Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jux atoa kauli ishu ya mtoto mitandaoni, DNA yatajwa

Muktasari:

  • Jux, ambaye kwa sasa ni mume wa Priscilla Ojo, binti wa mwigizaji mkongwe wa Nollywood, Iyabo Ojo, tayari ni baba wa mtoto mmoja, baada ya yeye na Priscilla kupata mtoto wa kwanza, Prince Rakeem Mkambala aliyezaliwa nchini Canada, Agosti 24, 2025.

SAKATA la msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux, na mwanamke anayetambulika kwa jina la Happy, limechukua sura mpya baada ya pande hizo mbili kutoa kauli zinazokinzana kuhusu madai ya mtoto mwenye umri wa miaka 11.

Jux, ambaye kwa sasa ni mume wa Priscilla Ojo, binti wa mwigizaji mkongwe wa Nollywood, Iyabo Ojo, tayari ni baba wa mtoto mmoja, baada ya yeye na Priscilla kupata mtoto wa kwanza, Prince Rakeem Mkambala aliyezaliwa nchini Canada, Agosti 24, 2025.

Happy ndiye aliyeibua sakata hilo siku chache zilizopita, akidai Jux ni baba mzazi wa mtoto huyo na kwamba ameshindwa kuwajibika.

Baada ya madai hayo kusambaa kwa kasi mitandaoni, Happy alionekana kwenye video akiomba msaada kutoka kwa waziri mwenye mwenye dhamana ya masuala ya jinsia, wanawake na watoto ili kusaidia kutatua jambo hilo.

Kubwa alilotaka Happy ni kipimo cha DNA, akisema anaamini Jux ndiye baba mzazi wa mtoto huyo na kwamba kipimo hicho ndicho kinachoweza kuweka wazi ukweli.

Hata hivyo, wakati Happy akiendelea kusisitiza DNA, upande wa Jux kupitia uongozi wake wa African Boy umepinga  madai hayo ukisema taarifa hizo hazina ukweli.

Uongozi huo umeeleza kuwa madai hayo yamebuniwa na kwamba Jux na Happy hawajawahi hata kukutana, huku ukiwaonya wanablog na, vyombo vya habari kusambaza taarifa ambazo hazina ukweli.


JUX ATOA KAULI

Jux mwenyewe ametoa tamko kuhusu sakata hilo, akieleza mwanzoni aliamua kukaa kimya na kulifuatilia kwa utulivu kwa sababu hakuliona kuwa na msingi wala kustahili kupewa nafasi.

Lakini amesema hali imefika mahali ambapo madai hayo yanaendelea kugusa jina lake, familia yake, biashara zake pamoja na taswira ambayo ameijenga kwa miaka mingi kupitia kazi, nidhamu na kujituma.

Jux amesema jambo kama hilo liliwahi kujitokeza hapo nyuma na wakati huo alichukua hatua ya kumtafuta mhusika mwenyewe ili kufahamu chanzo cha madai hayo.

Kwa mujibu wa Jux, katika mazungumzo yao, mhusika huyo alithibitisha kwa maneno na kwa sauti yake kuwa hakuwahi kukutana naye kimwili wala kuwa na mahusiano ya kimapenzi naye.

Pia, Jux alisema mhusika huyo alimwomba asilipe uzito suala hilo, akieleza kuwa madai hayo yalitokana na baadhi ya watu waliokuwa wakimfananisha mtoto huyo na Jux na baadaye kuanza kumhusisha msanii huyo kuwa baba yake.

"Kumekuwa na taarifa zinazosambaa zikidai kuwa mimi ni baba wa mtoto wa mtu fulani. Nimekuwa nikilifuatilia jambo hili kwa utulivu, bila kulipa uzito ambao halina wala halistahili," ilisema taarifa iliyochapishwa na Jux na kuongeza

"Hata hivyo, kwa kuwa suala hili sasa limefika mbali na limeendelea kuhusisha jina langu, familia yangu, biashara zangu na taswira ambayo nimeijenga kwa miaka mingi kwa jasho na kazi kubwa, nimeona ni muhimu kuliongelea kwa uchache.

"Suala hili limewahi kujitokeza hapo nyuma, na kwa kuwa nina uhakika kuwa taarifa hizi hazina ukweli wowote, nilichukua hatua ya kumtafuta mhusika mwenyewe ili kufahamu ni kwanini amesema alichokisema hapo awali.

"Mhusika alithibitisha kwa maneno na sauti yake kuwa hakuwahi kukutana kimwili na mimi wala kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mimi, na hata kuniomba nisilipe uzito suala hili.

“Kwa upande wangu, nimechagua utulivu, ukweli na hatua sahihi za kisheria."


SAUTI YAIBUA MAPYA

Wakati sakata hilo likiwa bado moto, African Boy HQ ilichukua hatua nyingine kwa kutoa kile ilichodai kuwa ni kumbukumbu ya mazungumzo ya simu kati ya Jux na Happy.

Katika sauti hiyo, ambayo uongozi huo umehusisha na mazungumzo ya Jux na Happy, mwanamke anayesikika anadaiwa kueleza kuwa mtoto huyo si mtoto wa Jux.

Sauti hiyo imeongeza uzito wa mjadala kwa kuwa inakinzana na madai ya awali ya Happy kwamba Jux ndiye baba mzazi wa mtoto huyo na kwamba yuko tayari kuthibitisha hilo kupitia DNA.