Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jihan achomoza top 8 Miss Grand International

Muktasari:

  • Jihan amesema mafanikio hayo yamechangiwa na kura, machapisho, jumbe na ushiriki wa Watanzania walioungana kumuunga mkono katika mashindano hayo.

Miss Grand Tanzania 2026 Jihan Dimack, amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano na sapoti waliompa katika mchakato wa kura za kipengele cha Country’s Power of the Year kwenye mashindano ya Miss Grand International, baada ya Tanzania kuingia hatua ya nane bora.

Jihan amesema mafanikio hayo yamechangiwa na kura, machapisho, jumbe na ushiriki wa Watanzania walioungana kumuunga mkono katika mashindano hayo.

Kupitia ujumbe wake, Jihan amesema kila kura iliyopigwa, chapisho lililoshirikishwa, ujumbe wa kumtia moyo na dua vilikuwa sehemu ya safari hiyo hadi Tanzania kufanikiwa kuingia kwenye nafasi nane bora.

“Kutoka moyoni, asanteni sana kila mmoja aliyekuwa nasi kwenye safari hii. Kila kura, kila post, kila share, kila ujumbe wa kutia moyo na kila dua yenu imekuwa sehemu ya mafanikio haya,” amesema Jihan.

Amesema hatua hiyo ni sababu ya Watanzania kusherehekea, akieleza kuwa ushirikiano wao umeonyesha nguvu ya Tanzania katika jukwaa hilo la kimataifa.

“Leo tuna sababu ya kusherehekea. Tanzania imefanikiwa kuingia Top 8, Country’s Power of the Year.

Tumeonyesha dunia nguvu ya Tanzania, tumeungana kama taifa na tukasimama nyuma ya bendera yetu kwa upendo na mshikamano,” amesema.

Jihan amewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono katika hatua inayofuata, ambapo washiriki wanachuana kupata nafasi ya kuingia Top 4.

Kwa mujibu wa Jihan, kura za hatua hiyo zinapigwa kupitia tovuti na zoezi hilo litadumu kwa saa 24, kuanzia saa 2 usiku leo hadi kesho.

“Hatimaye tumefanya hivyo. Asanteni Tanzania. Hii ni yetu sote. Safari bado inaendelea,” amesema.