Mke wa Jux, Omoni Oboli wang’ara Nigeria
Muktasari:
- BOZ Diamond iliandaa jioni ya kifahari ya karibu na iliyotulia kwa ajili ya wateja wake muhimu zaidi katika hafla hiyo ya Love & Boz Circle- Prive, iliyokuwa na lengo la kipekee kudhihirisha uaminifu, ubunifu, na simulizi za kipekee zilizo nyuma ya kila kazi ya BOZ.
MWANADADA Priscilla Ojo, mke wa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Jux sambamba na Omoni Oboli wameng’ara katika hafla ya tukio maalumu la BOZ ‘Love & Boz Circle-Prive lililofanyika juzi Nigeria.
BOZ Diamond iliandaa jioni ya kifahari ya karibu na iliyotulia kwa ajili ya wateja wake muhimu zaidi katika hafla hiyo ya Love & Boz Circle- Prive, iliyokuwa na lengo la kipekee kudhihirisha uaminifu, ubunifu, na simulizi za kipekee zilizo nyuma ya kila kazi ya BOZ.
Tukio hilo la kipekee, lililoongozwa na mwanzilishi wa BOZ, Sherifat Mohammed, liliwakutanisha wageni walioteuliwa kwa umakini, akiwamo mwigizaji na mtayarishaji wa filamu aliyeshinda tuzo Omoni Oboli, mrembo maarufu wa mitindo na mke wa Jux, yaani Priscilla Ojo na mjasiriamali Akin Faminu pamoja na wageni wengine mashuhuri.
Tofauti na maonyesho ya kawaida ya vito vya thamani vinavyojaa mwonekano wa kifahari kupita kiasi, Love & Boz Circle-Prive ilifanyika kwa umaridadi wa hali ya juu usio na makeke.
Tukio hili lilibuniwa kama ishara ya upendo na shukrani kwa wateja ambao wamekuwa sehemu muhimu ya safari ya BOZ.
Sherifat alitoa mwanga wa falsafa inayouongoza mtindo wake: kila almasi ina simulizi, kila muundo una roho na kila mteja anashika sehemu ya urithi unaoendelea kukua wa BOZ.
“Ninyi si wateja tu, ni sehemu ya safari hii,” alitoa ujumbe uliotawala anga tulivu la jioni hiyo.
Wageni walipata nafasi ya kuona ubunifu wa ndani wa BOZ, kufurahia shampeni, mazungumzo ya kuvutia na vito vilivyoangaza kwa ustadi, huku mke wa Jux na Omoni wakiwa gumzo kwa namna walivyofunika ukumbini.
Priscilla Ojo na Jux walifunga ndoa Februari 7 mwaka huu na tayari wana mtoto mmoja wa kiume.