Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Udhaifu timu zinazopewa nafasi ya ubingwa NBA

Muktasari:

  • Ikumbukwe kuwa msimu wa 2026-27 una timu nyingi zenye uwezo mkubwa, lakini hadi sasa hakuna iliyojitenga na nyingine kwa kiwango cha kutawala mashindano. Timu zote zimecheza kati ya mechi 11 na 15, hivyo tayari kuna idadi ya kutosha ya michezo inayoweza kutumika kupima maeneo yanayohitaji maboresho.

LOS ANGELES, MAREKANI: UKIONDOA timu moja inayozitawala nyingine kwa kiwango kikubwa, kuna timu kadhaa zinazokaribia kilele cha ubora katika NBA msimu huu na ni sita pekee. Hapa tunakuchambua udhaifu wa kila moja na mambo yanayopaswa kubadilika ili ziweze kufikia kiwango cha juu zaidi.

Ikumbukwe kuwa msimu wa 2026-27 una timu nyingi zenye uwezo mkubwa, lakini hadi sasa hakuna iliyojitenga na nyingine kwa kiwango cha kutawala mashindano. Timu zote zimecheza kati ya mechi 11 na 15, hivyo tayari kuna idadi ya kutosha ya michezo inayoweza kutumika kupima maeneo yanayohitaji maboresho.

Kwa ujumla majeraha yamechangia kwa baadhi ya timu kuathirika kimchezo, huku kila kikosi kikiwa na aina fulani ya udhaifu. Timu zinazoweza kuwa bora zaidi ni zipi? Kuna tatu za juu kutoka kila kanda yaani Mashariki na Magharibi, kwa kuzingatia nafasi zake katika utabiri wa kabla ya msimu na hali ya sasa kupitia kipimo cha TRACR kinacholinganisha kiwango cha timu kwa kuzingatia ubora dhidi ya wastani wa NBA.  TRACK hutumia mfumo unaojumuisha takwimu za kina na vigezo vingine kupima tofauti ya pointi ambazo timu inazalisha au kuruhusu kwa kila nafasi 100 za kumiliki mpira ikilinganishwa na wastani wa ligi. Karibu!


OKLAHOMA CITY THUNDER

Udhaifu wa Thunder ni kukosa wachezaji wa kutosha wenye ubora benchi, kwani msimu uliopita ilikuwa na kikosi kipana zaidi NBA, lakini iliwapoteza Luguentz Dort, Aaron Wiggins na Isaiah Joe, huku Jalen Williams, Cason Wallace na Chet Holmgren wakikosekana muda mrefu kutokana na majeraha. Suluhisho kwa sasa ni kuongeza wachezaji wenye ubora kupitia dirisha la kubadilishana wachezaji kabla ya mwisho wa Februari, 2027. Herbert Jones wa New Orleans Pelicans anaweza kuwa chaguo kutokana na mshahara wake wa chini ya Dola 15 milioni.


SAN ANTONIO SPURS

Udhaifu wa timu hii ni kuwa na walinzi wengi wenye uwezo mkubwa, ambapo imekuwa na changamoto ya kuwaunganisha De’Aaron Fox, Stephon Castle na Dylan Harper, ambao wana majukumu yanayofanana. Licha ya uwezo, hakuna aliyefikia kiwango cha nyota anayeweza kuamua matokeo dhidi ya timu imara. Fox anashika nafasi ya 32 katika kipimo cha DRIP. Pia, ratiba yao ya awali haijawakutanisha mara nyingi na timu zenye ushindani mkubwa. Suluhisho pekee ni walinzi hao kuweka maslahi binafsi kando na kukubali majukumu tofauti. Pia, Castle au Harper wanahitaji kuongeza viwango ili kuongoza mashambulizi. Fox, ambaye yupo msimu wa 10, huenda akawa amefikia kiwango chake cha juu.


NEW YORK KNICKS

Udhaifu uliopo ni ulinzi wa eneo la karibu na kikapu; Knicks imeanza vizuri, lakini kuondoka kwa Mitchell Robinson aliyejiunga na Boston Celtics kumeacha pengo katika ulinzi wa karibu na kikapu. Karl-Anthony Towns ana kiwango cha kuzuia mitupo cha asilimia 1.8, tofauti na asilimia 5.0 za Robinson. Andre Drummond, aliyechukua nafasi yake, hana ubora mkubwa katika eneo hilo. Suluhisho ni kusaka mchezaji mwenye thamani kubwa kuliko inavyoonekana sokoni au kumpa nafasi zaidi Mohamed Diawara. Mshambuliaji huyo ana kiwango cha kuzuia mashambulizi cha asilimia 3.6, lakini amecheza dakika 61 pekee katika mechi tano.


BOSTON CELTICS

Udhaifu wa kikosi hicho ni kufunga karibu na kikapu, na kinategemea zaidi mitupo ya pointi tatu, kikiwa nafasi ya tano kwa majaribio, lakini ni  29 kwa pointi kinazopata ndani ya eneo la karibu na kikapu. Hali hiyo inaweza kuwa tatizo katika mchujo, hasa baada ya kupoteza mfululizo wa mechi licha ya kuongoza 3-1 dhidi ya Philadelphia 76ers msimu uliopita. Suluhisho, wanahitaji mshambuliaji anayeweza kupenya kuelekea kikapuni bila kudhoofisha ulinzi. Naji Marshall wa Dallas Mavericks anaweza kuwa chaguo, hasa ikiwa Mavericks watashindwa kuwania nafasi nzuri ya mchujo.


HOUSTON ROCKETS

Rockets wanamtegemea zaidi Steven Adams. Ingawa wanao wachezaji wenye uwezo mkubwa, lakini Adams ni muhimu katika kurejesha mipira inayoshindwa kuingia wavuni na kuipa timu nafasi nyingine za kushambulia. Changamoto ni umri wake wa miaka 33, kucheza mchezo mmoja pekee na historia ya majeraha. Kwa sasa suluhisho ni kutumaini Adams atarejea akiwa fiti, lakini pia kutafuta mchezaji mwenye mchango unaofanana naye au kumuendeleza Oscar Tschiebwe kuziba pengo hilo.


DETROIT PISTONS

Udhaifu wao ni kukosa wachezaji wanaofanya vizuri katika ushambuliaji na ulinzi. Pistons wana ulinzi imara, lakini kiwango cha ushambuliaji ni cha wastani, wakiwa nafasi ya 13. Cade Cunningham na Jalen Duren ndiyo wachezaji pekee wenye viwango chanya katika vipimo vya O-DRIP na D-DRIP vya ushambuliaji na ulinzi. Suluhisho ni kusajili mshambuliaji wa pembeni anayeweza kutupa mitupoi ya mbali, kuzuia wapinzani na kupunguza mzigo wa kuandaa mashambulizi kwa Cunningham. Meneja Mkuu Trajan Langdon anapaswa kuanzisha mazungumzo na timu yake ya zamani, Pelicans, kuhusu kumsajili Trey Murphy III.