Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dullvani afungukia mwonekano wake

DULLIVAN Pict

KWA takribani miezi miwili, mwonekano wa mchekeshaji Dullvani umeendelea kuzua maswali miongoni mwa mashabiki wake kutokana na kupungua kwa mwili wake. Mabadiliko hayo yameibua maswali kuhusu kinachoendelea katika maisha yake.

Akizungumza na Mwanaspoti wakati wa uzinduzi wa filamu yake mpya ya Ukweni, uliofanyika Novemba 14, 2026, katika ukumbi wa EACLC, Ubungo jijini Dar es Salaam, Dullvani amesema hapendi kuwa na mwili mnene, huku akitaja matumizi ya baadhi ya virutubisho alivyowahi kutumia kuwa miongoni mwa mambo anayodhani yamechangia kupungua kwake.

“Mimi sipendi unene. Lakini pia kuna supplements ambazo nilishawahi kutumia, ndiyo nadhani pia zimechangia kwenye kunikondesha, na kuwa hivi afya yangu,” amesema Dullvani.

Aidha Dullvani amesema, mashabiki zake wasimshangae wala kushtuka kutokana na afya yake kwani wamekuwa wakimuonea huruma na hali ya kuwa yeye anajiona yuko sawa.

"Napata simu nyingi sana, meseji kutoka kwa watu wangu wa karibu na mashabiki zangu kutokana na afya yangu kupungua, hivyo nawaomba wasinishangae wala kushtuka mimi niko salama kabisa."


DULL 01

CHANZO CHA UKIMYA  WAKE

Mbali na mabadiliko ya mwonekano wake, Dullvani amezungumzia pia ukimya wake wa muda mrefu, amesema alikuwa akipata mialiko ya matukio mbalimbali lakini alishindwa kuhudhuria.

Amesema maandalizi ya Filamu ya Ukweni ambayo inapatikana kupitia mtandao wa Paoflix, ndiyo yaliyomfanya ajitenge na matukio ya burudani kwa kipindi hicho, kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa akipata katika kuhakikisha kazi hiyo inakamilika.

“Nimekaa kimya muda mrefu, ni siku nyingi sana. Sikutaka kuonekana popote. Nilikuwa naalikwa matukio yote ambayo unayajua, lakini nilikuwa siwezi kuonekana kwa sababu hili jambo ambalo limefanyika leo (juzi) ndiyo jambo pekee ambalo limekuwa likinipa sana mawazo,” amesema.


DULL 02

UKWENI NI MAISHA YAKE HALISI

Akizungumzia maudhui ya filamu hiyo, Dullvani amesema sehemu kubwa ya simulizi iliyomo imetokana na matukio halisi aliyopitia katika maisha yake, yakiwemo changamoto za kimahusiano yaliyopita na namna baadhi ya watu wanavyoitazama kazi ya uchekeshaji.

Miongoni mwa matukio hayo ni kukutana na mama wa aliyekuwa mpenzi wake, ambapo mwitikio alioupata kuhusu kazi yake ulimuumiza.

“Mimi sipendi kuzungumzia vitu sana, lakini kwenye mahusiano yangu yaliyopita, kuna siku nilishawahi kukutana na mama mkwe ambaye mtoto wake ni mwanamke ambaye mahusiano yake yamepita,” amesema.

Dullvani alisema tukio hilo lilimfanya kutafakari kwa nini baadhi ya watu hudharau kazi ya uchekeshaji, huenda wakidhani kuwa kinachofanyika katika kazi hiyo si jambo la kuchukuliwa kwa uzito.

“Unahisi kwa nini watu wanadharau sana wachekeshaji? Labda kwa sababu wanahisi kazi ya comedy kinachofanyika pale watu wanakuwa mara nyingi hawako serious,” amesema.

Kwa mujibu wa Dullvani, changamoto za mapenzi ni sehemu nyingine ya simulizi ya Ukweni, huku akitumia pia uzoefu mwingine wa maisha yake kujenga maudhui ya filamu hiyo.