Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nandy, Billnass wafungua siri ya ‘911’

NANDY Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa maelezo yake, amefanya kazi kubwa kuhakikisha anawapatia mashabiki wake muziki wenye ubora na ladha tofauti.

MSANII wa Bongo Fleva,  Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’, ameanza ukurasa mpya wa safari yake ya muziki baada ya kutangaza ujio wa albamu mpya inayokwenda kwa jina la ‘911’, ikiwa ni mradi unaokuja miaka minane tangu alipotoa albamu yake ya kwanza ‘The African Princess’, mwaka 2018.

Nandy alitangaza ujio wa kazi hiyo katika hafla maalumu iliyofanyika usiku wa kuamkia Novemba 2, 2026, jijini Dar es Salaam na alifunguka kuhusu safari ya maandalizi ya albamu hiyo iliyochukua takribani miaka miwili.

Kwa mujibu wa maelezo yake, amefanya kazi kubwa kuhakikisha anawapatia mashabiki wake muziki wenye ubora na ladha tofauti.

NAND 02

Katika hafla hiyo, Nandy alieleza safari ya albamu mpya imekuwa na changamoto mbalimbali, huku akionyesha kuwa sasa anataka kuanza ukurasa mwingine wa kisanii kupitia ‘911’.

Albamu yake ya kwanza, ‘The African Princess’, iliyotoka mwaka 2018 bado ni sehemu muhimu ya historia yake ya muziki na ilimpatia mashabiki nyimbo zilizovuma kama ‘Aibu’ na ‘Hazipo’.


NAND 01

‘911’ YABEBWA NA LADHA ZA KIMATAIFA

Tofauti na kazi zake zilizopita, ‘911’ imebeba ladha ya kimataifa baada ya Nandy kushirikisha wasanii kutoka mataifa sita ambayo ni Tanzania, Nigeria, Uganda, Ghana, Uingereza na Jamaica.

Albamu hiyo inatarajiwa kuwa na zaidi ya nyimbo 10, hatua inayoonyesha namna msanii huyo anavyotaka kupanua wigo wa muziki wake na kuwafikia mashabiki wa mataifa mbalimbali.

Akitoa ladha ya kile kilichomo ndani ya albamu hiyo, Nandy alipanda jukwaani na kutambulisha kwa mara ya kwanza wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Oya’.