Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kampeni kumpigia kura Miss Grand Tanzania yashika kasi

Muktasari:

  • Jihan, maarufu katika mitandao ya kijamii kupitia akaunti ya jihandimack, amepenya raundi ya pili ya mashindano hayo na sasa yupo katika kundi A lenye jumla ya washiriki 10 kutoka, Uingereza, Peru, Mexico, Indonesia, Sri Lanka, Nicaragua, Kazakhstan, Dominican Republic na Chile.

Kampeni ya kumuwezesha Miss Grand Tanzania Jihan Dimack, kunyakua taji la Miss Grand International 2026, imeshika kasi baada ya mrembo huyo kufanikiwa kuingia katika 40 bora ya mashindano hayo.

Jihan, maarufu katika mitandao ya kijamii kupitia akaunti ya jihandimack, amepenya raundi ya pili ya mashindano hayo na sasa yupo katika kundi A lenye jumla ya washiriki 10 kutoka, Uingereza, Peru, Mexico, Indonesia, Sri Lanka, Nicaragua, Kazakhstan, Dominican Republic na Chile.

Katika hatua hiyo, nchi mbili kutoka kila kundi zinatarajiwa kusonga mbele, hali iliyochochea kampeni miongoni mwa Watanzania wanaotaka kumuona Jihan akiendelea na safari hiyo.

Kampeni hiyo imejikita zaidi katika kuhamasisha Watanzania kufuatilia akaunti rasmi ya Miss Grand International pamoja na akaunti ya Jihan. Kushiriki machapisho yake kwa njia ya kuposti na kushiriki katika zoezi la mashindano hayo raundi ya pili.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ushiriki kupitia wafuasi na repost ni miongoni mwa vitu vinavyopewa uzito katika hatua hiyo. Hivyo mashabiki wamekuwa wakihamasishana kuongeza ushiriki wao ili kuongeza nafasi ya Tanzania kusonga mbele.

Ukurasa wa Instagram wa Jihan tayari umefikia zaidi ya maoni milioni moja, like zaidi ya 192,000, repost zaidi ya 7,400 na share zaidi ya 315,000, idadi inayotajwa kuonyesha mwitikio wa Watanzania na mashabiki wengine katika kampeni hiyo.

Mbali na kampeni hiyo ya mitandaoni, Miss Universe Tanzania 2026, Queen Elizabeth Makune, amewaomba Watanzania kumuunga mkono Jihan ambaye anaiwakilisha Tanzania katika Miss Grand International 2026.

Makune amewataka Watanzania kushiriki katika zoezi hilo kupitia akaunti rasmi ya Miss Grand International kwa kuifuatilia na kushiriki katika chapisho maalumu linalohusu mashindano hayo kwa raundi ya pili.

Miss Grand International ni moja ya mashindano makubwa ya urembo yanayokusanya wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Kwa hatua ya sasa, kampeni hiyo imeendelea kuwa sehemu muhimu ya safari ya Jihan, huku Watanzania wakihamasishwa kushiriki kwa wingi katika shughuli za mitandaoni zinazohusishwa na kura na ushiriki wa mashabiki.

Namna ya kupiga kura

Kwa mujibu wa waandaaji, kura zinapigwa kupitia akaunti rasmi ya Instagram ya Miss Grand International kwa kushiriki katika chapisho la picha la mshiriki anayemuunga mkono. Kanuni kamili za upigaji kura pamoja na namna alama zinavyohesabiwa zitaelezwa katika maelezo ya kila chapisho.

Waandaaji pia wameweka sharti kwamba kabla ya kupiga kura, mshiriki wa kampeni anatakiwa kwanza kuifuatilia akaunti rasmi ya Miss Grand International Instagram.

Mashindano hayo yamefanyika nchini Thailand, ambayo pia imetangazwa kuwa mwenyeji wa Miss Grand International 2027 wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya mashindano hayo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mashindano hayo yatarejea Thailand ambako safari ya Miss Grand International ilianzia, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 15 ya historia ya mashindano hayo.