Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jaydee aja na Jide Silver miaka 25 ndani ya gemu

Muktasari:

  • Jay Dee aliyeachia ngoma ya kwanza ya Nakupenda mwaka 2000, ataadhimisha miaka 25 katika muziki wake Juni, mwaka huu maadhimisho ambayo yatafanyika kwa siku tano kuanzia Juni 9.

MWIMBAJI mkongwe wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jay Dee' amejitolea kuwa balozi wa ugonjwa wa saratani, akitumia maadhimisho ya miaka 25 katika muziki wake kuijengea jamii ufahamu juu ya saratani, ugonjwa ambao amesema ulipoteza maisha ya wazazi wake.

Jay Dee aliyeachia ngoma ya kwanza ya Nakupenda mwaka 2000, ataadhimisha miaka 25 katika muziki wake Juni, mwaka huu maadhimisho ambayo yatafanyika kwa siku tano kuanzia Juni 9.

Katika maadhimisho hayo, yaliyopewa jina la Jide Silver, mwimbaji huyo ataanza kwa kuijengea jamii ufahamu juu ya ugonjwa wa saratani akishirikiana na Hospitali ya Ocean Road, siku ya Juni 9.

"Nimejitolea kuwa balozi wa saratani kwa kuwa ni ugonjwa ambao ulichukua maisha ya wazazi wangu," amesema Jay Dee.

Akizungumzia matukio mengine atakayofanya katika maadhimisho ya miaka 25 kwenye muziki, Jay Dee amesema Juni 10, atashiriki katika kazi za sanaa za mikono.

"Lengo ni kuwaunga mkono wasanii wa sanaa za mikono na siku inayofuata kwa kuwa napenda upishi itakuwa ni siku ya Jide Misosi ambayo pia itawapa fursa wapishi mbalimbali hasa wasiokuwa maarufu kuonyesha ujuzi wao."

Kwa mujibu wa Jay Dee, Juni 12 atazindua kitabu cha safari yake ya muziki kiitwacho Jide Diary na kilele cha maadhimisho hayo ni Juni 13 akizindua albamu ya 10 aliyoipa jina la Silver, tukio hilo likifanyika kwenye ukumbi wa The Super Dome, Dar es Salaam ikipambwa na rangi nyeusi na fedha.

Akizungumzia safari ya miaka 25, Lady Jay Dee amesema haikuwa rahisi kwa binti kama yeye kuhimili kupambana mbele ya wanaume wengi, lakini hakukubali kukata tamaa.

"Watu wanaweza kuona ni kama juzi tu, lakini ilikuwa miaka 25 ya mapambano katikati ya wanaume," amesema Lady Jay Dee kwa hisia.

Alisema katika Diary ya Lady Jay Dee ataeleza safari yake ya muziki kwa miaka 25 ilivyokuwa hadi kubaki kuwa miongoni mwa wanamuziki wachache wakongwe wanaotamba hadi sasa.

Akimzungumzia mwimbaji huyo, mwandishi wa habari nguli, Absalom Kibanda amesema tangu amemfahamu Jay Dee, kipaji chake kinazidi kupanda na kuendana na wakati.

Amesema mwaka 2000 wakati Kibanda akiwa mfanyakazi wa Mwananchi Communications Limited, alimfahamu Lady Jay Dee kama mtangazaji na mwanamuziki ambaye hajawahi kuchuja katika gemu.