Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PUMZI YA MOTO: Khaligraph amewashika pabaya wabongo

AGOSTI ni mwezi wa Hip Hop. Ndiyo ambao aina hii ya utamaduni ilizaliwa miaka 50 iliyopita.

Ilikuwa Agosti 11, 1973, kwenye ukumbi mmoja uliokuwa kwenye jengo fulani katika mtaa wa 1520 Sedgwick Bronx, New York, Marekani pale kijana wa miaka 18 mwenye asili ya Jamaica, Clive Campbell maarufu kama DJ Kool Herc alipokuwa akiwarusha watu kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa aliyomuandalia dada yake.

Wakati akifanya makamuzi, DJ Kool Herc alibuni kitu tofauti na vilivyozoeleka. Badala ya kupiga wimbo kamili alipiga ala (instrumental) pekee huku rafiki yake, Coke La Rock akishika kipaza sauti na kuchombeza kwa maneno ya hapa na pale, hivyo ndivyo Hip Hop kama muziki ilivyozaliwa.

Miaka 50 sasa, Hip Hop imekuwa aina ya utamaduni unaounganisha dunia, siyo tu The Bronx au Marekani. Tanzania kama sehemu nyingine ya dunia ilikumbwa na kishindo cha Hip Hop tangu miaka ya 1980 na imesimama hadi sasa.

Wana Hip Hop wa Tanzania walipata umaarufu kwa ubunifu wa kucheza na maneno hadi nje ya Tanzania. Afrika Mashariki ikatekwa na Hip Hop ya Bongo na kuhamasisha vijana kadhaa akiwemo Brian Omollo kutoka Kenya.

Nyota huyo ambaye jina lake la sanaa ni Kalig raph Jones, amekiri mwe nyewe kupitia ‘Diss Track’ yake ya Bongo Favour ambamo ndani yake amewavua nguo wana Hip Hop wa Tanzania.


ILIVYOANZA

Kama kuna mahala Kaligraph amewashtukiza wana Hip Hop wa Bongo, basi kwenye hili. Alianza kama mtu anayetafuta ugomvi alipoonekana akijisifu kwa kukua Kiingereza na kuvaa vizuri ‘drip’, tofauti na Watanzania ambao wanajua Kiswahili tu. Haraka haraka wasanii wa Tanzania wakaibuka na mistari ya Kiingereza kumuonyesha hakuwa sahihi. Lakini kumbejalianzia tu. Punde si punde akatoa wimbo wa Bongo Favour ambamo ndani yake amerusha mawe mazito yasiyo na majibu hata kidogo. Amewananga wana Hip Hop wa Bongo kwa mistari mikali yenye maneno ya kistaarabu, lakini yanayovua nguo mtu. “Kusema ukweli Bongo Rap imenilea, but mnalegea.

“Na ndo kwa maana nawadea (dare), na sijakosea...but some of you people need a prayer.

“Bongo Rap ain’t be the same ever since mumpoteze Ngwair.” Huu ni ubeti wa pili kwenye wimbo huo wenye mashairi yaliyoshiba kweli kweli. Kaligraph anakiri kwamba amekuzwa kisanaa na rap ya Bongo ambayo kwa sasa anaona inayumba. Anaposema nawadea (dare) yaani anathubutu kuwatingisha akiwa na lengo la kuwaamsha kutoka usingizi mzito huku wengine wakihitaji maombi kutokana na anguko.

Anamalizia kwenye ubeti huu kwa kusema kwamba rap ya Bongo imebadilika sana (zaidi ya Zuwena wa Diamond tangu kufariki duni kwa Albert Mangwea. Kaligraph ameonyesha kwamba alijipanga kwelikweli kabla ya kuchokoza vita hii na kupitia mashairi yake amempiga kila mmoja kwa pigo analostahili, kama inavyoonekana kwenye ubeti wa tatu.

“And heavyweights hamtoi ngoma kama kitambo. “Oh some of you said that Roma alinihumble. “Na sitabishana coz padre alinifungulia mlango. “Then he disappeared siku hizi hatujui zake mpango.” Amerusha jiwe zito kwa wasanii wakubwa wa Hip Hop akisema ama wako kimya sana au wanatoa nyimbo mpya, lakini hazifikii ubora wa zile za zamani. Anasema baadhi  walisema Roma (Mkatoliki) alimbeba, jambo ambalo anakiri kwamba kweli Roma (ambaye amemuita padre) alimsaidia katika kutoka, lakini baada ya hapo akapotea, hajulikani anafanya nini sasa.

Baada ya kugusa wakongwe, akawarudia vijana wa sasa akianza na Msodoki. “Young Killer ameingiza missing ever since afungend ndoa. Kuna time niliamini Bongo Hip Hop angeikoa. Sina ubaya brother na sikatai inafanya poa, ila mimi si shabiki wa hizo ngoma mpya unatoa.”

Kaligraph ambaye pia anajiita OG, amemshukia Young Killer ambaye alikuwa na mwanzo mzuri tangu ajulikane kupitia Super Nyota ya Fiesta, kwamba siyo yeye tena kwa sasa. Maisha ya ndoa ni kama yamebadilisha kitu fulani kwake, kitu ambacho kiliwaaminisha wengi dogo angekalia kiti ambacho kina Profesa Jay, Sugu, AY, Juma Nature na wengine wengi wamekiacha. Lakini kazi anazofanya sasa zinawaangusha wengi akiwemo Kaligraph Jones. “Taking over TZ ain’t nothing easier. “Wakazi anafaa apewe kazi Wasafi Media. “Brother ni blogger, kubonga tu kwa mtandao. “Marekani hawakutaki na TZ wamekudharau.” Katika beti zote zenye shombo, ubeti huu na ubeti wa kwanza kabisa zinaongoza. Maana hapa kapiga bongo kwa ujumla na mmojammoja. Anasema hakuna kitu rahisi kama kuikabili Tanzania.

Halafu anamshukia Wakazi, mmoja wa wana Hip Hop wa Tanzania ambao wana posti nyingi za mitandaoni kuliko mashairi ya nyimbo zao. Anasema jamaa anafaa kuajiriwa Wasafi Media kwa sababu amekuwa mwandishi kuliko msanii.

Anaenda mbali kwa kusema hatakiwi Marekani hadi Tanzania. Hii ni kwa sababu Wakazi mara zote amekuwa akijisifia kuishi Marekani. Ukiacha Wakazi, mwathirika mwingine wa OG ni mwanadada maarufu wa Hip Hop, Rosa Ree.

Kwenye sakata hili rapa huyo aliingia mazima akimjibu Omollo kwa kujiita mama Omollo. Sasa hapa kuna ujumbe wake.

“Rosa Ree you are my girl but usidhani mi nitakusare. “Talent unayo but ndo usikike mtafute Babu Tale. “Coz you ain’t have a hit since utokwe na Navy Kenzo. “Kakupa verse bure na ni sababu we ni mrembo. “But as far as rap goes, hauwezi kuwa solo writer. “Unaweza saidiwa kuandika na my nigga chllo brighter.” Kaligraph anamshukia Rosa Ree kwamba ni mshikaji lakini hatamuacha salama. Anasema dada huyo kipaji anacho lakini hawezi kutoka hadi asaidiwe na watu. Anaenda mbali zaidi na kukumbushia ngoma zilizomtambulisha  ambazo alifanya na Navy Nenzo, Bless up na Mchanga mchaga. Kwamba baada ya hapo hakuna tena ngoma za maana alizotoa. Akaenda mbali na kusema alitamba wakati huo kwa sababu alipewa bure mistari kutokana na urembo wake. Ukifungua zaidi ‘code’ hii, utaona hapa kuna jiwe la rushwa ya ngono. Kwa kweli Kaligraph kwenye hii ngoma amewakaanga sana wasanii wa hip hop wa bongo. Inavyoonekana alifanya utafiti wa kutosha na kukusanya taarifa sahihi. Mfano ni pale anapompiga na kitu kizito kichwani Bill Nas.

“Nimewafanyia favour kuwapatia platform. “Coz Bill Nas of late has been doing the worse songs.” Wimbo huu ameuita Bongo Favour badala ya Bongo Flava. Sababu ya kuuita Bongo Favour ndiyo inapatikana hapa. Anasema amewafanyia favour (upendeleo au msaada kwenye tuta) wasanii wa Tanzania kwa kuwapa jukwaa la kusikika. Yaani kwake yeye, huu ni msaada kwa wana hip hop wa Bongo ambao walipotea kabisa. Kwa mfano ni Bill Nas ambaye anasema anafanya ngoma za hovyo. Bila shaka utakumbuka kwamba Bill Nas ana ngoma ya Amapiano ya Chetu.

Kaligraph anaonekana anakerwa sana na wana Hip Hop kuimba Amapiano, na ndiyo maana anamkanya Young Lunya. “Lunya my brother usikubaki Piano juu inatrend.” Kaligraph anafikia wakati anatamani zama zirudi nyuma hadi nyakati zile kama Ngwea alipoachia ngoma yake ya Mikasi. Akikumbuka zama hizo anaishia kuwatakia mapumziko mema wakali kama Langa na Godzilla. Hii ina maana hawa waliopo amewavua vyeo.