Johari alia na ndoa
Muktasari:
- Johari amesemsa kwa sasa yupo single na yuko tayari kuingia kwenye ndoa endapo mwanaume mwenye nia hiyo atajitokeza.
BAADA ya miaka kadhaa ya mashabiki kusubiri kusikia habari za ndoa yake, mwigizaji mkongwe wa filamu Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka tena kuhusu suala hilo, safari hii akisema bado hajampata mwanaume wa kumuoa.
Johari amesemsa kwa sasa yupo single na yuko tayari kuingia kwenye ndoa endapo mwanaume mwenye nia hiyo atajitokeza.
Akizungumza na Mwanaspoti, Johari amesemsa kwa hatua aliyofikia sasa hana tena orodha ndefu ya sifa anazozitafuta kwa mwanamume, bali anachohitaji ni mtu aliye tayari kuwa naye kwenye ndoa.
“Bado sijapata mtu wa kunioa. Naweza nikasema hivyo, nipo free. Mtu akijitokeza kunioa, nipo tayari. Kwa sasa nilipofikia, awe tu anapumua,” amesemsa Johari.
Kauli hiyo ni tofauti kidogo na alivyowahi kueleza hapo nyuma kuhusu aina ya mwanaume anayemtaka, ambapo katika mahojiano yake na Mwanaspoti ya Agosti 27, 2025, amesemsa wanaume wengi waliokuwa wakijitokeza walikuwa tayari wameoa na walitaka awe mke wa pili.
Johari amesemsa wakati huo kuwa hawezi kuingia kwenye ndoa ya wake wengi kutokana na kutoweza kuvumilia changamoto za ukewenza na wivu alionao.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa bado yuko tayari kuolewa na mwanaume ambaye atamheshimu, kuwa mwaminifu na kumuunga mkono katika mambo anayoyafanya.
Mwaka mmoja kabla, Juni 2024, Johari pia aliliambia Mwanaspoti kuwa alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi, lakini akasema amekua kiakili na hataki tena kuweka maisha yake ya mapenzi hadharani kama alivyokuwa akifanya zamani.
Sasa, akiwa amerudi tena kwenye mjadala wa ndoa, Johari anaonekana kutokuwa na presha ya kutafuta mwanaume mwenye vigezo vingi.