Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Quick Rocka kutoka MJ Records hadi Jua Kali

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Quick Rocka maarufu kama Frank, alifanya kazi na MJ Records kabla ya kufungua lebo na studio yake ya Switch Music Group (SMG), na kisha baadaye kuibukia katika uigizaji. Fahamu zaidi.

RAPA Quick Rocka ameendelea kuwa maarufu katika tasnia ya uigizaji kiasi kwamba kuna baadhi ya mashabiki hawajui kama alishawahi kuwa mwanamuziki tena akifanya kazi na moja ya rekodi lebo kubwa nchini.

Quick Rocka maarufu kama Frank, alifanya kazi na MJ Records kabla ya kufungua lebo na studio yake ya Switch Music Group (SMG), na kisha baadaye kuibukia katika uigizaji. Fahamu zaidi.


1. Master J alimsikia Quick Rocka redioni Clouds FM akifanya freestyle na kuvutiwa na uwezo wake, akawasiliana na B Dozen na kumuomba kumkutanisha na rapa huyo ambaye alikuwa ndani ya kundi la Rockaz akiwa na wenzake watatu.


2. Kwa mara ya kwanza wawili hao wakakutana Sinza, Dar es Salaam, ambapo na Master J alimpa ofa Quick Rocka ya kumsaini MJ Records lakini akiwa peke yake na siyo pamoja na wenzake wa Rockaz.

3. Kutokana Master J alikuwa ameshastaafu utayarishaji muziki, kazi za Quick Rocka ndani ya MJ Records zikasimamiwa na Marco Chali ambaye ndiye aliachiwa studio hiyo kwa wakati huo.


4. Marco Chali ambaye alianza kuvuma akiwa Kama Kawa Records, ndiye alitengeneza ngoma iliyomtoa Quick Rocka chini ya MJ Records, Bullet (2009) akimshirikisha Q Jay ambaye alitolewa kimuziki na Master J.


5. Mdogo wake na Marco Chali, Bifu Chaa ambaye ni mtayarishaji muziki pia, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuisikia ngoma ya Bullet na akaipenda, hivyo akamshawishi Marco wairekodi. Ikumbukwe ngoma hiyo ilitoka kipindi ambacho Marco Chali alishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2008 kama Mtayarishaji Bora wa Mwaka.


6. Marco Chali aliendelea kutengeneza nyimbo za Quick Rocka, moja kati ya hizo ni ule uitwao My Life (2013) ambao pia alishirikishwa akiimba kiitikio chake, kazi ambayo pia ameifanya katika nyimbo za wasanii wengi. Utakumbuka Marco amesikika kwenye nyimbo kama 'Kamili Gado' wa Professor Jay, 'Party Zone' wa AY, 'King Zilla' & 'Nataka' zake Godzilla na kadhalika.

7. Hatua ya Quick Rocka kusainiwa MJ Records, tunaweza kusema ulikuwa ni mwanzo wa kusambaratika kwa kundi la Rockaz ambalo lilikuwa linakuja kwa kasi.


8. Mbali na Quick Rocka, wasanii wengine waliounda kundi hilo ambalo jina lake walipewa na marehemu Ngwea, ni Chief  Rocka, Dau Rocka na Mo Rocka. Hivyo wote majina yao ya mwishoni yanaishia na Rocka, ukiwa ndio utambulisho wao mkuu.


9. Baada ya kupata umaarufu kwenye muziki, Quick Rocka akaingia kwenye uigizaji baada ya kushawishiwa kufanya hivyo na mtayarishaji maarufu Bongo, Lamata ambaye walikutana kwa mara ya kwanza studio kwa Tuddy Thomas.


10. Tamthilia ya kwanza kwa Lamata na Quick Rocka kufanya pamoja ni Kapuni, kisha ikafuata ya Jua Kali ambayo hadi sasa anaendelea nayo akitumia jina la Frank, uhusika ambao ameuvaa kiasi kwamba kuna baadhi ya mashabiki hawajui kama alishawahi kufanya muziki.