Kajala: Sijatangaza kuachana na Harmonize!
Muktasari:
- Akizungumza na Mwanaspoti, Kajala amesema hajawahi kutoa tamko la kuachana na Harmonize baada ya hii mara ya mwisho kurudiana, ila anashangaa kuhusishwa na baadhi ya watu hiyo .
STAA wa filamu za Bongo Movie, Frida Masanja ‘Kajala’, amesema hakuna sehemu ambayo amewahi kutangaza kuwa ameachana na mwanamuziki Harmonize, akifafanua msimamo wake kuhusu uhusiano wao.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kajala amesema hajawahi kutoa tamko la kuachana na Harmonize baada ya hii mara ya mwisho kurudiana, ila anashangaa kuhusishwa na baadhi ya watu hiyo .
“We bana achana na masuala ya mapengo ama nini, mimi wapi niliwahi kusehemu nimewakusema nimeachana na Harmonize,” amesema Kajala.
Kauli hiyo imeweka wazi msimamo wake kuhusu madai ya kutengana na Harmonize, huku akisisitiza kuwa hakuwahi kutoa tangazo rasmi la kuvunja uhusiano wao.
Kajala na Harmonize wamekuwa na historia ya uhusiano wenye misukosuko, ikiwamo vipindi vya kutengana na kurudiana. Desemba 2025, wawili hao walirudiana na baadaye Harmonize kumvisha Kajala pete ya uchumba Desemba 30.
Hata hivyo, Septemba 2026, Harmonize aliwahi kueleza kuwa yeye na Kajala hawakuwa pamoja kwa takribani miezi mitatu, kauli iliyozua maswali kuhusu hatima ya uhusiano wao.
Sasa, kupitia mazungumzo yake na Mwanaspoti, Kajala amesisitiza kuwa hajawahi kusema ameachana na Harmonize, akiacha maswali kuhusu hali halisi ya uhusiano wao kwa sasa.