Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usiyoyajua na ukweli kuhusu Baba wa Patrick

Muktasari:

  • Wakati ikisemwa baba mzazi wa mtoto huyo ni Mtangazaji wa Clouds, Casto Dickson wengine wameibuka na kumtaja Peter Zacharia Komu ‘Kossovo’ kuwa ndiye baba halali.

KIFO cha mtoto wa msanii, Rose Alphonce ‘Muna Love’, Patrick aliyefariki juzi jijini Nairobi kinaendelea kutikisa na kuzua utata mkubwa. Ishu ni nani hasa baba halisi wa mtoto huyo.

Wakati ikisemwa baba mzazi wa mtoto huyo ni Mtangazaji wa Clouds, Casto Dickson wengine wameibuka na kumtaja Peter Zacharia Komu ‘Kossovo’ kuwa ndiye baba halali.

Mwanaspoti ambalo limeweka kambi Mwananyamala, nyumbani kwa Peter, anayetajwa kama mume wa ndoa wa Muna na ndiye baba mzazi wa Patrick aliyefariki akiwa katika matibabu kule Nairobi, Kenya linakupa mkanda mzima.

Peter anatajwa ndiye aliyekuwa akimhudumia mtoto huyo kuanzia matibabu, matunzo na ada ya shule.

Katika mazungumzo na Mwanaspoti, Peter amesema Casto si baba wa mtoto huyo na kusisitiza ana vielelezo vyote kuhusu mtoto wake, akiwemo huduma za matibabu.

Amesema yeye ndiye baba wa mtoto na mume halali wa Muna, ambaye alifunga naye ndoa kanisani mwaka 2010 na mwaka 2011 Patrick alizaliwa.

“Mimi ndio baba wa Patrick, na asingekuwa mwanangu nisingempeleka Moshi kumfanyia mila za kwetu, kwanini Muna ananidhalilisha hivi?”

Peter anafichua kisa na mkasa cha Muna kumdhalilisha ni baada ya kumkataza kurudi usiku na mambo mengine yasiyopendeza, ndipo alipoanza kuchukia kwa kuona anabanwa.

“Mbaya zaidi nikaanza kuona kwenye mitandao Casto akimposti mtoto wangu, nikamwambia Muna sipendi na mwambie sitaki achezee familia yangu, kwani mimi sio mtu wa mitandao na nalinda kazi yangu, hivyo siwezi kujidhalilisha kwenye mitandao.

“Ikawa haitoshi, Muna alivyoona nachukia kuhusu Casto kumposti Patrick, basi akawa akitaka kufanya mambo yake ili nichukie anamwambia huyo Casto amposti Patrick kwenye mitandao.”

Kama haitoshi, Peter anasema sio Casto tu, kuna Joel ambaye yuko na Muna Nairobi. Huyu ndiye yuko naye kimapenzi kwa sasa na Muna alishawahi kumtamkia na hadi mtoto amefariki, Joel yuko Nairobi.

“Huyu Casto alishaachana na Muna muda mrefu ndio akahamia kwa Joel,” alisema Peter.

Aidha, Peter alifunguka kila Muna alipotaka pesa alimpatia kwa kuwa alikuwa akimheshimu kama mke wake. Lakini, matokeo yake pesa hizo alikuwa akienda kuzitumia katika starehe na kuonekana kwenye magazeti akidhamini ‘birthday’ za marafiki.

“Acha leo nifunguke, najua watu wanajiuliza kwanini siku zote sikujitokeza baada ya Casto kujitangaza kuwa Patrick ni mtoto wake, ila nilikuwa nalinda heshima yangu pamoja na kwa jamii na ukizingatia mimi sio mtu wa mitandao. Yaani nionekane nagombea mtoto, ambaye najua ni wangu! Na sababu tu za kupishana na mke wangu ndio anakwenda kunikana mtandaoni? Nilishindwa, ila leo achana niseme.

“Na hata siku nilivyomnunulia gari Muna, lile gari alienda kumpa yule mwanamuziki wa Twanga Pepeta (African Stars), Kalala Junior na siku moja nilimkuta nalo pale Mango Garden.

“Nikamuuliza vipi uko na gari la mke wangu, akanijibu amekodisha. Nilivyorudi nyumbani, nilimuuliza Muna, akaniambia kamkodishia lakini, kumbe alikuwa mpenzi wake tena nilifahamu baada ya Kalal Junior na Casto kupigana katika birthday ya mwanangu ambayo sikuwepo. Nilimuuliza Muna akaniambia sio kweli.”

Aidha, Peter anadai tangu mtoto wake ameanza kuumwa mwaka juzi na alikuwa akimhudumia na wakati mwingine Muna alikuwa akilazimisha nitoe pesa haraka akiambiwa asubiri anakuwa mkali.

Anasema kuna wakati alimshauri Muna kwenda na mtoto katika hospitali fulani, lakini hakutaka na alichotaka ni kupewa pesa na sio kupelekwa kwa daktari. Peter anaongeza kuwa, mara ya pili mtoto alipoanza kuumwa, Muna alimwambia amtumie Sh 300,000 na baada ya hapo akamwambia mtoto anatakiwa apelekwe Nairobi kutibiwa.

“Anavyosema simuhudumii nashanga sana,” anasema Peter kwa masikitiko.

Mwanaume huyo anadai Muna alipomwambia mtoto anatakiwa kupelekwa Nairobi, alimwambia asuburi kwa kuwa alikuwa safarini.

“Baadaye alinitumia ujumbe ‘kama hutaki kunitumia acha huyu mtoto sishindwi kumlea, nitamuazima Zamaradi pesa, atampeleka Nairobi.”

“Nilipofika Iringa mjini, nikamtumia pesa, baada ya siku mbili akaniambia zinatakiwa Sh 22 milioni kwa ajili ya kumpeleka Nairobi, nikamwambia kwa sasa sina hiyo yote.

“Nilichofanya nikamkatia tiketi ya ndege na pesa ya kuanzia, lakini matokeo mtoto wangu alisafirishwa kwa basi, ile pesa ya ndege akaichukua.

Kinachomsikitisha Peter, kuna kundi la WhatsAp ambalo Muna alikuwa akichangiwa michango. Anadai alionyeshwa meseji kuwa mkewe anaomba michango kwa ajili ya matibabu ya mtoto.

Anadai hata Zamaradi alimwambia alimchangia Muna Sh1 milioni kwa ajili ya kwenda kwenye matibabu.

“Hapo ndipo nilipogundua Muna anamfanya mwanangu ni biashara, kwa sababu nilishamaliza kila kitu. Sasa nikajiuliza nimekata tiketi ya ndege, lakini kaenda kwa basi. Na hata kama hospitali imempa mtoto uhamisho wa kwenda Nairobi, lazima angeenda na nesi au daktari, lakini hakuna kitu kama hicho,” alisema Peter

Lulu anamjua

baba halali

Peter anamshangaa msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kushabikia msiba wa Patrick kuwekwa Mbezi Jogoo badala ya Mwananyamala.

“Lulu anajua kabisa mimi ni baba wa Patrick, anaelewa kila kitu, sababu hii nyumba unayoiona hapa Lulu ameishi sana. Hata mara ya kwanza alipotoka gerezani alifikia hapa ili kukwepa usumbufu wa wana habari. Na alipokuwa jela mimi ndiye niliyegharamikia chakula. Mke wangu, Muna alipika nikamkodia bajaji kila siku kwa ajili ya kumpelekea chakula Lulu.

“Sasa sijajua kwanini Lulu amejitoa fahamu ya kushughulikia msiba huko Mbezi, badala ya kumshauri mwenzie aniletee damu yangu.

“Lulu anafahamu vitu vingi kati yangu na Muna kuhusu uhalali wa Patrick, nilimpigia simu na kumuuliza kwanini unafanya vitu vya ajabu, akanijibu amepewa maagizo na Muna, hivyo alishindwa kukataa?”

Peter anaonekana kudhamiria kuipigania haki yake ya kupewa mwili wa mwanawe ili aweze kumfanya mazishi.

“Sasa waaache waendelee kuweka msiba huko Mbezi. Tuone kama watazika. Nipo tayari hata kwenda kupima DNA na hapa taratibu za kisheria nimeshaanza kuzifuata,” alisema kwa hasira Peter.

Wema aibuka msibani

Inafahamika wazi kuwa, Wema Sepetu na Muna kwa sasa hawapikiki chungu kimoja, baada ya kutupiana lawama za ushirikina.

Wema ilifikia hatua alimshutumu Muna kuchukua nguo yake ya ndani na kuipeleka kwenye mambo ya kishirikina. Lakini, juzi Wema alipopata taarifa ya msiba wa Patrick, alikwenda nyumbani kwa Peter kutoa pole.

Hata hivyo, Wema alilieleza Mwanaspoti kuwa: “Huwa sina tatizo nikiona nimekosea au nimekosewa, hivyo huu ni msiba na Patrick alikuwa ni mtoto tunayependana sana.

“Watu waache tofauti zao, ndio maana nimekuja kushiriki kwani kuna tatizo? Basi tuombe hizi tofauti zinazojitokeza za wazazi ziishe na kumzika mtoto, ambaye ni malaika wa Mwenyezi Mungu.”

Mama amchana Muna

Kutokana na hayo, ndugu wa Muna ambao ni mama yake mzazi, dada yake, kaka yake, wajomba na mdogo wake wameungana na Peter na kudai wao wanachofahamu baba halali wa Patrick ni Peter.

Ndugu hao walidai Casto wanamsikia mitandaoni tena baada ya Patrick kufikisha umri wa miaka mitano.

Mwanaspoti lilizungumza na Mama Muna, ambaye kila wakati alikuwa akiishiwa nguvu na kupoteza fahamu kutokana na msiba huo.

“Huyu Peter ndio baba halali wa Patrick hivyo ndivyo ninavyojua, ila sifahamu Muna amepatwa na nini? Kwani kitu anachokifanya sio sahihi kwa Peter, wakati ukweli anaujua kabisa.

“Sielewi kabisa na hii sio mara ya kwanza kugawa msiba kwani, mara ya kwanza aliniua baada ya mume wangu kufariki, akaweka msiba Mwananyamala kwa Peter, sisi tukaweka msiba Makongo nyumbani kwa mume wangu, akaenda mochwari kuomba mwili wa baba yake na kuwaambia kuwa, nimefariki, hivyo yeye ndiye atakayechukua huo mwili.

“Bahati nzuri ndugu wengine walikuwepo na huwezi kuamini hadi tunasafirisha mwili wa baba yake hakuna anayeongea naye kwani, alichukua gari nyingine tukakutana kwenye mazishi Musoma.”

Mwanaspoti halikuishia hapo lilizungumza na dada wa Muna ambaye amefunguka familia inafahamu mtoto huyo ni wa Peter na sio Casto.

“Kama Peter sio baba halali wa Patrick kwanini msiba wa baba alilazimisha kuuweka kwa Peter? Na kwanini Patrick anaitwa Patrick Peter? Huyo Casto alikuwa mpenzi wake, nimeanza kumsikia baada ya mtoto kufikisha miaka mitano.”

Baadhi ya mahojiano ya video ya Peter kudai yeye ndiye baba wa Patrick kumfikia Muna akiwa Nairobi na kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika kuwa baba wa mtoto ni Casto na akitulia atazungumza kila kitu.

Mwanaspoti lilimpigia simu Casto ili aweze kuzungumza chochote kuhusu Patrick na mwandishi alipojitambulisha na kumtaka aweka wazi juu ya sakata hili alikata simu.

Tumgeukie Lwaga sasa

Katika sakata hili la msiba linaloendelea, kumeibuka habari zinazodai kuwa Muna kwa sasa anatoka kimapenzi na msanii wa muziki wa injili, Joel Lwaga.

Lwaga anatamba na wimbo uliopata maarufu hivi karibuni ‘Sitabaki kama Nilivyo’ ambao marehemu Patrick aliupenda sana kuuimba enzi za uhai wake. Tetesi za Lwaga kutoka kimapenzi na Muna zilianza miezi minne iliyopita.

Hata hivyo, kwa mujibu wa dada wa Muna, zimeeleza kuwa Muna alipompeleka Patrick Nairobi akiwa na Lwaga.

Hata Patrick alivyofariki dunia Joel aliandika katika ukurasa wake wa Instagram: “Patrick alikuwa pembeni yangu na kuniita dady mara akakata roho.”

Mwanaspoti lilimuuliza dada wa Muna na baadhi ya familia kuhusu uhusiano wa Joel na Muna nao hawakuacha kufunguka:“Ni kweli nilipokwenda Nairobi kumuona Patrick nilimkuta Joel na Muna.