Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka 20 ya Rihanna kuvunja sheria za mchezo

VIBE Pict

Muktasari:

  • Albamu ya mwisho ya kuachia 'ANTI' ambayo ni ya nane kwake ilitoka Januari 28, 2016 baada ya kumaliza mkataba wake na Def Jam Recording, lebo iliyokuwa inasimamia albamu zake tangu mwaka 2005.

MWANAMUZIKI wa pop na RnB duniani, Rihanna, 37, licha ya kukaa kimya kwa miaka mingi bila kutoa albamu anaendelea kufanikiwa huku akiweka rekodi nyingi kupitia muziki kwa kuvunja sheria za mchezo.

Albamu ya mwisho ya kuachia 'ANTI' ambayo ni ya nane kwake ilitoka Januari 28, 2016 baada ya kumaliza mkataba wake na Def Jam Recording, lebo iliyokuwa inasimamia albamu zake tangu mwaka 2005.

Mkali huyo wa kibao 'Diamonds' (2012) alipata umaarufu baada ya kuachia albamu yake ya tatu, Good Girl Gone Bad (2007), iliyokuwa na nyimbo kali kama 'Rehab', 'Hate That I Love You' na 'Umbrella' uliompatia tuzo yake ya kwanza ya Grammy.

Tayari ameuza rekodi zaidi milioni 250 na ndiye msanii wa pili wa kike duniani aliyeuza zaidi kwa muda wote, huku akishinda tuzo tisa za Grammy, tuzo 13 za America Music Awards, tuzo 12 za Billboard na kadhalika.

Ikiwa ni miaka 20 tangu kuachia albamu yake ya kwanza, Music of the Sun (2005), Rihanna anaendelea kufanya vizuri kimauzo kuliko hata wasanii wengi wa sasa licha ya kukaa kimya muda mrefu.

VI 01

Anashikilia rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike duniani kufikisha nyimbo 10 ambazo zimesikilizwa (streams) zaidi ya mara bilioni 1.5 katika mtandao wa Spotify wenye watumiaji zaidi ya milioni 696 kwa mwezi. 

Nyimbo hizo ni We Found Love, This Is What You Came For, Umbrella, Love The Way You Lie, Needed Me, Diamonds, Stay, Work, Only Girl (In The World) na Love On The Brain.

Kwa mafanikio haya, ni wazi Rihanna anazidi kuvunja sheria za mchezo kwa kufanya mambo yake makubwa, ni kama alivyosema katika kolabo yake na Jay Z 'Run This Town' kutoka katika albamu, The Blueprint 3 (2009).

VI 02

"... Maisha ni mchezo, lakini hauna usawa, navunja sheria, kwa hiyo sijali, ndiyo maana naendelea kufanya mambo yangu mwenyewe, nikitembea nikiwa imara dhidi ya mvua (Life's a game, but it's not fair, I break the rules, so I don't care, So I keep doin' my own thang, Walkin' tall against the rain)," anaimba Rihanna.

Kufikia Agosti 2021 utajiri wake ulikadiriwa na Jarida la Forbes kufikia Dola 1.7 bilioni na kumfanya kuwa mwanamuziki wa kike tajiri zaidi duniani na wa pili baada ya Oprah Winfrey kama mburudishaji.

Kwa sasa utajiri wake ni Dola 1.4 bilioni ambao unatokana na muziki, chapa yake ya vipodozi 'Fenty Beauty' anayoimiliki kwa asilimia 50 kwa kushirikiana na LVMH. Pia chapa yake ya nguo za ndani 'Savage X Fenty' anayoimilikia kwa asilimia 28.

VI 03

Rihanna katika mahojiano na Jarida la Vogue la Uingereza anasema ana mpango wa kuachia albamu mpya lakini amekuwa na presha kubwa akiona kama haitakuwa bora kuliko albamu yake ya mwisho (ANTI), basi haifai kutoka.

"Kwa hivyo niligundua kuwa ikiwa nitaendelea kusubiri hadi nihisi imekuwa kamili na bora zaidi, labda itaendelea kuchukua muda na hata milele, labda haitatoka kabisa," alisema mkali huyo wa kibao, Rude Boy (2009).

Rihanna ameshatoa albamu nane ambazo ni Music of the Sun (2005), A Girl like Me (2006), Good Girl Gone Bad (2007), Rated R (2009), Loud (2010), Talk Talk Talk (2011), Unpologetic (2012) na ANTI (2016), huku akitoa EP tatu pia.

VI 04

Licha ya ukimya wake kimuziki, Februari 2023, Rihanna alifanya vizuri katika onyesho lake la Super Bowl, watu milioni 121.017 duniani walitazama akitumbuiza, na ndio show namba tatu ya Super Bowl ilitotazamwa zaidi kwa muda wote.

Shoo za Super Bowl ambazo zimempita ni zile zilizofanyika nyuma yake nazo ni yake Usher (Feb. 2024) iliyopata watazamaji milioni 123.4, na yake Kendrick Lamar (Feb. 2025) iliyopata watazamaji milioni 133.5. 

 Jay Z ambaye ana mchongo mkubwa katika mafaniko ya Rihanna akimsaini Roc Nation na Def Jam, alisema Rihanna ana kipaji kikubwa, ni mwanamke mnyenyekevu tangu mwanzo ambaye anavuka matarajio ya watu kila siku.

VI 05

"Ni mtu aliyezaliwa kwenye kisiwa kidogo cha Barbados na sasa ni mmoja wa wasanii mashuhuri kabisa aliyejitengeneza katika biashara na burudani," alisema Jay Z wakati akizungumza na The Hollywood Reporter.

Ikumbukwe wakati Jay Z akiwa Rais wa Def Jam, ndipo alimsaini Rihanna katika lebo hiyo pamoja na wasanii wengine kama Ne-Yo, Lady Sovereign na Young Jeezy, na kwa wakati huo tayari Kanye West na Ludacris walikuwa ndani ya Def Jam.