Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PRIYANKA CHOPRA: Bollywood hadi Hollywood kusaka mkwanja, umaarufu

Muktasari:

  • Priyanka, ambaye pia ni mjasiriamali, balozi wa bidhaa mbalimbali na mwanzilishi wa miradi ya kijamii, amejijengea utajiri mkubwa unaokadiriwa kufikia takribani Dola 70 milioni, jambo linalomfanya kuwa mmoja wa mastaa wa kike wenye kipato kikubwa zaidi.

MUMBAI, INDIA: JINA la Priyanka Chopra limeendelea kuvutia vichwa vya habari kutokana na mafanikio yake makubwa katika filamu, muziki, televisheni na biashara.

Priyanka, ambaye pia ni mjasiriamali, balozi wa bidhaa mbalimbali na mwanzilishi wa miradi ya kijamii, amejijengea utajiri mkubwa unaokadiriwa kufikia takribani Dola 70 milioni, jambo linalomfanya kuwa mmoja wa mastaa wa kike wenye kipato kikubwa zaidi.

Hapa tumekusogezea mchanganuo wa utajiri wake na njia anazopiga pesa, kutoka kwenye filamu hadi biashara na matangazo ya kimataifa.


ANAPIGAJE PESA

Sehemu kubwa ya mapato ya Priyanka yanatokana na filamu na vipindi vya televisheni. Kila filamu inayoigiza inaweza kumpa takribani Dola 5–10 milioni huku miradi mikubwa ya Hollywood alikohamia kutoka Bollyhood, ikimpa mapato ya juu zaidi, ikiwamo filamu aliyoitoa mwaka huu iitwayo The Bluff.

Pia kipindi chake cha televisheni cha Quantico kilimpa umaarufu mkubwa duniani na mapato yenye thamani ya mamilioni ya dola.

Mbali na kazi ya filamu na televisheni, Priyanka anaingiza pesa kupitia, kampuni yake ya uzalishaji wa filamu, Purple Pebble Pictures, inayozalisha filamu ndogondogo, pia na kazi nyingine za kidigitali.

Ushirikiano na matangazo ya bidhaa za kimataifa kama Nivea, Jaipur Jewelry, na ushirikiano wake na mashirika kama vile UNICEF na mikataba ya mwaka inaweza kumpa mapato ya zaidi ya Dola 5–10 milioni.

Mwaka 2024, jarida la Forbes India liliitaja kama mmoja wa mastaa wenye kipato kikubwa kutoka India.


MIJENGO NA MAISHA YA KIFAHARI

Priyanka anamiliki nyuma Mumbai, yenye thamani ya takribani Dola 5 milioni, ikijumuisha bustani kubwa, bwawa la kuogelea, studio ya muziki na maeneo mengine ya burudani.

Pia anamjengo mwingine ambao upo Los Angeles, Marekani ambako mara nyingi huutumia wakati wa kazi zake za Hollywood, unatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya Dola 6 milioni.

Mbali na hizo ambazo zinafahamika anatajwa kuwa na mijengo sehemu nyingine kwa siri ambayo amekuwa akiitumia kujichimbia akihitaji utulivu.

NDINGA ZAKE

Range Rover Vogue – Dola 120,000

Mercedes-Benz G-Class – Dola 150,000

BMW X7 – Dola 90,000

Audi Q7 – Dola 80,000

Tesla Model X – Dola 120,000


MSAADA KWA JAMII

Priyanka ambaye aliwahi kuwa mrembo wa dunia 2000, ni balozi wa kimataifa wa UNICEF na amekuwa mstari wa mbele kusaidia watoto, afya, elimu na miradi ya kijamii.

Tukio maarufu ni wimbo wake wa In My City na kampeni za kijamii ambazo ziliwahusisha mashirika mbalimbali kutoa misaada kwa jamii zenye uhitaji, hasa kwenye elimu na afya ya watoto.

Pia amefadhili miradi ya kusaidia wanawake wanaopambana katika biashara na kutoa elimu ya maisha kwa jamii mbalimbali nchini India na Marekani.

FAMILIA NA MAISHA BINAFSI

Priyanka alizaliwa Mumbai, India lakini amekuwa akiishi sana Marekani katokana na kazi yake ya sanaa.

Amekuwa katika ndoa na Nick Jonas na mara nyingi huonekana pamoja kwenye hafla mbalimbali.

Priyanka ni mfano wa staa wa kike ambaye anapambana katika nyanja tofauti huku akiwa na moyo wa kurudisha kwa jamii.


HATUA MUHIMU

2000 – Miss World

2003 – Filamu ya kwanza Bollywood

2015 – Quantico (TV ya Marekani)

2017 – Kuanzisha Purple Pebble Pictures