Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Steve Nyerere awauma sikio wanasiasa uchaguzi 2025

Muktasari:

  • Hata hivyo, anafichua kuhusu hilo na mengine ya maisha yake na analiambia Mwanaspoti kupitia ‘Dakika 5 Na..., anayoyafanya sio kwa nia mbaya ikiwamo kuwachana wasanii wenzake.

KAZI ya ‘kimbelembele’ ngumu jamani. Hayo ni maneno ya msanii wa Bongo Movie na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Mengele ‘Steve Nyerere’, kutokana kuwepo kwake kwenye mambo mengi na kuyazungumzia.

Hata hivyo, anafichua kuhusu hilo na mengine ya maisha yake na analiambia Mwanaspoti kupitia ‘Dakika 5 Na..., anayoyafanya sio kwa nia mbaya ikiwamo kuwachana wasanii wenzake.

Anasema kwenye harakati zake za maisha yake za miaka mingi ametengeneza jina ‘Steve Nyerere’ ana leo imekuwa rahisi kwake kufika sehemu yoyote ambayo baadhi ya watu hawawezi kufika na kuzungumza na watu ambao siyo kila msanii anaweza kuwafikia.


Kujitolea kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoibuka, hii imekaaje?

“Kazi ya kimbelembele ni ngumu sana, lazima usome nyakati, ujue unakubalika vipi kwa unayemfanyia kimbele mbele na siyo unakurupuka tu, hivyo ukiona nimeongelea jambo jua wazi huyo mtu tunafahamiana.”


Vipi kuhusu kuwachana wasanii walioenda Dodoma?

Baada ya wasanii kwenda kwa wingi kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuibua maswali miongoni mwa watu, Steve aliibuka na kulizungumzia ikiwamo kuwachana wasanii waliokwenda huko.

“Kiukweli mimi sitaki kuwa mnafiki kwa wasanii wenzangu na bora nichukiwe lakini niseme ukweli roho yangu iwe na amani. Nachukizwa na kitendo cha wasanii kuacha kuzungumzia miradi ya Rais Samia Suluhu Hassan ila wakisikia kuna kampeni au tukio la chama basi watajitokeza kwa wingi, kampeni zikiisha watu wanarudi kulekule, wakati kabla ya uchaguzi kuanza ulikuwa ukimwambia msanii tushirikiane kuposti kitu cha Rais amefungua mradi au amefanya kitu hiki hawaposti mtu anakwambia siwezi kuposti bila hela na wengine wanakutukana kabisa kwenye mitandao na kuambiwa unajipendekeza unataka uteuzi. Mie niwashauri tu, bado hatujaenda kwenye kampeni, tujaribu hata siku moja tuposti miradi maana hakuna Taifa lingine zaidi ya Tanzania,” anasema Steve.


Inasemekana unawagawa wasanii makundi, ni kweli?

“Naanzaje kuwagawa wasanii wakati mimi nina Taasisi ya Mama Ongea na mwanao inazunguka kila mkoa?  Hii taasisi ipo huru kwa kila msanii kujiunga, kwanza nawagawa nawapeleka wapi? Mimi wasanii wote niko nao pamoja labda wajibague wenyewe tu, na fursa zikitokea lazima niwaangalie waliopo kwenye taasisi kwanza ambao nashikana nao kwenye harakati zote ninazokuwepo.”


Ukikutana na Rais kitu cha kwanza utamwambia nini kuhusu sanaa?

“Nitamwomba Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan azidishe kipaumbele kwenye elimu kwa wasanii, maana  kuna watu wanahitajika kupewa elimu kama madairekta, watu wa kamera, maprojuza na wahariri wa filamu wa sanaa ili sanaa yetu ifike mbali zaidi ndani na nje ya nchi.”


Vipi ishu ya kuteuliwa kiongozi?

“Mimi sipo kwa ajili  ya uteuzi, lazima Mheshimiwa Rais ateue watendaji kwa ajili ya masilahi ya Watanzania, asimchague steve sababu anapambana naye kwenye utendaji wake kwa Watanzania”


Kampeni za uchaguzi zinakuja, unawaambia wanasiasa?

“Mimi nawaomba wanasiasa kufanya siasa safi bila kutumia matusi pindi wanapokuwa kwenye majukwaa mbalimbali pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, wananchi wanataka kusikia hoja sio lugha chafu.”


Una ushauri gani kwa wasanii?

“Ushauri wangu kwa wasanii, kuna mahali wasanii tunachemka hasa hili la kutokuwa na mahusiano mazuri na wanahabari huku tukitambua ili kazi yako ifike haraka kwa jamii ni lazima ushirikiane na vyombo vya habari lakini hapa kwetu kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakiwakwepa waandishi wa habari hata katika mambo ya kawaida katika jamii.”

“Katika ulimwengu wa leo hakuna sababu ya msanii kumkwepa mwandishi wa habari kwani wote ni watoto wa baba mmoja tatizo vyumba tofauti, hivyo nawashauri wawape ushirikiano, mimi kwanza  niwapongeze wanahabari licha ya kupitia mambo magumu lakini wamekuwa karibu na kwa kila aina ya tukio ukweli natambua thamanj yao sana na mambo yangu mengi yanaenda kupitia wanahabari.”


Ni kitu gani sasa hivi unajivuni?

“Kuna vitu vingi sana, ila kikubwa ni hii Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, imekuwa msaada mkubwa sana kwa jamii na hadi kufikia hapa jua tumepambana sana, maana wakati imeanzishwa ilikuwa kwa lengo la kuhakikisha  Mama Samia na mgombea wa kiti cha urais wakati huo hayati John pombe Magufuli wanapata kura za kutosha, baada ta uchaguzi kupita tukasema hii taasisi tutaielekeza kwenye siasa, mambo ya jamii na sanaa kwa jumla na nikuambie tu hii ni taasisi bora iliyofanya vizuri kwa kipindi hiko, sasa ikatokea changamoto watu wengine kuchomolewa au kujitoa lakini bado ipo na itaendelea kuwepo hadi sasa inadunda.”