Mwonekano wa Hamisa Mobetto gumzo, ujauzito, Aziz Ki watajwa
Muktasari:
- Mwonekano huo na mabadiliko umehusishwa na uwezekano wa kuwa mjamzito huku wengi wakimtaja nyota huyo wa Yanga, Aziz KI ambaye ni mumewe licha ya awali kuzagaa stori wawili hao wameachana.
MFANYABIASHARA na mwanamitindo ambaye ni mke wa Stephane Aziz KI, nyota wa Yanga, raia wa Burkina Faso, Hamisa Mobetto amezua gumzo mitandaoni kutokana na mwonekano wake hasa alipokuwa katika sherehe akiwa amevalia vazi jeupe.
Mwonekano huo na mabadiliko umehusishwa na uwezekano wa kuwa mjamzito huku wengi wakimtaja nyota huyo wa Yanga, Aziz KI ambaye ni mumewe licha ya awali kuzagaa stori wawili hao wameachana.
MADAI YA MIMBA YAIBUKA
Kinachotajwa ni umbile lake ambalo limekuwa na mabadiliko na vazi alilokuwa amevaa katika sherehe hiyo ya CIELO iliyokutanisha baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva akiwamo Ben Pol ambaye alionekana akicheza na Hamisa.
Vazi hilo jeupe alilovaa mrembo huyo, lililokata sehemu ya kifua, liliwafanya baadhi ya waliotazama video iliyosambaa mitandaoni kutoa maoni yao kuhusu umbo lake.
Hata hivyo, hakuna uthibitisho rasmi uliotolewa wa Hamisa ni mjamzito.
Mwanaspoti limefanya jitihada za kumtafuta Hamisa kwa njia ya simu ili afafanue mwenyewe madai hayo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Kwa upande mwingine, mama yake Hamisa alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, alisema hajui chochote kuhusu habari ya mwanawe kuwa mjamzito.
Hamisa na Aziz KI, walifunga ndoa ya Kiislamu (Nikah) Februari 16, 2025, katika Msikiti wa Nnuur, uliopo Mbweni, Dar es Salaam. Ndoa hiyo ilitanguliwa na utoaji wa mahari Februari 15, huku sherehe ya harusi ikifanyika Februari 19, 2025, katika Ukumbi wa SuperDome, Masaki, Dar es Salaam.