Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubabe wa Joh Makini  katika Bongo Hip Hop!

Muktasari:

  • Ni miongoni mwa wasanii wachache wa Hip Hop Bongo ambao wamekuwa na mwendelezo mzuri wa kufanya vizuri kwa kipindi kirefu. Fahamu zaidi.

RAPA Joh Makini amekuwa akifanya vizuri tangu kipindi cha kundi la River Camp hadi sasa Weusi ambapo nyimbo zake zimeacha kumbukumbu nyingi kwa mashabiki wake.


Ni miongoni mwa wasanii wachache wa Hip Hop Bongo ambao wamekuwa na mwendelezo mzuri wa kufanya vizuri kwa kipindi kirefu. Fahamu zaidi.

1. Katika miaka yake 20 ya umaarufu ndani ya muziki, Joh Makini amefanikiwa kutoa albamu moja, Zamu Yangu (2007), pamoja na Extended Playlist (EP) moja, Wave (2023) yenye nyimbo sita.

2. Albamu yake ilikuja takribani mwaka mmoja baada ya kuvuma kwa mara kwanza kupitia wimbo wake, Chochote Popote (2006) ambao ulitayarishwa na Dunga wa Madungu Digital.

3. Tayari amefanya kazi na wasanii wa kimataifa kama marehemu AKA (Don't Bother - 2015), Chidinma (Perfect Comb - 2016), Davido (Kata Leta - 2017), Tanzanite (Jay Rox - 2022), Bien (Formula - 2024) na kadhalika.

4. Joh Makini alishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2011 kama Msanii Bora wa Hip Hop, akiwabwaga washindani wake wanne ambao ni Fid Q, Ngwea, Chid Benzi na Godzilla. Ushindi huo ulikuja kupitia ngoma yake, Karibu Tena (2010) kutoka katika mikono ya marehemu Pancho Latino aliyeanza kazi studio kwa Dully Sykes, 4.12, zamani Dhahabu Records, kisha akaja kuhamia B'Hits (sasa Bxtra) kwa Hermy B.

5. Ni Joh Makini na G Nako pekee ndio hawajawahi kukosekana katika wimbo wowote wa kundi la Weusi ambalo hadi sasa limetoa albamu moja, Air Weusi (2021) yenye nyimbo 14.

6. Ujio wa Weusi ulitokana na muunganiko wasanii wa River Camp na Nako 2 Nako, ambapo awali ushirikiano wa mara kwa mara wa wasanii wa makundi hayo ulitambulika kama Good Music Family (GMF).

7. Joh Makini ndiye rapa ambaye Rama Ree amefanya naye kolabo nyingi zaidi, Rama Dee alimjua Joh Makini kupitia kundi la Mapacha, na kupitia Joh Makini ndipo akawajua Nikki wa Pili na G Nako. Hadi sasa Rama Dee na Joh Makini kutoka wameshirikiana katika nyimbo kama Sina Time, Furuha Yetu, Tommorow na kadhalika.

8. Video ya wimbo wake, Sijutii (2012) iliyofanyika Arusha ndio ilimtangaza zaidi marehemu Director Nisher, na punde tu akaanza kupewa kazi na wasanii wengine wakubwa hadi alipokuja kushinda Tuzo za Watu 2014.

9. Mdundo wa wimbo wa Joh Makini, Stimu Zimelipiwa (2009), ulitengenezwa na Nahreel kipindi yupo masomoni India katika chuo cha Punjab College ambapo alisomea Computer Science.

10. Joh Makini na Nikki wa Pili wameshafanya nyimbo nyingi pamoja na hata kwenye kundi la Weusi, lakini kolabo yao, Niaje Ni Vipi (2010) chini ya Kama Kawa Records ina heshima yake kwa Nikki. Kwa sababu ndio kolabo yao ya kwanza, na ndio uliomtambulisha Nikki wa Pili vizuri kwenye muziki wa Bongofleva na kumpatia mashabiki wengi.