Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jux aandaa tamasha ukweni

Muktasari:

  • Jux alifunga ndoa na Priscilla Ojo, binti wa muigizaji wa Nollywood, Iyabo Ojo na miezi mitatu baadaye wakabarikiwa kupata mtoto wa kiume aitwaye Rakeem.

VYOMBO vya habari Nigeria vimeripoti msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux (King of Heart), Desemba 18, mwaka huu atazindua tamasha lake la kwanza nchini humo lijulikanalo kama Juma Jux in Lagos.

Jux alifunga ndoa na Priscilla Ojo, binti wa muigizaji wa Nollywood, Iyabo Ojo na miezi mitatu baadaye wakabarikiwa kupata mtoto wa kiume aitwaye Rakeem.

Tangu Jux afunge ndoa na Priscilla ambaye ni mtu maarufu na mwenye ushawishi mkubwa Nigeria, Mtanzania huyo amechukua tuzo ya The Headies kama msanii bora Afrika, lakini ngoma zake kama God Design ziliingia kwenye 'trending' namba moja nchini humo.

Sasa wakati anaendelea kuweka rekodi nchini humo, inaelezwa Jux anaandaa shoo yake mwenyewe Nigeria na tayari tiketi zimeanza kuuzwa. Pia, familia ya mkewe imekuwa mstari wa mbele kusapoti jambo hilo ikifanya chalenji mbalimbali za kuwahamasisha mashabiki wajaze ukumbi.

Jux aliandika kwenye mtandao wa Instagram "Upendo na msaada ambao mmeonyesha kwangu umekuwa wa ajabu sana. Najisikia nyumbani hapa Nigeria. Kila jiji lina midundo yake, lakini Lagos lina roho."

"Tarehe 18 Desemba, tutafanya tukio kubwa tukileta pamoja upendo, maisha na urithi Kutoka Tanzania hadi Nigeria, moja kwa moja."

“JUMA JUX IN LAGOS” Hii si tamasha tu, bali ni kama kukutana tena kwa familia na siwezi kusubiri kushirikiana nanyi acha hadithi ianze na tuburudike kwa pamoja Decemba iwe ya kuvutia kabisa."