Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kina Fid Q, Harmonize walivyodata kwa Ray C

Muktasari:

  • Ray C ametoa albamu, ameshinda tuzo na ameshiriki katika miradi na kampeni nyingi za kijamii kutokana na nguvu yake ya ushawishi aliyoipata kupitia kazi yake ya muziki. Fahamu zaidi.

Historia inamtambua Rehema Chalamila maarufu Ray C kati ya wanamuziki wa kike waliojitokeza kwenye Bongofleva na kufanya vizuri tena katika daraja la juu, tayari ana heshima kubwa na himaya aliyojijengea kupitia muziki wake.

Ray C ametoa albamu, ameshinda tuzo na ameshiriki katika miradi na kampeni nyingi za kijamii kutokana na nguvu yake ya ushawishi aliyoipata kupitia kazi yake ya muziki. Fahamu zaidi.


1. Ray C na Stara Thomas kabla ya kutoka kimuziki, kwa nyakati tofauti waliwahi kuwa watangazaji East Africa Radio, ila baadaye Ray C alihamia Clouds FM ambapo safari ya muziki wake ndipo ilipoanza rasmi.


2. Mbali na Ray C na Stara Thomas, mastaa wengine waliowahi kuwa watangazaji kisha kuja kuibukia katika muziki ni pamoja na TID (Magic FM), Lady Jaydee (Clouds FM), na Vanessa Mdee (MTV Base & Choice FM).

3. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds, hayati Ruge Mutahaba, ndiye alimshawishi Ray C kuanza muziki baada ya kuona uwezo wake. Wakati huo Ruge tayari alikuwa akiwasimamia Lady Jaydee na Banana Zorro kupitia Smooth Vibes.


4. Mwanamuziki wa Taarabu, Patricia Hillary, ndiye aliyeandika wimbo uliomtoa Ray C kimuziki, Mapenzi Yangu (2003), ambao pia ndio uliobeba jina la albamu yake ya kwanza.


5. Mwaka 2003 na 2007, Ray C alishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike, huku msanii mwenzake wa Smooth Vibes, Banana Zorro akishinda Msanii Bora wa Kiume katika miaka yote miwili.


6. Albamu ya pili ya Ray C, Sogea Sogea (2007), ilishirikisha wanamuziki kama TID, Nako 2 Nako Soldiers na D. Gritty kutokea Marekani ambaye alikuja Tanzania 2006 akiwa ameongozana na rapa mwenzake, Loon. Huyo Loon alikuja Tanzania kushuti video ya wimbo wake, Distracted (2006), ambapo Miss Tanzania na Miss World Africa 2005, Nancy Sumari alitokea kwenye video hiyo. Vilevile Loon na D. Gritty wakiwa bado Bongo, walishiriki katika wimbo wa rapa wa Nako 2 Nako, Ibra Da Hustler, Worldwide Bachelor (2006) ambao ulitayarishwa na Ambrose Dunga wa Mandugu Digital.


7. Ray C aliwashirikisha Nako 2 Nako (Lord Eyes & Ibra Da Hustler) katika wimbo wake, Kwa Ajili Yako (2007) ukitayarishwa na Dunga, na wakati huo Ray C na Lord Eyes wakiwa na uhusiano.

8. Mbali na Ray C na Lord Eyes, mastaa wengine wa muziki Bongo waliowahi kuwa wapenzi na kushirikiana katika nyimbo zao ni pamoja na Lady Jaydee na Spicy Music (Together Remix), Diamond Platnumz na Tanasha Donna (Gere) na Vanessa Mdee na Jux (Juu & Sumaku). Pia kuna Amini na Linah (Mtima Wangu & Nimenasa), Kusah na Ruby (Kelele, Chelewa & Nadondosha), Izzo Bizness na Abela (Dangerous Boy, Umeniweza & Tumeoana), One The Incredible na Grace Matata (Salamu & Light It Up), Shilole na Nuh Mziwanda (Ganda la Ndizi) na kadhalika.


9. Baada ya kuwa staa mkubwa katika Bongofleva, Ray C alitokea kuvutiwa na waimbaji wawili wa kike kutokea Marekani, nao ni Ciara na Rihanna, bilionea wa Barbados ambaye ni mshindi wa tuzo za Grammy mara tisa.


10. Ray C aliyepewa a.k.a ya Kiuno Bila Mfupa kutokana na uchezaji wake, wasanii mbalimbali wameitaja sifa yake hiyo katika ngoma zao, baadhi yao ni Mwana FA (Mabinti 2002), Fid Q (Kadi na Ua Rose 2005), Mangwair (Speed 120 - 2010), Young Killer (Mrs SuperStar 2013) na Harmonize - (Uno 2019).