Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama Mobetto awajibu wanaomuulizia Daylan

MAMA MOBETTO Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo inaonyesha kuwa ladha ya muziki ya Mama Mobetto inagusa pande mbili, huku muziki wa dansi wa Kongo ukiwa sehemu ya muziki anaoutafuta zaidi wakati wa mapumziko na muziki wa Tanzania ukiendelea kuwa sehemu ya burudani yake.

MAMA Mobetto amevunja ukimya kuhusu mjadala unaoendelea wa watu wanaoulizia kuhusu Daylan, mtoto wa Hamisa Mobetto, hasa kuhusiana na namna anavyohusiana na familia ya Diamond Platnumz.

Akizungumza na Mwanaspoti  jijini Mwanza, Mama Mobetto amesema suala la Daylan ni jambo la familia, hivyo hapendi kuingia kwa kina kuhusu namna familia nyingine inavyofanya mambo yake.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mjadala kuhusu Daylan kutokuwa akionekana kwenye machapisho ya baadhi ya wanafamilia wa Diamond Platnumz, huku suala hilo likihusishwa na madai yaliyowahi kutajwa kuhusu uhusiano wa mtoto huyo na Diamond.

MAMA 01


Mama Mobetto amesema kwa upande wa familia yake, wanapompost Daylan na kumuweka karibu nao, kwake hilo linatosha, akisisitiza kuwa hawezi kuzungumza kwa niaba ya watu wengine au kuwalazimisha kufanya wanachotakiwa kufanya.

“Tukimposti  sisi familia ya Hamisa Mobetto inatosha, hao wengine siwezi kuwazungumzia, kila mtu ana maamuzi yake,” amesema Mama Mobetto.

MAMA 02

Ameongeza kuwa suala la Daylan kutokuwa karibu na familia hiyo ni jambo ambalo linapaswa kuachwa kwa wahusika wenyewe, badala ya watu wa nje kuendelea kulizungumzia.

“Mambo hayo ni ya familia yaachwe kama yalivyo,” amesema.

Kauli hiyo ya Mama Mobetto imekuja wakati ambapo jina la Daylan limekuwa likitajwa mara kwa mara kwenye mijadala ya mitandaoni, hasa linapohusishwa na familia ya Diamond Platnumz.