Queen Makune ashinda Miss Universe Tanzania 2026
Muktasari:
- Shindano hilo lililokuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na washiriki kupambana kwa nguvu kubwa kutafuta mshindi lilimalizika kwa Makune kuibuka mshindi wa jumla.
QUEEN Makune ameibuka mshindi wa shindano la urembo la Miss Universe 2026, lililofanyika usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Septemba 21, 2026, jijini Dar es Salaam.
Shindano hilo lililokuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na washiriki kupambana kwa nguvu kubwa kutafuta mshindi lilimalizika kwa Makune kuibuka mshindi wa jumla.
Kwa ushindi huo, Makune amenyakua taji la Miss Universe 2026 pamoja na zawadi ya Sh 20 milioni, huku akipata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Universe ya Dunia.
Katika fainali hizo, zilizoandaliwa na Kampuni ya Millen Prive & Co.Lifestlye, Sandra Giovina alishika nafasi ya pili na kujishindia zawadi ya Sh 10 milioni, huku washindi wa tatu hadi watano wakipata zawadi mbalimbali.
Ushindi wa Makune unaifanya Tanzania kuwa na mwakilishi katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, ambako ataiwakilisha nchi katika hatua inayofuata.