Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jux: Simu yangu ipo huru, hata mke wangu ruksa

Muktasari:

  • Agosti 25, 2025 Jux na Priscilla walibarikiwa kupata mtoto wa kiume aliyepewa jina la Rakeem.

NYOTA maarufu wa Bongo Fleva, Jux, amesema kuwa hana mipaka ya simu kwa mke wake, hivyo amempa uhuru wa kushika simu yake muda wowote anaotaka.

Akizungumza na Mwanaspoti, msanii huyo amesema kuwa mke wake ni muelewa hivyo amempa uhuru wa kushika simu yake vile anavyojisikia kwa sababu haoni sababu ya kumficha chochote.

“Unajua kitu ambacho wanaume wengi wanakosea ni kuwanyima uhuru wake zao, na asilimia kubwa ya wanaume wanadhani kumpa mke wako simu aitumie muda wote anaotaka ni ushamba, sio kweli kama umeamua kumuweka ndani kuna haja gani kwa wewe kumficha kila kitu? Mimi mke wangu anashika simu yangu muda wote na mimi hivyohivyo nashika yake, hakuna tatizo kabisa,”  amesema Jux.

Februari 07, 2025, Jux alifunga ndoa na mfanyabiashara na mwigizaji wa Nigeria, Priscilla iliyohudhuriwa na ndugu na marafiki wa karibu akiwamo Diamond Platnumz, Zuchu, S2kizzy, Ommy Dimpoz na wengineo.

Agosti 25, 2025 Jux na Priscilla walibarikiwa kupata mtoto wa kiume aliyepewa jina la Rakeem.