Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tamu, chungu za tuzo Grammy 2027

GRAMMY Pict

Muktasari:

  • Tuzo za 69 za Grammy, zinatarajiwa kufanyika Februari 7, 2027 katika ukumbi wa Crypto.com Arena huko Los Angeles, Marekani na kurushwa live na kituo cha ABC, pamoja na mitandao ya Disney+ na Hulu.

TAYARI waandaaji wa Grammy wametangaza majina ya watakaowania tuzo hizo kwa mwaka 2027 na kwa mara nyingine tena wasanii wa Bongo Fleva wamekosa nafasi huku wenzao wa Nigeria wakiendelea kutamba kama kawaida yao!.

Tuzo za 69 za Grammy, zinatarajiwa kufanyika Februari 7, 2027 katika ukumbi wa Crypto.com Arena huko Los Angeles, Marekani na kurushwa live na kituo cha ABC, pamoja na mitandao ya Disney+ na Hulu.

Katika kipengele cha Best African Music Performance ambacho ni maalum kwa wasanii wa Afrika, wanamuziki waliopata nafasi ni Asake (Nigeria) - Gratitude, na Tems (Nigeria) - Big Daddy.

Wengine ni Angelique Kidjo (Benin) na Ayra Starr (Nigeria) - Aye Kan (Are You Coming Back?), King Ayisoba & Rocky Dawuni (Ghana) - No Tradition, No Africa, na Wizkid & Asake (Nigeria) - Jogodo.

Hata hivyo, baada ya kutangazwa kwa majina yatakayowania Grammy 2027, kuna sehemu wasanii na mashabiki wao wamefurahi, na kuna upande umebaki na mshangao kama ifuatavyo.


GRAM 01

1. TEMS - VIPENGELE VINNE

Mwimbaji kutokea Nigeria, Tems amechaguliwa kuwania vipengele vinne katika Grammy 2027, akiwa ni mwanamuziki wa kwanza wa kike barani Afrika kufanya hivyo.

Tems ametajwa vipengele vya Best African Music Performance (Big Daddy), Best Solo RnB Performance (What You Need), Best RnB Song (What You Need), Best Global Music Album (Love Is a Kingdom).

Utakumbuka Tems ameshashinda Grammy mara mbili akifanya hivyo mwaka 2025 kupitia wimbo wake, Love Me Jeje (2024), na awali alishinda kupitia kolabo yake na Future na Drake, Wait For U (2022).


GRAM 02

2. BEYONCE - TEUZI 100

Mwimbaji wa Marekani, Beyonce ameingia katika historia baada ya kufikisha jumla ya uteuzi 100 za tuzo za Grammy, na kuwa msanii wa kwanza kuwahi kufikia idadi hiyo tangu tuzo hizo kuanzishwa mwaka 1959.

Katika Grammy 2027, Beyonce anawania kipengele kimoja cha Best RnB Solo Performance kupitia wimbo wake, Morning Dew (Donk) (2026), hatua inayomfanya kuwa msanii aliyechaguliwa kuwania tuzo mara nyingi zaidi.

Mume wa Beyonce, Jay Z ndiye anafuatia akiwa ameshapata teuzi 89 hadi sasa, huku Beyonce akiendelea kushikilia rekodi ya kushinda tuzo nyingi za Grammy kwa muda wote ambapo ameshinda tuzo 35.


GRAM 03

3. BURNA BOY - MIAKA 8 MFULULIZO

Mwanamuziki kutokea Nigeria, Burna Boy naye amechaguliwa kuwania Grammy 2027, kwa matokeo hayo anaweka rekodi ya kuwania tuzo hizo kwa miaka minane mfululizo.

Kolabo yake na Shakira, Dai Dai (2026) ambayo ilitoka kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2026, imetajwa kuwania kipengele cha Best Global Music Performance.

Burna Boy alichaguliwa kuwania Grammy kwa mara ya kwanza mwaka 2020 kupitia albamu yake, African Giant (2019), na tangu wakati huo hakuna mwaka ambao hajachaguliwa, huku akishinda mara moja.



GRAM 04

4. TYLA - AWAMU HII CHALI

Imekuwa ni mshangao mkubwa baada ya msanii wa Afrika Kusini, Tyla kukosa uteuzi wowote katika Grammy 2027 licha ya kuwa miongoni mwa wasanii walioandika historia katika kipengele cha Best African Music Performance.

Tyla amekuwa akifanya vizuri katika kipengele hicho tangu kilipoanzishwa, msanii huyo alifanikiwa kushindi mwaka 2024 na 2026, na kuweka rekodi kama msanii akiyeshinda kipengele hicho mara nyingi.

Mashabiki wengi walitegemea kumuona Tyla tena katika tuzo hizo hasa baada ya kufanya vizuri na wimbo wake, Chanel (2025) lakini kwa bahati mbaya awamu hii ameangukia pua. Hivyo endapo Tems atashinda, basi watakuwa wamefungana katika kipengele hicho.


GRAM 05

5. DIAMOND - AJARIBU TENA

Mwanamuziki wa Bongofleva, Diamond Platnumz ameshiriki katika albamu ya Angelique Kidjo, Hope (2026) ambayo inawania Grammy 2027 katika kipengele cha Global Music Album.

Lakini hiyo haina maana kuwa naye Diamond anawania Grammy au albamu hiyo ikishinda naye atapokea tuzo, hilo hapana. Hilo lingetokea tu endapo Diamond angekuwa ameshiriki kwa asilimia zaidi ya 50 katika albamu hiyo.

Hata hivyo, Diamond ameshiriki katika wimbo mmoja tu (Kakua) katika albamu hiyo, hivyo endapo albamu hiyo ya Angelique itashinda, Diamond atapokea tu cheti kutoka kwa waandaaji wa Grammy, Recording Academy kwa kutambua mchango wake.