Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujio wa Davido waibua maswali kwa Diamond, S2Kizzy

UGOMVI Pict

Muktasari:

  • Mjadala huo umeongezeka kufuatia ujio wa mwanamuziki wa Nigeria, Davido, nchini Tanzania Novemba 10 mwaka huu, ambapo alikutana na Diamond na kuibua matarajio ya kufanya mradi mwingine wa pamoja, miaka 12 baada ya wawili hao kufanya wimbo ‘Number One Remix’.

KUNA maswali yameibuka kuhusu uhusiano wa kikazi kati ya mwanamuziki Diamond Platnumz na mtayarishaji wa muziki, Salmin Maengo maarufu S2Kizzy, hasa baada ya Diamond kuonekana akifanya kazi na watayarishaji wengine, akiwemo Pablo.

Mjadala huo umeongezeka kufuatia ujio wa mwanamuziki wa Nigeria, Davido, nchini Tanzania Novemba 10 mwaka huu, ambapo alikutana na Diamond na kuibua matarajio ya kufanya mradi mwingine wa pamoja, miaka 12 baada ya wawili hao kufanya wimbo ‘Number One Remix’.

Katika mazungumzo ya mashabiki mitandaoni, baadhi wamekuwa wakijiuliza S2Kizzy yuko wapi katika maandalizi ya mradi huo, huku wengine wakieleza kuwa huenda Pablo amechukua nafasi yake katika timu ya Diamond.

Hali hiyo imeibua mjadala mpana kuhusu kinachoendelea kati ya wawili hao, ambao kwa miaka kadhaa wamekuwa na ushirikiano uliozaa nyimbo mbalimbali zilizofanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva.

Lakini je, Diamond na S2Kizzy wameachana kikazi au ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea katika mfumo wa utayarishaji wa muziki?

OGOM 03

HISTORIA YA DIAMOND NA S2KIZZY

Ili kuelewa mjadala huu, ni muhimu kurejea historia ya ushirikiano wao na namna S2Kizzy alivyojijengea nafasi katika muziki wa Diamond.

S2Kizzy ni miongoni mwa watayarishaji waliopata nafasi kubwa katika muziki wa Bongo Fleva kupitia kazi zake na wasanii mbalimbali, akiwemo Diamond na Rayvanny. Miongoni mwa nyimbo zinazohusishwa na ushirikiano wake na Diamond ni ‘Baba Lao’ na ‘Jeje’. Pia alihusika katika utayarishaji wa ‘Tetema’ ya Rayvanny aliyomshirikisha Diamond, wimbo uliopata mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania. Nyimbo nyingine ni ‘Pepeta’ ya Nora Fatehi na Rayvanny pamoja na ‘Amaboko’ ya Diamond na Rayvanny.

OGOM 02

PABLO AMECHUKUA NAFASI MAZIMA?

Jambo lililoongeza mjadala ni kuonekana kwa mtayarishaji Pablo katika shughuli za muziki zinazohusishwa na Diamond, hasa katika kipindi ambacho macho ya mashabiki yalikuwa kwenye ujio wa Davido na matarajio ya mradi mpya.

Baada ya Diamond na Davido kukutana Dar es Salaam, matarajio ya mashabiki yalikuwa kuona watayarishaji watakaohusika katika kazi hiyo, kutokana na ukubwa wa majina hayo mawili katika muziki wa Afrika. Hata hivyo, kuonekana kwa Pablo kumefanya baadhi ya mashabiki kuanza kulinganisha nafasi yake na ile ya S2Kizzy, wakijiuliza kama kuna mabadiliko ya watu wanaohusika katika utayarishaji wa muziki wa Diamond.

OGOM 01

WIMBO WA ‘HAPPY’ UZINGATIWE

Wakati mjadala ukiendelea, taarifa nyingine muhimu imeibuka kupitia wimbo ‘Happy’ wa Diamond, uliotoka Machi 21, 2026, ambao S2Kizzy amehusika kuutayarisha.

Wimbo huo ulipotoka uliibua mjadala kuhusu kufanana kwa baadhi ya midundo yake na nyimbo za Nigeria. Na katika hilo S2Kizzy alijibu madai hayo katika mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari, akieleza kuwa kazi hiyo ilikuwa na ubunifu wake na ilichochewa na ladha za muziki wa kimataifa.

OGOM 04

WIMBO, MALIPO NA MASWALI

Sehemu nyingine inayoongeza uzito katika mjadala huu ni madai yanayosambaa kuhusu kutokuelewana kunakodaiwa kuhusisha utayarishaji na malipo ya wimbo.

Inadaiwa kulikuwa na wimbo uliotengenezwa na mtayarishaji mwingine, lakini S2Kizzy akauwasilisha kwa Diamond kana kwamba yeye ndiye aliyeutengeneza na baadaye akalipwa fedha. Inaelezwa kuwa mtayarishaji aliyedai kuhusika katika utengenezaji wa wimbo huo alimfuata Diamond akitaka malipo yake, jambo ambalo linadaiwa kumkasirisha msanii huyo. Ikiwa madai hayo yana ukweli, yanaweza kueleza kwa nini masuala ya uaminifu na umiliki wa kazi yanaweza kuwa sehemu ya changamoto katika ushirikiano wa wasanii na watayarishaji.

Hata hivyo, madai hayo bado hayajathibitishwa na ushahidi wa moja kwa moja kutoka kwa Diamond, S2Kizzy au mtayarishaji anayedaiwa kuhusika. Kwa hiyo, hayawezi kuchukuliwa kuwa sababu iliyothibitishwa ya mabadiliko yoyote katika uhusiano wao.


S2KIZZY JINA KAMA MSANII

Jambo lingine linalostahili kuangaliwa ni mabadiliko ya S2Kizzy kutoka kuwa mtayarishaji anayefahamika zaidi nyuma ya pazia na sasa kujitanua kama msanii.

Mtayarishaji huyo ametangaza albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Virus’, ambayo ilipangwa kuzinduliwa Novemba 13, 2026. Katika tasnia ya muziki, hatua hiyo inaweza kuja na changamoto ya kugawa muda kati ya utayarishaji wa kazi za wasanii wengine na kusimamia miradi yake binafsi. Pia inaweza kumpa nafasi ya kujenga chapa yake, kutafuta mashabiki wake na kuingia katika soko ambalo kwa muda mrefu amekuwa akilishiriki akiwa upande wa utayarishaji.

Hata hivyo, kuanza kuimba hakumaanishi kwamba hawezi kuendelea kutengeneza muziki wa Diamond au wasanii wengine. Watayarishaji wengi wamekuwa wakifanya shughuli hizo kwa pamoja bila kuathiri kazi zao za kisanii.