Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isha mashauzi aibuka na gauni la harusi

AISHA Pict

Muktasari:

  • Gauni jeupe lenye shela, wimbo Nani Kama Mama na dua kwa wazazi wake vilikuwa miongoni mwa matukio yaliyotofautisha shoo hiyo ya maadhimisho ya miaka 20 ya Isha Mashauzi katika muziki wa Taarab.

MWIMBAJI wa Taarab, Isha Mashauzi, aliwashangaza mashabiki alipoingia ukumbini akiwa amevalia gauni jeupe lenye shela, lililompa mwonekano wa bibi harusi katika shoo ya kuadhimisha miaka 20 ya safari yake ya muziki.

Isha alifafanua mapema kuwa vazi hilo halikuwa na maana nyingine zaidi ya ubunifu wake wa mavazi, akiwataka mashabiki kutolitafsiri tofauti na alivyokusudia.

Akizungumza na watu waliokuwa ukumbini, Isha alisema: “Msinishangae sana, ni ubunifu tu wa mavazi.”

ISH 01

Baada ya hapo, msanii huyo alianza kutumbuiza kwa wimbo wake Nani Kama Mama, uliogeuka kuwa sehemu ya kumbukumbu za kihisia alipowakumbuka wazazi wake wote wawili, ambao wamefariki dunia.

Akiwa jukwaani, Isha aliwaombea dua wazazi wake huku akieleza kuwa angependa wangekuwepo kushuhudia maadhimisho hayo muhimu ya miaka 20 ya muziki wake.

Tukio hilo liliupa usiku huo mguso wa kipekee, likiunganisha ubunifu wa mavazi, burudani na kumbukumbu za watu waliokuwa na nafasi kubwa katika maisha ya mwimbaji huyo.

ISH 02

Kwa Isha, maadhimisho hayo hayakuwa tu fursa ya kusherehekea safari yake ya muziki pamoja na mashabiki, bali pia wakati wa kuwakumbuka wazazi wake na kutambua mchango wao katika maisha yake.

Gauni jeupe lenye shela, wimbo Nani Kama Mama na dua kwa wazazi wake vilikuwa miongoni mwa matukio yaliyotofautisha shoo hiyo ya maadhimisho ya miaka 20 ya Isha Mashauzi katika muziki wa Taarab.