Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota za Priscilla katika Ufalme wa Jux

PRISILLA Pict

Muktasari:

  • Priscilla, binti wa staa wa Nollywood, Iyabo Ojo, tangu ameingia rasmi katika maisha ya Jux, kwa namna fulani amebadili muziki wa msanii huyo hasa upande wa video za nyimbo zake. 

MSHAWISHI maarufu wa chapa kutokea nchini Nigeria, Priscilla Ojo anazidi kuikuza rekodi yake katika muziki wa staa wa Bongo Fleva, Jux ambaye pia ni mumewe wake wa ndoa.

Priscilla, binti wa staa wa Nollywood, Iyabo Ojo, tangu ameingia rasmi katika maisha ya Jux, kwa namna fulani amebadili muziki wa msanii huyo hasa upande wa video za nyimbo zake. 

Ni hivi karibuni tu Priscilla ameonekana tena katika video mpya ya wimbo wa Jux, Sexy & Bad (2026) ambao amemshirikisha Stonebwoy kutokea Ghana.

Video hiyo ambayo imefanyika jijini London, England, pia ndani yake wametoka mastaa wengine kutokea Nigeria akiwemo Davido, Mr. P wa kundi la P-Square, pamoja na Tiwa Savage.

PRI 01

Katika video hiyo, Priscilla ametokea akiigiza kama mpenzi wa Jux, kazi ambayo ameifanya mara nyingi zaidi kuliko mrembo yeyote tangu mwanamuziki huyo ameanza kujihusisha na sanaa.

Hiyo inakuwa video ya sita ya Jux kushuti na Prisiclla baada ya hapo awali kutoa Ololufe Mi (2024), Si Mimi (2025), God Design (2025), Thank You (2025) na See Body (2026).

Video ya kwanza (Ololufe Mi) kufanya pamoja, ndio inaongoza kutazamwa (views) katika mtandao wa YouTube kati ya hizo sita walizoshirikiana, ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 39.2 hadi sasa.

PRI 02

Utakumbuka wimbo huo ulimfanya Jux kushinda tuzo ya Jayli zilizofanyika jijini Abidjan nchini Ivory Coast, akitakata katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki 2025.

Wimbo huo ambao Jux amemshirikisha Diamond Platnumz, wawili hao wamecheza kama watoto wa Mfalme mwenye nguvu kubwa kiutawala na baba yao amewachagulia wanawake wa kuoa ila tayari kila mmoja ana chaguo lake.

Jux amempenda Priscilla kutokea Nigeria ambaye alijuana naye kupitia mitandaoni, huku Diamond akiangukia kwa mtumishi anayefanya kazi katika Ufalme wao kitu ambacho ni kinyume na matakwa ya baba yao.

Basi wanajadili ikiwa ni sawa kuacha urithi wa Ufalme ili kufuata kule walipopenda, Diamond anamshauri Jux kuusikiliza moyo wake ingawa yeye mwenyewe mwanzoni alipanga kuheshimu chaguo la mfalme.

PRI 03

Mwishowe wote wanafuata nyoyo zao na sio matakwa ya baba yao, kufikia hapo mfalme anakuwa hana jinsi zaidi ya kubariki uamuzi wa watoto wake na hivyo ndoa mbili zinafungwa ambapo Jux anamuoa Priscilla.

Hatua ya Jux kuwa na Priscilla kutoka Nigeria kilibeba maana nyingi kwa mashabiki, wapo waliodhani alifanya hivyo ili kumrusha roho aliyekuwa mpenzi wake, Vanessa Mdee ambaye amechumbiwa na Rotimi mwenye asili ya Nigeria. 

Vilevile wapo waliona kabisa kuna mradi mkubwa unakuja nje ya mapenzi yao, na ni kweli, hiyo ni baada ya Priscilla kuonekana katika video ya wimbo huo wa Jux, Ololufe Mi (2024) ambao umetayarishwa na S2kizzy kutokea studio za Pluto Republic.

Jambo hili lilitabirika kutokana na utamaduni wa Jux wa kuwatumia warembo anaokuwa nao katika video zake. Kipindi yupo na Vanessa alimtumia katika video ya wimbo wake, Sisikii (2015), huku wakitoa pamoja nyimbo mbili na video zake, Juu (2016) na Sumaku (2019).

PRI 04

Na baada ya kuachana na Vanessa, Jux alizama kwenye penzi jipya na Nayika kutokea Bangkok, Thailand ambaye alitokea kwenye video ya wimbo wake, Unaniweza (2020) ingawa muda mfupi baada ya video hiyo kutoka waliachana!.

Hata kipindi anahusishwa kuwa na uhusiano na Huddah Monroe wa Kenya, madai ambayo wote waliyakanusha, ndio wakati Huddah alionekana katika video ya wimbo wa Jux, Simuachi (2022).

Hivyo tangu Vanessa hadi sasa, Prisiclla anasalia kuwa mrembo aliyeonekana mara nyingi zaidi katika video za Jux, mwanachama wa zamani wa kundi la Wakacha.

Lakini hadi sasa Vanessa ndiye mrembo pekee aliyedumu na Jux kwa muda mrefu zaidi katika uhusiano. Wawili hao walikuwa pamoja tangu mwaka 2014 hadi 2019 walipoachana wakiwa amefanya mengi pamoja kama kuandaa tamasha lao, Inlove & Money Tour 2018. 

Ikumbukwe Jux na Priscilla waliweka wazi uhusiano wao mnamo Julai 2024 ikiwa ni miezi michache tangu mwanamuziki huyo kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Karen Bujulu ambaye walidumu kwa takribani mwaka mmoja.

Jux na Priscilla ambao walifunga ndoa mnamo Februari 2025, walitangaza wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza hapo Julai 24, 2025 kupitia Instagram, na kufikia mwishoni mwa Agosti, wakatangaza kuwa wamejaliwa mtoto wa kiume na kumpa jina la Rakeem.