Mapenzi yalivyowapaisha mastaa kimataifa
Muktasari:
- Mastaa wengi nchini wamejizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania kupitia uzuri wa kazi zao na mahusiano yao ambayo yamekuwa gumzo kwa mashabiki zao.
KATIKA ulimwengu wa burudani, kuanzia muziki, soka na mitindo, umaarufu haujengwi studio, jukwaani au uwanjani pekee kwani maisha ya mapenzi ya mastaa huwa sehemu ya safari yao ya kukuza majina yao, kuvutia mashabiki wapya na kujizolea umaarufu nje ya nchi zao.
Mastaa wengi nchini wamejizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania kupitia uzuri wa kazi zao na mahusiano yao ambayo yamekuwa gumzo kwa mashabiki zao.
Hilo limeonekana kwa Diamond Platnumz, Harmonize, Jux, Hamisa Mobetto na ambao mahusiano yao yamekuwa yakizungumziwa sambamba na kazi zao.
DIAMOND PLATNUMZ
Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' ni Mwanamuziki maarufu wa Bongofleva ambaye anaoongoza kwa kuwa na mahusiano na wanawake kutoka mataifa tofauti ya Afrika ambayo yalimsaidia kujizolea umaarufu nje ya mipaka ya Tanzania.
Mwaka 2014, alianzisha uhusiano na Zari Hassan Mfanyabiashara na mwanamitindo kutoka Uganda, walibahatika kupata watoto wawili 'Tiffah na Nillan'na walidumu kwa miaka 4 hadi 2018.
Baadaye alianzisha uhusiano na Tanasha Donna mwanamuziki kutoka Kenya, walidumu kwa miaka miwili mwaka 2018 hadi 2020 na kubahatika mtoto mmoja 'Naseeb Junior'.
Kwa sasa uhusiano wake na Zuchu nao ni sehemu ya gumzo la mashabiki kwa kuwa wote ni wanamuziki na wamejenga majina makubwa, maisha yao ya pamoja yanavutia watu wanaofuatilia muziki wao na simulizi zao za mapenzi.
HARMONIZE
Mwanamuziki Rajabu Abdul Kahali 'Harmonize', aliwahi kuwa na mahusiano na wanawake kadhaa kutoka mataifa ya nje ya Afrika wa kwanza ni Sarah ni raia wa Italia walifunga ndoa ya siri 7 Septemba 2019, walidumu kwa mwaka mmoja uhusiano huo ulimsaidia kwa kiasi kikubwa kukuza muziki wake kimataifa.
Baada ya Sarah alianzisha uhusiano na Briana raia wa Australia, ambaye walidumu kwa muda mfupi kuanzia mwishoni mwa 2021 hadi 2022.
JUX
Mwanamuziki Juma Jux, aliwahi kuwa na mahusiano na Nayika Thongom raia wa Thailand walikuwa kwenye walidumu kuanzia 2019 na 2020 uhusiano huo ulianza baada ya Jux kuachana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, msanii Vanessa Mdee.
Na sasa ndoa yake na Priscilla Ojo, mwanamitindo na muigizaji kutoka Nigeria, imekuwa daraja muhimu la kuunganisha Tanzania na soko la Afrika Magharibi.
Pia Jux mwenyewe alikiri kuwa Priscilla na mama yake, muigizaji maarufu Iyabo Ojo, wamechangia kuongeza umaarufu wake Nigeria. Katika mahojiano yaliyoripotiwa na Premium Times Desemba 2025, alisema kuwa kufahamika kwake nchini humo kumeongezeka tangu uhusiano wao ulipojulikana.
HAMISA MOBETO
Mfanyabiashara huyo na mwanamitindo maarufu nchini aliwahi kuwa na mahusiano nje Tanzania ambaye ni mfanyabiashara Kevin Sowax raia wa nchini Togo.
Sasa ni mke wa mwanasoka Stephane Aziz Ki raia wa Burkinafaso, ambaye ni mchezaji timu ya Yanga kwa zaidi ya miaka mitatu hali hiyo imezidi kuongeza hamasa kwa mashabiki wa pande zote mbili. Kuolewa na mwanasoka huyo anayefahamika kumeunganisha zaidi hadhira za mitindo na michezo.
Hamisa mwenyewe aliwahi kuzungumza kuwa ndoa hiyo ilivyoongeza kutambulika kwake ndani na nje ya Tanzania na kumletea kazi za kutangaza biashara 'Brand Ambassador'.
PHINA
Mwanamuziki wa Bongofleva Sarah Michael Kitinga 'Phina' uhusiano wake na Enioluwa Adeoluwa 'Enioluwa'muigizaji na mtangazaji kutoka Nigeria umeedelea kumkuza kimuziki na kumtangaza nje ya mipaka ya Tanzania kwani wameimba nyimbo kadhaa kwa pamoja na kwa kutumia lugha ya Kiswahili kama 'Nakuaminii' 'Smile for me', 'I Do' na 'Kilakshar'
Ikumbukwe kuwa mwanzo wa mahusiano yao ni unahusishwa na harusi ya Jux na Priscilla Ojo ambaye ni rafiki wa karibu na Enioluwa na kupitia tukio hilo Eni alipata nafasi ya kufahamiana na Phina na ukaribu wao ukaendelea kukua hadi kuwa uhusiano wa kimapenzi.