yake na Rich, akisisitiza kuwa maisha halisi ya ndoa yao anayajua yeye na mwenzake.


Lakini stori haikuishia hapo.

Mwezi mmoja baadaye, Februari 2025, Wolper aliliambia tena Mwanaspoti walikuwa wamesameheana na kurudiana, akisema migogoro katika ndoa ni sehemu ya maisha na waliona ni busara kuipa nafasi familia yao. Hapo ndipo wengi waliamini ukurasa  wa kuachana umefungwa. Lakini miezi iliyofuata, wawili hao walionekana pamoja katika matukio mbalimbali ya kifamilia, hali iliyowafanya watu waamini huenda walikuwa wamerudisha ndoa yao katika mstari.


Rich yeye kimya

Tofauti na Wolper, Rich Mitindo amekuwa akichagua kutokuwa msemaji wa ndoa yao.

Katika mahojiano na Mwanaspoti baada ya kauli mpya za Wolper, Rich alisema hapendi kuzungumzia mambo ya familia kwenye vyombo vya habari, akisisitiza yeye ni mtu wa kukaa kimya na kumuomba Mungu kila mmoja aendelee na maisha yake. Hilo limefanya simulizi ya ndoa yao kuwa na upande mmoja unaozungumza zaidi na mwingine unaochagua kukaa kimya.

WOLP 02

Na hapo ndipo swali la sasa linapopata uzito zaidi.

Wolper anaendelea kueleza ukurasa wake mpya wa maisha, lakini Rich hajajitokeza kueleza kama mchakato huo wa talaka umekamilika au bado.


Sasa ni maisha mapya

Kwa upande mwingine, Wolper haonekani kama mtu anayesubiri maisha yarudi nyuma. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, amekuwa akizungumza kuhusu mahusiano na mpenzi mpya, jambo linaloonyesha wazi kwamba anaendelea na maisha yake baada ya Rich.

Hii si mara ya kwanza kwa Wolper kuwa wazi kuhusu maisha yake ya mapenzi. Miaka kabla ya ndoa yake, alikuwa akizungumza kwa uhuru kuhusu mahusiano yake na hata mwaka 2020 aliwahi kueleza kuwa alikuwa na wanaume kadhaa waliokuwa kwenye mawasiliano naye huku akitafuta anayemfaa.

Kwa hiyo, sasa anaporejea tena kwenye lugha ya mpenzi, kwa baadhi ya mashabiki inaweza kuonekana kama Wolper amerudi kwenye ule uhuru wa maisha yake ya kabla ya ndoa. Lakini tofauti ni moja kubwa. Safari hii anaingia kwenye mahusiano akiwa ametoka kwenye ndoa, na bado kuna neno ‘talaka’€  linalozunguka.


Ndoa yao ilianza vipi?

Kwa kumbukumbu, Wolper na Rich Mitindo walifunga ndoa ya Kikristo Novemba 19, 2022, katika Kanisa la St. Peter jijini Dar es Salaam.

Ndoa hiyo ilikuwa ya kifahari na ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa filamu, muziki na wafanyabiashara. Wawili hao walikuwa tayari wameanza maisha ya familia kabla ya ndoa hiyo, na baadaye wakaja kupata watoto pamoja.

Miaka miwili baadaye, Januari 2025, Wolper alitangaza kuvunjika kwa ndoa hiyo na kusema yupo kwenye mchakato wa talaka. Baadaye wakapatanishwa, kabla ya mwaka 2026 Wolper kurejea na msimamo ndoa yao imekwisha.