Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isha Mashauzi ataja ‘Top 5’ yake kwa sauti na utunzi

TOP 5 Pict

Muktasari:

  • Isha aliadhimisha miaka hiyo kupitia tamasha lililofanyika Oktoba 24, 2026, lililowakutanisha mashabiki wa Taarab na wadau wa burudani.

MWIMBAJI wa Taarab, Isha Mashauzi, maarufu kama Queen of the Best Melody, ametaja waimbaji watano anaowakubali kwa ubora wa sauti na uwezo wa kutunga nyimbo katika muziki huo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Isha alitaja majina ya Mzee Yusuf, Khadija Omar Kopa, Thabit Abdul, Hemedi Omar na Abdul Misambano kuwa ndiyo yanayounda orodha yake ya watano bora.

“Hawa hapa Top 5 yangu ni Mzee Yusuf, Khadija Omar Kopa, Thabit Abdul, Hemedi Omar na Abdul Misambano,” alisema Isha.

Orodha hiyo inaonyesha namna Isha anavyotambua uwezo wa wasanii wenzake katika muziki wa Taarab, unaohitaji sauti yenye mvuto pamoja na tungo zenye ujumbe unaogusa mashabiki.

Mzee Yusuf na Khadija Omar Kopa ni miongoni mwa majina yanayofahamika katika muziki huo, huku Thabit Abdul, Hemedi Omar na Abdul Misambano nao wakiingia katika orodha ya wasanii wanaokubaliwa na Isha kwa vigezo hivyo.

Uteuzi huo umefanyika wakati Isha akiadhimisha miaka 20 ya safari yake ya muziki, hatua inayompa nafasi ya kutazama alikotoka na kutambua wasanii anaowakubali katika tasnia hiyo.

Isha aliadhimisha miaka hiyo kupitia tamasha lililofanyika Oktoba 24, 2026, lililowakutanisha mashabiki wa Taarab na wadau wa burudani.