Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kopa awataka Zuchu, Mondi kuongeza watoto

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Khadija amesema anapenda Zuchu na Diamond waongeze watoto, akieleza kuwa watoto ni baraka na furaha katika familia hivyo hata akipata ujauzito sasahivi Zuchu wala sio tatizo.

MALKIA wa muziki wa taarab, Khadija Kopa, amewataka binti yake, Zuhura Othman ‘Zuchu’, na mkwe wake, Diamond Platnumz, kuongeza watoto katika familia yao, huku akisema watoto wengi ndani ya nyumba ni Baraka tosha.

Akizungumza na Mwanaspoti, Khadija amesema anapenda Zuchu na Diamond waongeze watoto, akieleza kuwa watoto ni baraka na furaha katika familia hivyo hata akipata ujauzito sasahivi Zuchu wala sio tatizo.

“Ningependa Zuchu aongeze watoto na mume wake Diamond, Mungu akiwajaalia. Watoto ni baraka, unapokuwa na watoto wengi unakuwa na furaha kubwa katika familia na ni jambo zuri kwa wanandoa hao na familia yao kwa ujumla, iwapo Mungu atawajaalia,” alisema Khadija.

Matamanio hayo ya Khadija yanakuja miezi michache baada ya Zuchu kujifungua mtoto wake wa kwanza na Diamond, ambaye ni msichana. Wawili hao walimkaribisha mtoto huyo duniani Agosti 2, 2026, hatua iliyoongeza furaha katika familia zao.

Mtoto huyo alitimiza siku 40 Septemba 12, 2026, ambapo wazazi wake waliandaa hafla maalumu katika Ukumbi wa Saint Laurent Garden, Kawe, Dar es Salaam. Hafla hiyo ilihudhuriwa na ndugu, marafiki na watu mbalimbali wa karibu na familia hizo.

Katika sherehe hiyo, Khadija ndiye aliyefichua jina la mtoto huyo kuwa Sandrah Nasibu, huku akieleza furaha yake ya kumpokea mjukuu huyo. Ujio wa Sandrah ulikuwa hatua mpya katika maisha ya Zuchu na Diamond kama wazazi.

Kwa Khadija, furaha ya kuwa na mjukuu mwingine inaambatana na matumaini ya kuona familia ya binti yake ikiendelea kukua. Hata hivyo, ameachia suala la kuongeza watoto mikononi mwa Mungu, akitambua kuwa kupata watoto ni majaliwa.