Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Koffi jela miezi 18 kwa utekaji

Koffi jela miezi 18 kwa utekaji

Mwanamuziki nguli wa mtindo wa Rumba kutoka DRC, Koffi Olomide amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kuwateka nyara madensa wake wa zamani.

Koffi, ambaye jina lake halisi ni Antoine Christophe Agbepa Mumba, hakuwepo mahakami wakati hukumu hiyo iliposomwa Jumatatu Desemba 13, na mahakama ya Versailles, nchini Ufaransa.

Katika kesi ya awali msanii huyo alituhumiwa kuwanyanyasa kingono wasichana wanne waliokuwa wakicheza katika bendi yake Quartier Latin lakini mashtaka hayo yalifutwa na katika kosa la utekaji nyara pia atatakiwa kulipa euro 72,000 kama faini ambazo zitagawanywa kwa waathirika.

Unyanyasaji huo ulidaiwa kutekelezwa kati ya mwaka ya 2002 na 2006 katika jumba la kifahari la mwimbaji huyo huko Asnières, Paris.