Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 10 kuhusu Dolly Parton ambayo huenda hukuyajua!

Muktasari:

  • Je, Dolly Parton, mkali wa kibao cha Coat of Many Colors (1971) alikuwa mtu wa namna gani hasa?, haya hapa ni mambo 10 ambayo huenda hukuyajua kuhusu mwanamuziki huyo aliyesifika kwa utunzi na sauti nzuri ambayo iliwakosha wengi.

DUNIA inaomboleza kifo cha Malkia wa Country Music, Dolly Parton ambaye alifariki Agosti 25, 2026 akiwa na umri wa miaka 80. Rais wa Marekani, Donald Trump ameamuru bendera kushushwa nusu mlingoti hadi Septemba mosi kufuatia kifo cha mwanamuziki huyo.

Je, Dolly Parton, mkali wa kibao cha Coat of Many Colors (1971) alikuwa mtu wa namna gani hasa?, haya hapa ni mambo 10 ambayo huenda hukuyajua kuhusu mwanamuziki huyo aliyesifika kwa utunzi na sauti nzuri ambayo iliwakosha wengi.


1. Tina Turner

Huenda unajua kwamba Dolly Parton ndiye aliyeandika wimbo maarufu, I Will Always Love You (1974), ambao baadaye ulikuja kurudiwa na Whitney Houston na kufanya vizuri zaidi. Lakini je, unajua kuwa alimwandikia na Tina Turner? Tina Turner, mkali wa kibao cha What’s Love Got to Do with It (1984), kwa mujibu wa Grammy.com, katika albamu yake ya kwanza, Tina Turns the Country On! (1974), Dolly Parton alimwandikia wimbo uitwao There’ll Always Be Music.


2. Walizaliwa 12

Dolly Parton alizaliwa Januari 16, 1946, huko Pitman Center, Tennessee nchini Marekani akiwa mtoto wa nne katika familia ya watoto 12. Hadi anafariki Jumaanne hii, ni ndugu zake sita pekee ndio waliokuwa hai bado. Aliwahi kusema uwezo wake wa muziki ulitokana na upambanaji wa mama yake, Avie kuitunza familia kubwa. Alisema kila mara mama aliwaburudisha kwa kuwaimbia nyimbo nzuri za zamani na mlo safi.

3. Chanjo ya COVID-19

Mwaka 2020, Dolly Parton alitoa Dola1 milioni, wastani wa Sh2.6 bilioni ili kusaidia utafiti wa chanjo ya COVID-19 ya Moderna, ambao ulikuwa unafanywa na Kituo cha Tiba cha Chuo Kikuu cha Vanderbilt. Utafiti huo ulifanikiwa, na hatimaye Machi 2021, Parton aliposti picha akichanjwa chanjo hiyo na kuwashauri watu wengine kufanya hivyo pia. Picha hiyo aliambatanisha na ujumbe wa utani uliosomeka; Dolly anapata dozi ya dawa yake mwenyewe.


4. Ndoa miaka 60

Mwimbaji Dolly Parton alilkutana na mumewe Carl Dean mwaka 1964 wakati huo akiwa na umri wa miaka 18, walifunga ndoa Mei 30, 1966 katika kanisa la Ringgold Baptist huko Ringgold, Georgia. Hawakupata mtoto katika ndoa yao iliyodumu kwa miaka 60. Dean ambaye alifariki mwaka uliopita, alipenda sana maisha ya faragha hivyo ilikuwa ngumu sana kuwaona pamoja hadharani, Parton alidai siri ya ndoa yao yenye furaha ilikuwa ni kila mmoja kukaa mbali na mwenzake.

5. Mawigi zaidi ya 300

Mwimbaji Dolly Parton alikuwa maarufu kwa muonekano wake wa nywele ambao hakubadilika sana, nywele zake zilizokuwa sehemu ya utambulisho wake, zilimfanya atambulike kwa urahisi lakini nyuma ya pazia kuna siri yake. Siri yenye ni kwamba alikuwa na mawigi mengi ambayo yalifanana kwa sehemu kubwa, alipoulizwa ana mawigi mangapi?, alisema anayo kama 365 hivi kwa sababu kila siku lazima abadilishe hivyo ni muhimu kuwa nayo mengi.

6. 11 Guinness

Kipindi cha uhai Dolly Parton alishinda tuzo nyingi ziki- wemo 11 za Grammy, vilevile aliweka rekodi mbalimbali za dunia za Guinness, rekodi ambazo zilitokana na mafanikio makubwa ya muziki wake. Rekodi zake 11 za Guinness zinajumuisha rekodi ya kuwa mwanamke aliyedumu katika muziki kwa miongo mingi zaidi akiwa na nyimbo nyingi zilizoingia Top 10 ya chati ya Billboard Hot Country Songs, pamoja na kuwa mwanamke aliyetoa albamu nyingi zaidi katika muziki wa Country.


7. Heshima kwa Whitney Houston

Ipo hivi, Dolly Parton ndiye aliyeandika wimbo maarufu wa mapenzi ‘I Will Always Love You’ na kuurekodi mwaka 1973, baadaye 1992, Whitney Houston alikuja kuu-rudia ambapo ulitumia kama soun dtrack ya filamu yake ya The Bodyguard. Lakini toleo hili la Whitney ndilo maarufu zaidi, ulifanya vizuri ukushika namba moja chati za Billboard Hot 100 kwa wiki 14, ukishinda tuzo mbili za Grammy 1994 na hadi sasa unatambulika kama wimbo uliouza zaidi duniani uda wote.


8. Wanaofanana naye

Katika mahojiano na Robin Roberts mwaka 2009, Dolly Parton alifichua kwamba aliwahi kushiriki mashindano ya watu wanaofanana naye lakini akashindwa, na hata hakuukaribia ushindi wenyewe. Alisema katika mashindano hayo yalifanyika huko Santa Monica, aliamua kuboresha muonekano wake kwa makusudi na kupanda jukwaani akiwa amejipamba kama yeye mwenyewe lakini hakushinda!.

9. Jolene ni kisa cha kweli

Wimbo wake Jolene (1973), ambao anamsisitiza mwanamke aliyemtaja kama Jolene kutomchukua mumewe, kisa chake ni cha kweli na kilitokana na dada mmoja ambaye alikuwa mhudumu wa benki ambaye alipenda kumchangamkia mumewe Dean. Mwaka 2008, Dolly Parton aliiambia NPR kuwa mwanamke huyo alimfanya Dean kwenda benki kila wakati, ingawa hakuna kilichokuwa kinaendelea ila alitoa tu wimbo huo, na jina la Jolene lilitoka kwa shabiki yake mmoja.


10. Vitabu milioni 200

Kwa miaka zaidi ya 30, Dolly Parton alikuwa akiwasaidia mamilioni ya watoto duniani kupitia programu yake, Imagination Library inayotoa msaada wa vitabu kwa watotoi, ambapo hadi sasa  zaidi ya milioni 200 vimetolewa. Mwaka 2018 aliliambia Jarida la People kuwa alipata msukumo mkubwa wa kuanzisha programu kwa sababu baba yake mzazi, Lee hakujua kusoma wala kuandika kwa sababu hakwenda shule. “Alikuwa ni kijana wa shambani tu, hivyo ilimbidi afanye kazi za shambani badala ya kwenda shule, kwa hiyo hakuwahi kupata nafasi ya kupata elimu... Hivyo nikataka nifanye kitu kwa ajili ya baba yangu, ni mmoja wa watu waerevu zaidi niliopata kuwajua,”  alisema Dolly Parton.