Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nandy, Billnass wafichua siri ya ‘911’

Muktasari:

  • Nandy ametangaza ujio wa kazi hiyo katika hafla maalumu iliyofanyika usiku wa kuamkia Novemba 2, 2026, jijini Dar es Salaam, ambapo alifunguka kuhusu safari ya maandalizi ya albamu hiyo iliyochukua takribani miaka miwili.

MWANAMUZIKI Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’, ameanza ukurasa mpya wa safari yake ya muziki baada ya kutangaza rasmi ujio wa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘911’, ikiwa ni mradi unaokuja miaka minane tangu alipotoa albamu yake ya kwanza ‘The African Princess’, mwaka 2018.

Nandy ametangaza ujio wa kazi hiyo katika hafla maalumu iliyofanyika usiku wa kuamkia Novemba 2, 2026, jijini Dar es Salaam, ambapo alifunguka kuhusu safari ya maandalizi ya albamu hiyo iliyochukua takribani miaka miwili.

Kwa mujibu wa maelezo yake, amefanya kazi kubwa kuhakikisha anawapatia mashabiki wake muziki wenye ubora na ladha tofauti.

Katika hafla hiyo, Nandy alieleza kuwa safari ya albamu mpya imekuwa na changamoto mbalimbali, huku akionyesha kuwa sasa anataka kuanza ukurasa mwingine wa kisanii kupitia ‘911’.

Albamu yake ya kwanza, ‘The African Princess’, iliyotoka mwaka 2018, bado ni sehemu muhimu ya historia yake ya muziki na ilimpatia mashabiki huku nyimbo zilizovuma ni kama ‘Aibu’ na ‘Hazipo’.


‘911’ YABEBWA NA LADHA ZA KIMATAIFA

Tofauti na kazi zake zilizopita, ‘911’ imebeba ladha ya kimataifa baada ya Nandy kushirikisha wasanii kutoka mataifa sita ambayo ni Tanzania, Nigeria, Uganda, Ghana, Uingereza na Jamaica.

Albamu hiyo inatarajiwa kuwa na zaidi ya nyimbo 10, hatua inayoonyesha namna msanii huyo anavyotaka kupanua wigo wa muziki wake na kuwafikia mashabiki wa mataifa mbalimbali.

Akitoa ladha ya kile kilichomo ndani ya albamu hiyo, Nandy alipanda jukwaani na kutambulisha kwa mara ya kwanza wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Oya’.

Wimbo huo ni miongoni mwa kazi zitakazopatikana ndani ya ‘911’ na umetumika kuanza kuwapa mashabiki picha ya aina ya muziki aliouandaa katika mradi huo mpya.


BILLNASS AFICHUA MAANA YA ‘911’

Wakati Nandy akieleza mipango yake ya muziki, mume wake William Nicholaus Lyimo 'Billnass', naye alikuwa sehemu ya hafla hiyo. Billnass alizungumzia namna anavyomuunga mkono mkewe katika safari yake ya muziki.

Moja ya mambo yaliyoibua udadisi zaidi ni maana ya jina ‘911’. Billnass ameeleza kuwa namba hizo zina uhusiano wa karibu na maisha yao binafsi kama wanandoa.

Kwa maelezo yake, namba 11 inahusishwa na mwezi wa Novemba, ambao amezaliwa Nandy, huku ikiwa ni tarehe aliyozaliwa Billnass (Aprili 11, 1993), huku namba tisa ikihusishwa na tarehe ya kuzaliwa kwa Nandy (Novemba 9, 1992).


ALBAMU YATARAJIWA NOVEMBA 27

Kwa upande wa tarehe ya kutoka, albamu hiyo inatarajiwa kuachiwa rasmi Novemba 27, 2026.

Kabla ya hapo, Nandy amepanga pia kufanya matukio maalumu ya kusikiliza albamu hiyo na mashabiki katika baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki na Uingereza, ili kuwapa nafasi ya kuisikiliza kazi hiyo kabla na wakati wa uzinduzi wake.

Ujio wa ‘911’ unafuatia kipindi ambacho amekuwa akipanua shughuli zake za muziki kupitia tamasha lake la Nandy Festival pamoja na lebo yake ya The African Princess.