Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Piga che che kule mwanao akushangaze

Muktasari:

  • Ingawa ni ngumu kuzuia kuyafahamu mambo yaliyo nje ya umri wao, kutokana na utandawazi uliopo, lakini unaweza kuwajenga kisaikolojia kuendana na vitu vya ngazi yao.

NI wikiendi fulani hivi upo na watoto wako au wadogo zako, unataka kujua maendeleo yao ya shule ama vitu gani wanavipenda kuvisikia, ili kuwajengea furaha na kuifanya siku yao iwe nzuri, Mwanaspoti linakupa mbinu ya kipi ukifanye.

Ingawa ni ngumu kuzuia kuyafahamu mambo yaliyo nje ya umri wao, kutokana na utandawazi uliopo, lakini unaweza kuwajenga kisaikolojia kuendana na vitu vya ngazi yao.

Miongoni mwa nyimbo unazozipenda kuzisikiliza kwa umri wako, basi usisahau kuweka na wanazopenda watoto wako, kama ulikuwa hujui kwa sasa habari ya mjini, ukipiga tu wimbo wa Che Che Kule, utaona tabasamu la mwanao.

Wimbo huo umeimbwa kwa lugha za tamaduni za taifa la Ghana, unatumika zaidi shuleni na ni kati ya zile zinazopendwa.

Kwa sasa wimbo huo umesambaa kwa Afrika, unapendwa zaidi na watoto ingawa wapo watu wazima ambao wanaufanyia chelenji katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Taarifa kutoka Apple Music zinaeleza wimbo huo umetungwa na Osibisa pia ni mwigizaji, mzalishaji na mtayarishaji, wakati Sol Amarfio alishiriki kwenye kuuandika bila kumsahau John Punter ambaye alikuwa sehemu ya utayarishaji (producer)  miaka mingi iliyopita ingawa unaendelea kufanyiwa maboresho.

Maneno yaliyopo katika wimbo huo ni Che Che Kule, Che Che Kofisa, Kofisa Langa

(touch your head, touch your shoulders, hands on your hips, touch your knees all the way down).

Kwa lugha ya Kiswahili wimbo huo unamaanisha gusa kichwa mara nne, kwa kufuata mdundo, gusa mabega mara nne, huku ukizungusha sehemu ya juu ya mwili kutoka upande mmoja kwenda mwingine, weka mikono kiunoni huku ukizungusha sehemu ya juu ya mwili kutoka upande mmoja kwenda mwingine mara nne kwa kufuata mdundo, gusa magoti mara nne, kisha gusa kiuno kwenye neno “adende”, kama mwendo wa msumeno wa kunyanyua na kushusha.

Kwa hapa nchini, unatumika zaidi kwa shule za chekechea na wakirudi mtaani wanakuwa wanaimba bila kukosea maneno na una aina yake ya uchezaji.

Ukiacha Tanzania pia kwa Uganda unatumika zaidi kuanzia shule za chekechea hadi shule za msingi, jambo ambalo unazidi kuupa umaarufu, huku wengine wakiweka ufundi wa AI.

Aina ya video mbalimbali zinazotengenezea wimbo huo, zinaonyesha mazingira ya Kiafrika zaidi, ingawa hata wazungu wanaifanyia chelenji.


KAULI ZA WASANII

Msanii mkongwe wa Bonge Fleva, Juma Nature anasema: “Kuna sababu kubwa ya wasanii kuimba nyimbo ambazo zinaacha funzo, inanishangaza kuona kwa sasa unakuta nyimbo ambayo haina maadili na watoto inapigwa mchana, tofauti na zamani zilikuwa zinapigwa usiku na maeneo sahihi, sasa inapotokea kuna nyimbo za watoto ambazo zinawajenga ni jambo zuri.”

Msanii mwingine wa Bongo Fleva, Nedy Music anasema: “Kama sisi ni kioo cha jamii, lazima tujue kuwatunza watoto, ni jambo jema kufanya kitu kinachoendana na wao ili kufurahia kwa umri wao.”