Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wolper afunguka kuhusu penzi la Isarito

WOLPER Pict

Muktasari:

  • Wolper amekuwa akihusishwa zaidi na Isarito kutokana na ukaribu unaoonekana kwenye mitandao ya kijamii, ikiwamo kupenda na kutoa maoni kwenye baadhi ya posti zake, huku baadhi ya picha zikionyesha wapo pamoja kwenye matukio mbalimbali hali iliyowafanya mashabiki kuanza kujiuliza kama kuna penzi jipya limechipuka.

UBUYU wa penzi jipya la mastaa wa filamu Jackline Wolper na Isarito ‘Jitu’ umeendelea kuchafua mitandao, huku kila mmoja akijaribu kusoma alama zinazotokea kati ya wawili hao.


Wolper amekuwa akihusishwa zaidi na Isarito kutokana na ukaribu unaoonekana kwenye mitandao ya kijamii, ikiwamo kupenda na kutoa maoni kwenye baadhi ya posti zake, huku baadhi ya picha zikionyesha wapo pamoja kwenye matukio mbalimbali hali iliyowafanya mashabiki kuanza kujiuliza kama kuna penzi jipya limechipuka.

Wolper alipofuatwa na Mwanaspoti kuhusu sakata hilo, hakutaka kusema moja kwa moja kama yeye na Isarito ni wapenzi au la, badala yake akasema: “Watu waache kuwa na hofu na mapenzi yetu, kama kitu kipo kitajulikana tu.”

Kwa kauli hiyo, Wolper hakukataa moja kwa moja madai hayo.

Wakati huo huo, jina la msanii wa Tamthilia na filamu Mulky  ambaye anadaiwa ni mpenzi wa Isarito, limeingia kwenye sakata hilo baada ya sauti  iliyosambaa mitandaoni wiki iliyoisha ikihusisha suala hilo na madai hayo ya Wolper na Isarito.

Lakini ubuyu hauishii hapo, wapo wanaoamini huenda kinachoendelea kati ya Wolper na Isarito ni kiki ya filamu, kwa kuwa Isarito ni muigizaji na mtayarishaji, huku Wolper akiwa miongoni mwa waigizaji waliohusika kwenye kazi zake. Wolper pia amewahi kuonekana akimpongeza Isarito kuhusu kazi zake za filamu.Hata hivyo, kwa sasa hakuna uthibitisho wa wazi ukaribu huo ni sehemu ya kutengeneza kiki.

Isarito bado yupo kimya, Wolper naye ameacha mlango wazi kwa kusema kama kuna kitu kitajulikana tu. Kwa hiyo, kwa sasa swali limebaki kwa mashabiki: Wolper na Isarito ni penzi jipya au filamu ndiyo imeanza kabla ya kuonyeshwa?