Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bagamoyo Festival 2026 imetiki

BAGAMOYO Pict

Muktasari:

  • Tamasha hilo kubwa kuliko yote Tanzania Bara, msimu huu linarudi likiwa na msisimko wa kipekee na kaulimbiu ya “Sanaa na Utamaduni kwa Tabianchi”, huku likikutanisha mchanganyiko wa ngoma za asili, muziki wa moja kwa moja ‘live’, maigizo, sarakasi, vichekesho na maonyesho ya sanaa za mikono.

Viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), leo Oktoba 28 hadi 31, vinatarajiwa kufurika wapenzi wa burudani na sanaa, wakati Tamasha la 44 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo linapoanza rasmi.

Tamasha hilo kubwa kuliko yote Tanzania Bara, msimu huu linarudi likiwa na msisimko wa kipekee na kaulimbiu ya “Sanaa na Utamaduni kwa Tabianchi”, huku likikutanisha mchanganyiko wa ngoma za asili, muziki wa moja kwa moja ‘live’, maigizo, sarakasi, vichekesho na maonyesho ya sanaa za mikono.

Akizungumzia maandalizi ya tukio hilo, Kaimu Mkuu wa Chuo cha TaSUBa, Bw. Gabriel Kiiza ameweka wazi hadi sasa zaidi ya vikundi 82 vimeshakamilisha taratibu za kushiriki, ikiwemo safu ya wasanii nguli wa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

“Tamasha la mwaka huu linakwenda kuwa la aina yake. Mpaka sasa tuna vikundi 82 vilivyothibitisha kushiriki. Upande wa wasanii maarufu wa nyumbani tunae Vitalis Maembe, Ras Gwandumi na Sinaubi Zawose. Pia tuna washindi wa kitaifa wa ngoma kama Buyegu Theater Group na Mundu Arts Group, huku tukipokea burudani kutoka nje ikiwemo Jeremie Tshibi kutoka Kongo na Napsa Lusaka Theater Cooperative kutoka Zambia,” anasema Gabriel Kiiza.


NCHI NYINGINE

Ushiriki wa mataifa ya nje kwenye Tamasha la Bagamoyo si wa kutumbuiza jukwaani pekee, bali unahusisha mambo mbalimbali ya kitamaduni na kielimu.

Makongamano na warsha, wasanii na wadau wa sanaa kutoka nje ya nchi huendesha na kushiriki mafunzo ya pamoja na wasanii wa Kitanzania na wanabadilishana mbinu za kisasa za utunzi, upigaji wa vyombo, na uongozi wa kazi za sanaa.

Ubadilishanaji wa Utamaduni; nchi hizo huonyesha sanaa zao za asili, mavazi, ngoma na muziki wa kipekee kutoka mataifa yao, jambo linalofanya Bagamoyo kuwa kitovu cha mwingiliano wa kitamaduni duniani.

Sanaa na bidhaa; vikundi vya kimataifa hupata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa za sanaa za mikono na utamaduni kutoka katika nchi zao, huku vikijenga diplomasia imara ya kitamaduni na Tanzania.


BAGA 02

WASANII, VIKUNDI

Buyegu Theater Group: Washindi wa kwanza wa ngoma kwenye Tamasha la Taifa la Utamaduni 2026 (Tanzania)

Mundu Arts Group: Washindi wa pili wa ngoma kwenye Tamasha la Taifa la Utamaduni 2026 (Tanzania).

Wakali wa Nyumbani: Vitalis Maembe, Ras Gwandumi, na Sinaubi Zawose.

Burudani ya Kimataifa: Jeremie Tshibi (Kongo/DRC) pamoja na Napsa Lusaka Theater Cooperative (Zambia).


BAGA 03

NI TAMASHA LA NAMNA GANI?

Tamasha la Bagamoyo ni kitovu cha mwingiliano wa kitamaduni. Huwa ni jukwaa huru linalokutanisha sanaa za asili na za kisasa katika eneo moja.

Kuanzia asubuhi hadi usiku mnene, mashabiki hupata fursa ya kushuhudia michezo ya watoto, mashairi, mazingaombwe, makongamano, warsha za sanaa, vyakula vya asili na vinywaji vya kinyumbani, huku jukwaa kuu likitawaliwa na burudani za live kutoka kwa vikundi vya ndani na nje ya nchi.


WAKAZI WA BAGAMOYO NA MAENEO YA KARIBU WANAFAIDIKAJE?

Ukiachana na burudani ya kukata ardhini, tamasha hili ni mkombozi mkubwa wa kiuchumi na kijamii kwa mji wa kihistoria wa Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla.

Mzunguko wa Fedha na Biashara, Wajasiriamali wadogo na wakubwa, wakiwemo wauza vyakula vya asili, vinywaji, bidhaa za sanaa za mikono na nguo za kitamaduni, hupata soko kubwa la papo kwa papo.

Sekta ya Ukarimu na Usafiri, Hoteli, nyumba za wageni (guest houses), waendesha bodaboda na bajaji hupata msimu wa neema kutokana na wimbi kubwa la wageni wa ndani na wa kimataifa.

Fursa na Mtandao kwa Vijana, Wanachuo na wasanii chipukizi wa maeneo ya jirani hupata nafasi ya kujifunza, kuonyesha vipaji vyao na kujenga mahusiano ya kazi na wasanii nguli duniani.


BAGA 01

HISTORIA FUPI YA TAMASHA LA BAGAMOYO

Safari ya tamasha hili ilianza rasmi mwaka 1981 katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo (sasa TaSUBa).

Lengo lake kuu la mwanzo lilikuwa ni kutoa nafasi kwa wanafunzi wa chuo hicho kuonyesha kwa vitendo ujuzi na vipaji walivyovipata darasani mbele ya jamii inayowazunguka na kupata nafasi ya kujiliwaza.

Kutokana na ukubwa wa sanaa na mwitikio wa jamii, tamasha hilo lilianza kuvutia wadau na wasanii kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, na baadaye kuanza kupokea vikundi kutoka nje ya nchi.

Leo hii, limetoka kuwa tamasha la wanafunzi pekee na kuwa moja ya matamasha makubwa na ya kuheshimika zaidi barani Afrika, likiwa kiungo muhimu cha kukuza diplomasia ya kitamaduni, kujenga taswira chanya ya nchi, na kutangaza utalii wa Tanzania.